Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Watanzania,
Sote naamini tunaendelea kufuatilia taarifa ambayo imeisimamisha Dunia nzima na kuitikisa pamoja na kuteka vyombo vyote vya habari na mitandao ya kijamii ulimwenguni kwote kunakotokana na kupigwa risasi na kujeruhiwa kwa Donald Trump Rais mstaafu wa Marekani na mgombea Urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Republican alipokuwa akihutubia jukwaani huko Pennsylvania.
Taarifa za kupigwa kwa Donald Trump zimewashitua sana wamarekani na kuwaunganisha wanasiasa wote wakubwa Nchini humo wale wa Democratic na Republican,katika kulaani tukio hilo na kusema kuwa Marekani siyo mahali pa siasa za vurugu .Rais Bideni pia amelaani sana tukio hilo la kupigwa risasi kwa Mpinzani wake huyo Mkuu.
Tukio hilo limewakumbusha mbali sana hasa kwa kuzingatia kuwa wamarekani wamewahi kupoteza Marais wao baada ya kupigwa Risasi.na kwa mara ya Mwisho ni kwa John F Kennedy aliyepigwa risasi miaka ya 60 ambaye alifariki Dunia.
Sasa nataka kuwaulizeni Watanzania mmejifunza nini kupitia tukio hilo? Mimi nimejifunza kuwa matukio ya aina hiyo yanaweza kutokea mahali popote pale na nchi yoyote ile bila kujali ni nchi maskini au nchi tajiri, linaweza kutokea hata kama nchi ina teknolojia ya kiwango cha juu au intelijensia ya kiwango cha kimataifa.
Embu fikiria Marekani yenye kila aina ya teknolojia ya kisasa, zana za kisasa, miundombinu bora, ujuzi na maarifa ya kila kitu lakini walishindwa kung'amua tukio hilo na kulizima kabla ya risasi kumpata mgombea Urais jukwaani.
Nimejifunza pia uharaka wa vyombo vyake vya ulinzi katika kumuokoa mtu kutoka eneo la tukio na kumkabili adui, maana adui aliuawa palepale lakini ukiangalia namna walinzi walivyokimbia haraka kwenda kumzingira Trump pale jukwaani huku wengine wakiendelea kulizunguka jukwaa zidi ya adui, namna walivyokuwa wakimtoa jukwaani na kumkimbiza haraka kwenye gari na walivyojipanga kimapambano lile eneo.
Umahiri wa kumtungua adui bila kupiga risasi hovyo hovyo ambazo pengine zingeleta madhara kwa wengine, lakini pia umakini wa kutumia Risasi na silaha zao maana walinzi wale walijibu mapigo kwa kumuelekea adui na siyo kupiga risasi zisizo na maana au kuleta taharuki zaidi.
Lakini pia namna watu waliokuwa mkutanoni walivyokaa chini kwa uharaka sana kujihami, hapa ni somo zuri sana maana kama wangeamua kukimbia huku na huku pengine kungetokea maafa au vifo vingi kutokana na kukanyagana .lakini wamarekani wale nimeona wote walilala chini kwa haraka sana huku vyombo vyao vikimkabili adui kwa uhodari mkubwa sana.
Lakini pia watanzania hususani wanasiasa tuwe wasikivu sana pale vyombo vya ulinzi hususani Jeshi la polisi linapowanyima kibali chama kufanya mkutano sehemu fulani kwa sababu ya taarifa za kiintelijensia kwa sababu za kiusalama.
Kwa sababu nimekuwa nikiona baadhi ya vyama hususani CHADEMA wakinyimwa kibali kwa sababu ya intelijensia au taarifa kuonyesha viashiria vya uvunjifu wa amani au hali kutokuwa shwari au kutokea kwa uvunjifu wa amani. CHADEMA huanza kuleta kukejeli au kutoa lugha za dharau au ujuaji.
Mwisho tuache kuitupia lawama Serikali kwa kila jambo kuwa imehusika. Hii ni kwa kuwa unakuta mtu kapotea au kakutwa na majereha halafu watu kwa mihemuko wanaanza kuropoka kuwa Serikali imehusika, jambo ambalo unakuta hawana ushahidi wala uthibitisho wa aina yoyote ile ambao unaweza kutolewa mahakamani.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa,Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Pia, soma=> Marekani: Donald Trump ajeruhiwa kwa risasi akihutubia mkutano wa hadhara