Watanzania tulikubali suala la tozo mpya za miamala halafu leo tunaanza kulalamika!

Aise! Wabunge wa sasa wa CCM walipewa uwakilishi na wananchi gani wakati walipewa Ubunge na Mwendazake kwa kutumia Tume ya Uchaguzi ya CCM na Vyombo vya ulinzi na usalama wa Taifa?
 
Hao wabunge hawakuchaguliwa na wananchi, bali walichaguliwa na hiyo hiyo serikali, ndio maana wanalinda maslahi ya serikali. Usitake kutuletea story za kutuvuruga boss.
Ni kweli, lakini bado wanatuwakilisha. Na hata mbunge akichaguliwa, huwakilisha waliomchagua na wasio mchagua.
 
Aise! Wabunge wa sasa wa CCM walipewa uwakilishi na wananchi gani wakati walipewa Ubunge na Mwendazake kwa kutumia Tume ya Uchaguzi ya CCM na Vyombo vya ulinzi na usalama wa Taifa?
Kama tuliweza kukubali serikali kutuchagulia wawakilishi wa kuisimamia, basi hili la tozo ni dogo sana. Tutulie tu.
 
Ni kweli, lakini bado wanatuwakilisha. Na hata mbunge akichaguliwa, huwakilisha waliomchagua na wasio mchagua.

Wanawalisha kwenye hii kupitisha tozo ya kufuru?
 
Kamanda kwanza nikupe salute. Umenena vyema. Kati ya comment jamii forum ww unatakiwa upewe tuzo. Niliandikaga ujumbe kama huu kuna baadhi ya watanzania waliishia kuponda kuwa mbona inaniuma sana na wengine wakitoa vi like tu bila ku comment.wawili tu waka support
 
Wewe una mbunge uliyempeleka bungeni? Ninachojua, hao unaowaita ni wabunge, hawawawakilishi wananchi, waliteuliwa na marehemu, kuanzia kwenye kura za maoni ndani ya CCM.
 
Utawawajibisha wabunge vip wakati katiba haitoi hiyo nafasi.Kwa katiba hii ata tuwe na wabunge vihiyo kiasi gani hatuna chakuwafanya hadi miaka mitano ipite.Ndo maana wenye haja wanaona huitaji wa katiba mpya itakayoweza kuweka utaratibu wa wananchi kumwajibisha mwakilishi wao pale wanapoona hakidhi vigezo anapokua tayari ni mbunge.Kwa bunge hili la sasa tutegemee maumivi yakutosha maana kamwe huwezi kupata jambo jipya la kuinufaisha nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…