Safari_ni_Safari
JF-Expert Member
- Oct 5, 2007
- 23,265
- 17,120
Hakika ninayo furaha kuiona Tanganyika ikitajwa kwenye rasimu ya katiba mpya,ni ishara kubwa Tanganyika itarejea na kurejea kwake kutarejesha TANU maana Afro shiraz itarejea kwao za Zanzibar na CCM kufa kimiakimia.ooh karibu TANU uturejeshee utu wetu,uzalendo wetu,upendo wetu,aridhi yetu,madini yetu,elimu yetu na maendeleo yetu na utuondolee wanasiasa wanafiki waliosajili vyama kwa ajili ya matumbo yao na ndg zao huku wakijiita wakombozi,kumbe ni wezi wa mchana.karibu TANU,Karibu Tanganyika Uliyetuletea Uhuru wetu.
tatizo sio kuvunja muungano. bali ni namna ya kuuvunja tuna madeni ya taifa, tuna mipango ya maendeleo ya muda mrefu na sasa ina zaidi ya miaka 20 na inaendelea, kutakuwa na mabadiliko ya majengo ya mabalozi nchi zote m kiti cha umoja wa mataifa vitatakiwa viwili, kuna fungu benki kuu la kugawana na kugawana majeshi na polisi walioko kwenye ajira moja ya muungano yenye pension namafao tofauti. NADHANI KINACHOWATESA NI NAMNA YA KUUVUNJA SIO KUSEMA TU NENO TUVUNJE AU KURA ZA WANANCHI SIO TATIZO. pia na suala la kiusalama hawa wenzetu znz wanaweza kugeuka somalia tukapata maumivu kama wanayoyapata kenya.
Hakika ninayo furaha kuiona Tanganyika ikitajwa kwenye rasimu ya katiba mpya,ni ishara kubwa Tanganyika itarejea na kurejea kwake kutarejesha TANU maana Afro shiraz itarejea kwao za Zanzibar na CCM kufa kimiakimia.ooh karibu TANU uturejeshee utu wetu,uzalendo wetu,upendo wetu,aridhi yetu,madini yetu,elimu yetu na maendeleo yetu na utuondolee wanasiasa wanafiki waliosajili vyama kwa ajili ya matumbo yao na ndg zao huku wakijiita wakombozi,kumbe ni wezi wa mchana.karibu TANU,Karibu Tanganyika Uliyetuletea Uhuru wetu.
Mkuu naheshimu hisia zako na maoni yako fika, Lakini nachokijua mie kuwa " Zama (zamani) hairudi nyuma "Hilo ndio CCM hawalitaki maana ukiuwa muungano na yenyewe inakufa....hail TANGANYIKA you all!
By kimboka one
Hakika ninayo furaha kuiona Tanganyika ikitajwa kwenye rasimu ya katiba mpya,ni ishara kubwa Tanganyika itarejea na kurejea kwake kutarejesha TANU maana Afro shiraz itarejea kwao za Zanzibar na CCM kufa kimiakimia.ooh karibu TANU uturejeshee utu wetu,uzalendo wetu,upendo wetu,aridhi yetu,madini yetu,elimu yetu na maendeleo yetu na utuondolee wanasiasa wanafiki waliosajili vyama kwa ajili ya matumbo yao na ndg zao huku wakijiita wakombozi,kumbe ni wezi wa mchana.karibu TANU,Karibu Tanganyika Uliyetuletea Uhuru wetu.
Yaani hapa tumeshachanganywa na kukorogwa, hatujui hata kusini au kaskazini ni wapi! Mara wengine wanaikubali, mara wengine sio yote, mara wengine sijui nini... I don't see how we are going to get organized in this f***n business...
Kwa vyovyote vile, kama wataendelea kung'ang'ania hili limuungano lao, 2014 rasimu inapigwa chini kwenye kura ya maoni... wakilirudisha tena, tunaipiga chini tena... eeh, tuone watafanya nini. Sijui wataamua kutagaza kuwa mchakato wa katiba umeahirishwa hadi tutakapotangaziwa tena?!!!
Maana watu wanajitia kuwasemea watanzania kuwa tunapenda muungano!!! Nani kasema?
Kukata mzizi wa fitina, watupe hii kura ya referendum tujue moja na kila mmoja arudi majumbani kwake akijua wananchi wengi wanataka nini.Serikali ziwe mbili. Ya Tanganyika, na ya Zanzibar... Bora tuanze upya...
Mkuu naheshimu hisia zako na maoni yako fika, Lakini nachokijua mie kuwa " Zama (zamani) hairudi nyuma "
Sidhani kama TIME inajirejesha awali nyuma.
kama upo uhai Tupo tutona.
Kitu cha kushangaza ni kuona kuwa vyama vyetu vya siasa pamoja na asasi zimerukia hii bandwagon ya serikali tatu kana kwamba huu ndiyo muarobaini wa matatizo ya muungano wakati kiini cha tatizo na mazingira ya kisiasa kwa sasa hayawezi kutatuliwa na kuwepo kwa serikali tatu achilia mbali gharama za kuziendesha.umegusia ukweli japo ni kidogo mkuu, dudu muungano tukiling'ang'ania madhala yake yanaweza kuwa mabaya siku za usoni! tunaweza zalisha vikundi vya upigania uhuru, tuwe tayari kushuhudia mabomu yakilipuliwa, kwa kutumia charisma! madhala ya kutotaka kuongelea muungano yanaweza kuwa mabaya na makubwa!
kwa upande wa CCM wanawakalilisha vijana wao kuwa muungano uliopo unafaa, pasi kuangalia viashiria tulivyoanza kuvishuhudia! vijana wanacopy ideal za zamaani saana! nimemsikia kijana mmoja kwenye tv akichemka!
suala wanalotetea wale wanaopenda mfumo wa sasa uendelee ati ni ghalama za uendeshaji wa serikali itakuwa kubwa, they dont state upande gani utazidiwa na ghalama! kwa upande wa tanganyika kwa mtazamo wangu ghalama zitapungua tuu! hebu fikiria watanganyika tumekopa mpaka mawaziri kwa wenzetu! kwa ghalama zetu, achiambali mlalahoi wa bara kumlipia umeme wenzetu! tena wengine wenye uwezo! hebu tuangalie kwakina hoja zetu!
Kijana haujatafakari vizuri bali umekalili nani aliwahi kusema nini. tunachotaka wewe utushawishi nacho ni hoja yako ya referendum ina faida gani ukilinganisha na hoja iliyoletwa mbele yetu. Maana naamini muungano wa wazazi wako uliukuta hata kama baba na mama wanagombana kila siku huwezi kuja mtoto kuitisha referendum ya kujadili muungano wa wazazi wako. hii ni kwa sababu muungano unafaida kuliko matatizo yanayojitokeza ndani yake ambayo yanaweza kujadiliwa na kutatuliwa. naamini watanzania wote tutasapoti maboresho ya muungano labda anayetaka kutushawishi aje na hoja za kutuambia tunapata hasara gani ndani ya muungano ambazo tunaweza kuzieupuka nje ya muungano na alinganishe na faida tunazozipata ndani ya muungano ili tuangalie uzito mkubwa uko wapi. muungano si wa mtu au kundi Fulani bali muungano ni wa watanzania hivyo tushawishiwe kwa hoja zinazochambua watanzania sio kundi Fulani lilikuwa hivi au mtu Fulani alisema hivi.
Walivunja azimio la Arusha ambalo lilikuwa na impact kubwa kwa mstakabali wa taifa letu, wanashindwaje kuvunja muungano ambao hata faida yake haionekani. Nchi zilizokuwa nchi moja hapo zamani kama Ethiopia na Eritrea, Sudan na Sudan kusini, zinatengana, iwe ajabu kwetu ambaye unaunganishwa na nchi mbili huru?
Muamerika aitwaye H.P. Lovecraft aliwahi kusema, The oldest and strongest emotions of humankind is fear, and the oldest and strongest kind of fear is fear of the unknow.
Sisi hatutakuwa wa kwanza katika dunia hii na kuna mifano ambayo pamoja na muungano kuvunjika, nchi zimeweza kupiga hatua mbele za kimaendeleo. Nchi nyingi za ulaya ya mashariki ziliweza kuachana na zimeweza kusonga mbele.
Kibaya zaidi, muungano umekuwa kama ni siri ambaye wananchi wa kawaida hawatakiwi kuuchimba ili kuufahamu kwa undani zaidi ya kupata dodoso za hapa na pale kutoka kwa wanazuoni mbali mbali.
Kwa nini sisi tuwe tofauti na nchi zilizofanikiwa baada ya kuachana na muungano.