Mathanzua
JF-Expert Member
- Jan 4, 2017
- 17,251
- 22,929
Niliposikia kwa mara ya kwanza kwamba hii Sinema ya Royal Tour (ambayo Rais wetu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ni Main Actor and Tour Guide) ina assert kwamba kifo cha Hayati John Pombe Magufuli kimesababishwa na Covid, nilistuka na sikuamini masikio yangu!Kwa maoni yangu hii inam-compromise sana Rais Samia ambaye ndiye aliyetutangazia kifo cha Hayati Magufuli na kutufahamisha kwamba kilichomuua Rais Hayati Magufuli ni Ugonjwa wa Moyo! Sasa haya ya COVID-19 yametoka wapi tena?!
Najiuliza
a) Hivi Rais Samia alikubalije kushiriki sinema inayopotosha taarifa ya serikali kuhusu jambo zito kama hili?!
b) Kwa nini hakudai hicho kipande kiondolewe?!
Sitashangaa sana akitokea "mtetea chochote" akisema Rais Samia hakuiona script na kujiridhisha kwamba script ipo sahihi(if it is all acceptable) kabla ya uzinduzi wa movie huko Marekani! That would be a serious blunder and an act of gross incompetence on the part of her presidential advisers.
Kwa maoni yangu anayeongea kwenye hii script ni "Spin Master", na utetezi wake umekaa kipuuzi na hauna mashiko. Ashakum si matusi.
Iwapo anachosema "Spin Master" ndiyo hoja na majibu ya serikali (kwamba kilichosemwa kuhusu sababu ya kifo cha Magufuli ni COVID-19 ni kauli ya Wanaharakati (ambao wanatajwa kwa majina), mimi naomba kuuliza mbona sasa hawakusema (kwenye hiyo sinema ya Royal Tour) kwamba "kuna na Watanzania wengi wengine (na hata watu wa nje), ambao wanaamini Rais Magufuli kauawa?
Rais Samia aliwahi kuwakemea kwa hasira wanaodai Hayati Rais Magufuli kauawa.Akasema wenye ushahidi kwamba Hayati Rais Magufuli kauawa wampelekee.
Baada ya sinema ya Royal Tour kulikoroga, ni wazi sasa kwamba kumbe kweli kuna umuhimu wa kuunda Tume Huru ya kuchunguza kifo cha Rais John Pombe Magufuli. Wadanganyika tunataka kujua kwa uhakika: Je, Rais Magufuli alikufa kwa Ugonjwa wa Moyo (ambao haukusababishwa na mkono wa Mtu), alikufa kwa COVID-19 au aliuwawa?! Na alikufa lini exactly?
Naamini Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ataona umuhimu huu. Asipuuze hili, hasa ikizingatiwa kwamba yeye ndiye Main Actor and Main Guide in this movie that has come up with this act of not only gross disrespect for our late President but also explosive provocation directed towards our Nation and all Tanzanians!
Namshauri pia Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan awe mwangalifu sana kutambua kwamba kifo cha Magufuli kimeligawanya Taifa na hivyo afanye kazi ya ziada kutuunganisha badala ya kutugawa na kuruhusu Watu (na hasa) Viongozi kutonesha vidonda kila kukicha!
Kauli tata zimeshamiri nchini na zinaleta taharuki kila kukicha!
Mfano wa kauli tata!
a) "...ile ilikuwa Nidhamu ya woga tu!"
b) "Nchi imeharibiwa sana hii!"
c) "Sasa tunairudisha Tanzania Duniani!"
d) N.k.
Kwa bahati mbaya sana, kauli zinazotolewa kila kukicha kumkandia na kuchafua jina la Hayati Rais Magufuli zinachochea wasiwasi na hasira kwa baadhi ya Watanzania! Kama nilivyosema, zinaleta taharuki. Baadhi ya Wadanganyika tunajiuliza:
a) Kwa nini wenzie waliomo serikalini ndio wanaongoza mashambulizi?!
b) Kwa nini serikali ya Awamu ya 6 inaonekana ku-enjoy kuitupia madongo serikali ya awamu ya 5,yaani serikali ya Magufuli?
Strangely, by more than 90%, serikali ya awamu ya 6 ndiyo serikali ya awamu ya 5. Rais wa sasa ndiye alikuwa Makamu wa Rais Magufuli (na Mshauri wake Mkuu), Makamu wa Rais wa sasa ndiye alikuwa Waziri wa Fedha, Waziri Mkuu yuleyule, Mkuu wa Usalama wa Taifa yuleyule, IGP yuleyule, CDF yuleyule, Jaji Mkuu yuleyule n.k., n.k.
c) Kwa nini baadhi ya Viongozi wa serikali ya awamu ya 6 wanatoa matamshi ambayo yanaashiria kwamba kumbe (labda) walikuwa na Chuki kubwa kwa Rais, Mwenyekiti na Amiri Jeshi Mkuu wao, Rais Magufuli?!
d) Inakuwaje wale wote waliotofautiana na Rais Magufuli wamepandishwa vyeo na kauli zao na matendo yao yanaonyesha hawajutii walichofanya?! Ni kama vile wanatamba kwa "Ushujaa" wao wa kupambana na Rais Magufuli?! Wote tunazikumbuka zile audio clips...!!
e) Kwa nini baadhi ya viongozi wa "Matawi ya Juu" nchini wako bize kumbomoa Magufuli and his Legacy! Hivi hii well-coordinated attempt at "Character Assassination" ina lengo gani na faida gani?! Imesababishwa na nini?
f) Kwa nini serikali na Chama hamumtetei Magufuli?! Saa zote ni kimya au mashambulizi tu! Kwa nini???
g) Hivi mmesahau kwamba mwenzenu amepumzika na hana tena Uwezo wa Kujitetea?
h) Hivi mmesahau kwamba Hayati Rais Magufuli ameacha Mke na Watoto ambao mnawaumiza sana kwa Mashambulizi yenu na/au kimya chenu? Kwa nini msiwaache walau wakauke machozi? Hivi mnasahau kwamba wao ni Bin Adam na wanawashangaa sana, to say the least?
Hivi ni sawa kweli kwamba Serikali, Chama Tawala, Wabunge, Mawaziri, Taasisi mbalimbali, Jumuia mbalimbali (mfano: UV-CCM, UWT, Wastaafu, n.k.) wote mko kimya kabisa kila Hayati Magufuli anavyotukanwa na kudharirishwa?! Eti hata Viongozi wa Dini nao mko kimya! Mbona haiingii akilini?! Unafiki huu, mmm. Au labda ni ukondoo tu?! Au ni guilty consciousness?!
Sasa kama Magufuli alikuwa Rais mbaya kiasi hicho (which I don't believe anyway), inawezekanaje nyinyi washirika wake wote muwe wasafi kiasi hicho cha kuthubutu kumtupia mawe mazito hivyo Mwenzenu?
a) Collective Responsibility iko wapi?!
b) Hivi nyie wengine mnaponaje?!
c) Hivi mnajua kwamba kwenye sheria za kimataifa iliwekwa precedent kwenye Nuremberg Trials (baada ya Vita Kuu ya Dunia)? Kesi za Washirika wa Hitler. Kwa kifupi, Mahakama ya Kimataifa iliamua kwamba Rais/Kiongozi Mkuu hawezi kuwa Shetani na Mawaziri/Wasaidizi wake wote wakawa Malaika. Never!
d) Mbona mnatufanya wadanganyika mafala?
e) Mbona mnajichanganya hivyo?!
Narudia!
a) Wasiwasi na hasira za Wadanganyika zinasababishwa na mengi,na sina shaka yeyote kwamba siku moja sitakuja kuzaa matunda.
b) Mungu anayajua maovu yetu yote,huwezi kuficha,na hukumu zake ni za kweli.
c) Tusicheze na moto!
MUNGU IBARIKI TANZANIA!
Zaidi hapa👇