Humu kuna thread inasema "Rais Samia atoa shilingi bilioni 300 kukamilisha ujenzi majengo ya Serikali Dodoma". Hii ilishamiri zaidi kuanzia awamu ya tano na hii ya sita ninaona kama inaendeleza kwa kasi sana.
Utakuta hata Diwani na Mwenyekeiti wa Serikali za Mtaa anapoongelea fedha zilizotolewa na Serikali au jambo lililofanywa na Serikali wanaliunganisha na kutendwa na Mheshimiwa Rais.
Hii kwangu mimi imekuwa inanisumbua. Badala ya kusema tu kuwa Serikali imefanya hili au imetoa fedha basi fashion imekuwa ni jambo hilo limefanywa na Mhe. Rais au kitu hicho kimewezeshwa na Mhe. Rais.
Watanzania tumekuwaje? Hivi tumeshindwa hata kuelewa kuwa wananchi ndiyo kila kitu na wapo juu hata ya Rais? We are the people to make or unmake the government.
Yaani kadri siku zinavyoenda tunashindwa sana kujitambua! Na Ndugai kuomba msamaha wa namna ile ndiyo katengeneza precedent mbaya kabisa.