Watanzania, tumpongeze Yusuf Manji kwa kuwa mzalendo na kurudi nyumbani. Rais Samia asichelewe, amuite Ikulu wazungumze

Utopolo kwenye ubora wenu
 
Kwani Manji ana changamoto gani? Alikuwa na changamoto na bashite na mwendazake tu!!!
 
Naunga mkono hoja kwa 100%
 
Upo sahihi kabisa mkuu
 
Sukuma Ganga wanune ama wacheke lakini hii ndiyo hali halisi - wajifunze maisha mapya ndani ya CCM..!! Welcome back home Mr. Manji... Yule mfuga paka kashaondoka ila paka bado yupo hana madhara yoyote kwa sasa.
Na ww PANYA jichunge sana utapitiwa na huyo paka unayemsema hahahahahah
 
Shudu
 
Kwanza jiulize alikwenda wapi? Huko alikokuwa ni kama nani. Ukishafahamu kwamba huyu ni mchumaji mali tu na kuondoka ndo utaelewa ujimnga wako. Kuna watu muna ujinga wa kudumu! Yaani nchi ya watu milioni 60 inahangaika na mtu mmoja. Muhindi! Unaamini Manji ni muhimu sana! unaamini Yanga ni kitu muhimu sana!
 
Na kama huko haliko kungekua kuna masali asingerudi.
 
Hawa waonee huruma tu! Kuna watu hapa wanaandika mambo hadi unaogopa gharama ya kuwa na akili ndogo. Mtu analeta thrd ya kumtetea Manji na usalama wake wakati yeye hajui hata ana usalama gani. ni ubwege tu unatusumbua.
 

Hakika Mkuu ,wafanyabiashara ni watu muhimu sana katika kuchangia uchumi wa nchi ,wao ndio wanaleta maendelea ,kitendo cha JIWE/DAB "Kumfanizia" manji ilikuwa haijakaa sawa.

Manji chonde chonde rudisha majeshi uje kuinua uchumi wa TZ....Washamba washaondoka serikalini.
 
Hawa ndio wale wenye pesa lakini hazijulikani zimetoka wapi.
 
Kama mwekezaji anarudi ni kiashiria kizuri kuelekea kuifufua sekta binafsi ili ishike nafasi yake kama injini ya uchumi wa nchi, na hivyo kuwa mwarobaini wa ajira kwa vijana, angalizo tu wawekezaji washirikiane na serikali kwenye kutoa kodi na tozo stahiki ili kusitokee rabsha ambazo wakati mwingine huleta sintofahamu za hapa na pale.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…