Watanzania tumekataa kufa njaa na corona tunapambana nayo

Watanzania tumekataa kufa njaa na corona tunapambana nayo

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2015
Posts
36,900
Reaction score
52,056
Corona ilipoingia duniani iliwaambia watu wafanye uchaguzi wako tayari kufa kwa corona au njaa? Waliochangua njaa wakaji-lockdown ili wasife kwa corona, wafe njaa.

Watanzania tukasema No; kufa njaa ni kujitakia. Tukifa njaa hata Mungu atatuona wajinga ndio maana hatuku-lockdown watu wala uchumi.

Pili kama una njaa utapambana vipi nguvu za immunity mwilini huna na pesa huna? Hata wabunge wa Chadema na Zitto Kabwe walienda lockdown baada ya posho zao za bunge shilingi milioni 110 kuingia kwenye akaunti zao.Baada ya kuwa na uhakika wa chakula yaani food security ndio wakajilock down

Ukiwa umeshiba na pesa unayo hapo kupigana na corona unakuweza hata immunity mwilini inakuwemo sababu mwili umeshiba virutubisho vya kila namna unakuwa corona proof.

Uchumi tunaujali tusife njaa na corona tunapambana nayo. Tunapigana vita zote kwa mpigo
 
Officially MaFisiem MNAKIRI Mmefukarisha Watanzania Kwa Miaka 60 Mpaka Sasa Hata Mlo Wa Siku 2 Hawana, Wanategemea Watafute Ndio Wale.

Story Zote Za Sisi Matajiri Wa Kipato Cha Kati Hakuna Tena.
Watanzania Masikini Wa Kutupa Hohehahe.

Hata Zile Mbwembwe Za Akiba Ya Pesa Za Kigeni Za Kuhudumia Nchi Miezi 6 Bila Kufanya Kazi Kitu Ambacho Hakiwahi Kufanywa Na Marais Waliopita Hazipo Tena.

Anyway, Binafsi Najua Mtu Hohehohe Anaetoka Ili Ale Ndio Anatakiwa Kulinda Afya Yake Kuliko Mboni Ya Jicho.

Kama Wewe Ni Hohehohe UNatoka Ili ULE, Ukipuuza CORONA Ikakudaka Ukaugulia Ndani, UTAKULAJE SASA WAKATI KUNYANYUKA UKAFUTE TENA HUWEZI Wakati Afya Yako Ndio Mtaji Wako ?
 
Sijui kwa nini mna pokea misaada wakati hamtaki kuchukua measures kupambana na corona
 
Wewe kama serkali ya Magufuli isingekulinda ungekuwepo leo?

wee nae imenilinda kivipi kama hamna walilofanya kupunguza maambukizi..ni Mungu ndio ananilinda niko hai sio Magufuli..eboh
 
Ni hajizi na ajabu sana kwa zitto, mbowe na wengineo.

Tunajua kuwa wanasiasa hao wawili wanatafuta attention ya beberu's na huruma ya wananchi kuona serikali inafanya ovyo, lakini wajue wapo hapa hapa nchini na wanafaham mfumo wa wapiga kura wao wengi wanaishi vipi.

Huyo anayetaka tufungiwe ndani ili tupewe mkopo ndiye huyo huyo serikali ikichukua kesho anatoka mbele ya mic za waandishi, ...


"oooh tunakopa pesa za kazi gani"
"oooh hizo pesa zifanye kazi iliyokusudiwa"
"oooh mmewafungia watz ili mpate pesa"
 
Ni hajizi na ajabu sana kwa zitto, mbowe na wengineo.

Tunajua kuwa wanasiasa hao wawili wanatafuta attention ya beberu's na huruma ya wananchi kuona serikali inafanya ovyo, lakini wajue wapo hapa hapa nchini na wanafaham mfumo wa wapiga kura wao wengi wanaishi vipi.

Huyo anayetaka tufungiwe ndani ili tupewe mkopo ndiye huyo huyo serikali ikichukua kesho anatoka mbele ya mic za waandishi, ...


"oooh tunakopa pesa za kazi gani"
"oooh hizo pesa zifanye kazi iliyokusudiwa"
"oooh mmewafungia watz ili mpate pesa"
Watanzania hatuna akiki za kushikiwa kama nchi zingine duniani we are independent thinkers

Kwenye vita waweza kuwa na adui kibao unatakiwa upigane nao kwa mpigo .Adui wako wawili Wa corona na uchumi wrote wanatakiwa washambuliwe kwa pamoja not in isolation

Upande Wa kushoto watanziani tuna panga la kupigana na njaa na uchumi mkono Wa kulia tuna panga la kupigana na corona. ndio maana Raisi alisema tuombe mungu atusaidie sababu hats mitaifa mibabe kwa vita duniani kama marekani na China waneweka lockdown wameshindwa kupigana vita zote mbili kwa mpigo

Magufuli katuvusha kwenye vita ya dunia aendelee tu kutawala maraisi waliomtangulia walituvusha vita na majirani na makaburu Magufuli katuvusha vita ambayo hata ulaya China,Marekani na nchi wababe wa nchi za kiafrika hawaiwezi ya kupigana na maadui wawili kwa mpigo bila lockdown 2020 twende na Magufuli is good war commander than any president on Earth sasa hivi
 
Back
Top Bottom