Sir Robby,
Tatizo la watu wengi ni kuwa hawajui historia ya kweli ya uhuru wa Tanganyika.
Damu ya Waafrika ilimwagika kabla ya TANU kuundwa.
Tarehe 1 Februari, 1950, Dockworkers Union ilifanya mgomo mkali sana ambao wafanyakazi wa Bandari ya Dar es Salaam walipambana na askari wa kuzuia fujo waliotumwa na serikali kuvunja mgomo huo na askari 19 waliuliwa.
Historia ya Dockworkers Union inaanza mwaka wa 1947 na inaishia mwaka wa 1950 baada ya mauaji hayo.
Kiongozi wa Dockworkers Union Secretary General alikuwa Abdul Sykes akiwa na umri wa miaka 25 na nafasi hiyo alipewa na Waingereza lakini alijiuzulu kupisha shinikizo la mgomo na aliyechaguliwa kushika nafasi hiyo alikuwa Erka Fiah.
Yeye aliitisha mgomo uliosababisha mauaji na chama kupigwa marufuku.
Harakati hizi za Dockworkers Union na vyama vingine vya wafanyakazi vilitumika sana katika kusukuma agenda ya TAA kudai nchi pale Abdul Sykes alipochukua uongozi wa TAA 1950 kama Secretary General akitokea Dockworkers Union.
Hii historia nimeieleza kwa kirefu katika kitabu cha Abdu Sykes.
Inasikitisha sana kuwa mswada wa historia ya TANU ulioandikwa na Abdul Sykes na Dr. Wllbert Kleruu mwaka wa 1962 haujulikani uko wapi.
Hii nayo ni historia ya pekee iloyojaa mazonge mengi hadi kusababisha Abdul Sykes kujitoa katika mradi ule.
Sasa ikiwa wewe historia unayoijua ya TANU ni hii historia rasmi haya huwezi kuyajua.