Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ni kweli, lakini bado wanatuwakilisha. Na hata mbunge akichaguliwa, huwakilisha waliomchagua na wasio mchagua.Hao wabunge hawakuchaguliwa na wananchi, bali walichaguliwa na hiyo hiyo serikali, ndio maana wanalinda maslahi ya serikali. Usitake kutuletea story za kutuvuruga boss.
Kama tuliweza kukubali serikali kutuchagulia wawakilishi wa kuisimamia, basi hili la tozo ni dogo sana. Tutulie tu.Aise! Wabunge wa sasa wa CCM walipewa uwakilishi na wananchi gani wakati walipewa Ubunge na Mwendazake kwa kutumia Tume ya Uchaguzi ya CCM na Vyombo vya ulinzi na usalama wa Taifa?
Ni kweli, lakini bado wanatuwakilisha. Na hata mbunge akichaguliwa, huwakilisha waliomchagua na wasio mchagua.
Waliongelea banaKuna wapumbavu wengine wanailaumu chadema eti ni kwa nini hawapazi sauti
Kamanda kwanza nikupe salute. Umenena vyema. Kati ya comment jamii forum ww unatakiwa upewe tuzo. Niliandikaga ujumbe kama huu kuna baadhi ya watanzania waliishia kuponda kuwa mbona inaniuma sana na wengine wakitoa vi like tu bila ku comment.wawili tu waka support... huo ndio ukweli wenyewe. Let's learn in a hard way kwa ujinga wetu!
Nendeni kwenye mikutano ya kisiasa/kampeni mkasikilize na kuchuja sera na ilani - hatuna nafasi sisi!
Someni sera za vyama na ilani zao mpate mwanga wa jinsi zitakavyosaidia au kuumiza maisha yenu watanzania - hayatuhusu sisi!
Fuatilieni vyombo vya habari mjue yanayojiri nchini na Bungeni kwa manufaa ya maisha yetu na vizazi vyetu - mambo ya wanasiasa hayo!
Sikilizeni hotuba za viongozi wa kisiasa na kuzichambua kwa umakini - fiesta iko mtaani leo!
Kutakuwa na mikutano ya kisiasa kuhusu Katiba Mpya - hayatuhusu, tumpigie kura Diamond ashinde!
Jamani saa mbili usiku wekeni taarifa ya habari kuna jambo zito la kitaifa - kaangalie chumbani kwako na mkeo sisi tunaangalia mchezo!
Siasa ndio kila kitu ndiyo inayoamua maisha yetu ila ndicho kitu kinachopuuzwa zaidi na watanzania! Unapopuuza siasa unapuuza maisha yako hivyo tusilalamike wala kumsingizia mtu; ni matokeo ya upumbavu wetu wenyewe!
Wewe una mbunge uliyempeleka bungeni? Ninachojua, hao unaowaita ni wabunge, hawawawakilishi wananchi, waliteuliwa na marehemu, kuanzia kwenye kura za maoni ndani ya CCM.Wabunge ni wawakilishi wetu. Tumewapeleka wakaisimamie serikali kwa niaba yetu. Kama wawakilishi wetu wamekubali maana yake tunaowakilishwa tumekubali.
Kama hawa wawakilishi wameenda kukubali kitu ambacho hatujawatuma, tuwalalamikie wao na kuwawajibisha na si serikali. Zaidi ya hapo tutulie.