Watanzania tumtumieni Rais Magufuli vizuri, Akiondoka tutamkumbuka sana

small mind

Senior Member
Joined
Jun 1, 2012
Posts
129
Reaction score
58
Najua kuna watu ambao hawataelewa ninachotaka kusema ila wacha niseme tu.

Tangu wamau ya kwanza watu wamekuwa wakisubiri tu siku watakapopata kiongozi bora atakayeleta neema.Enzi za baba wa taifa watu hawakumtumia vizuri alipoondoka akaja Mzee ruksa akafanya yake naye watu hawakumtumia vizuri akapita akaja Mzee Mkapa,kisha Kikwete na sasa Magufuli.

Viongozi wote hao walikuwa na mazuri na mapungufu yao ila sasa wengi wetu badala ya kutumia yale mazuri yao vizuri ila kuhakikisha tunapiga hatua kati a maisha yetu na taifa letu tulifanya makosa tunayofanya sasa ya kubeza bila kutumia fursa zilizopo

Niseme tena jamani watanzania,Rais wa sasa ndo huyu, changamoto zake tumezijua na fursa zake tumeziona kwa hio basi ili tusonge mbele ni vyema tukamtumia ipasavyo.Kama tuna mambo tunataka yanyooke katika biashara, sheria, haki, uchumi n.k. na ambayo hayana majungua majungu na kejeli basi ni wakati wa kuyafikisha kwake kwa njia yoyote ile ili ayafanyie kazi.

Kama ni suala la elimu basi tujenge hoja ya kile tunataka kifanyike kuboresha elimu yetu na kwa hakika atachukua hatua.Kama ni huduma za afya, ulinzi na usalama,mawasiliano,biashara,uchumi n.k..tuseme kwa nguvu kubwa na sauti kubwa kile tunachotaka ambacho kitafanya maisha yako,ya watoto wako na taifa kwa ujumla wake liwe bora zaidi tuseme.

Kama kuna kero ya barabara mtaani kwenu simameni kwa pamoja mseme,jengeni hoja tumieni mitandao ya kijamii kuonesha tatizo na kushauri nini kifanyike na Rais wetu atafanya.kama ni tatizo la ajira jiungeni pamoja,ibueni miradi semeni changamoto zenu na rais wenu atafanya.Narudia tena kusema kwamba MTUMIENI HUYU MZEE KABLA HAJAONDOKA KWANI MTAMKUMBUKA SANA.

Msikae tu ksema kuhusu madhaifu yake na kumfrustarte kwa sababu ana ngozi laini kwa sababu hiyo haitaleta maendeleo yoyote.Narudia tena ibukeni semeni kila mnachotaka na mpendwa wetu JPM atafanya. Akiondoka Mtamkumbuka kwani hamjui ataekuja baada yake atakuwa na wajihi gani.

Mimi nimesema tu kwa atakenielewa anajua nini cha kufanya kwa wale ambao wanafikiri kila kitu ni siasa au mapenzi piteni kimya wala msisome huu uzi wa la kuchangi ila kwa wale mnaojua maana chukueni hatu mapema kwani akiondoka ni vigumu kumpata mwingine kama yeye na kwa hakika mtatamani arudishwe ila ndo basi tena awamu yake itakuwa imepita.

Wenu

SM
 
Wengi tutamkumbuka kwa dhuluma anazowafanyia watu.
Amewadhulumu wafanyakazi salary increments;
Amewadhulumu wakulima pesa zao;
Amewadhulumu wafanyabiashara kupitia TRA;
Sasa hivi ameanza kuwadhulumu wafanyabiashara wanaoidai serikali kihalali kutokana na huduma au bidhaa walizoiuzia serikali;
Anawadhulumu watoto wa nchi hii kwa kutoa elimu ya hovyo yeye akiita "elimu bure".
 
Dhulma ipi wewe ni Lijizi tu huna lolote
Watanzania waipendayo nchi hii lazima wamkumbuke Rais Magufuli
 
Nimesoma kichwa cha habari tu,utumbo wa ndani wa tumbo la kuhara sijausoma ila nikujibu tu kwamba HATUMTAKI MAGUFULI.
Ieleweke tu kwamba si kiongozi sahihi wa taifa hili hana maono,jana anazungumza eti world bank watatupa mkopo kwa sababu anazozijua na anaongea kwa vijembe baada ya masaa kadhaa world bank wanamjibu na kumwambia kuwa mkopo wamesitisha kwa sababu ya sera zake.
Harafu mtawazaji wake unakuja na kuleta uhalo hapa kwendaaaaaaaa.
2020 No Magufuli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wengi tutamkumbuka kwa dhuluma anazowafanyia watu.
Amewadhulumu wafanyakazi salary increments;
Amewadhulumu wakulima pesa zao;
Amewadhulumu wafanyabiashara kupitia TRA;
Sasa hivi ameanza kuwadhulumu wafanyabiashara wanaoidai serikali kihalali kutokana na huduma au bidhaa walizoiuzia serikali;
Anawadhulumu watoto wa nchi hii kwa kutoa elimu ya hovyo yeye akiita "elimu bure".
Mkuu mbona watu wanapewa increments za performance na kupandishwa madaraja kama kawaida?Ambacho ameondoa ni ilie ya kupandiha kima cha chini cha mshahara ambayo ilikuwa inasukuma sana inflation.Kama kuna uongo kwenye hili naomba mfanyakazi yeyote wa serikali aseme hapa kama watu hawapandishiwi mishahara kwa kutumia madaraja na utendaji kazi.
 
Mkuu kwenye hili wakulima ni changamoto iliyojitokeza katika kutaka kuwasaidia wasidhulumiwe zaidi.Jaribu kufikiria jinsi wakulima wa korosho walivokuwa wanaibiwa na Kangomba.Alikuwa na nia ya kuwasaidia wananchi tatizo ni kwamba wafanyabiashara walisusa kwa sababu walizoea kwa wakulima wanaweza kuwalalia wanavyotaka
 
Baada ya awamu ya Kwanza, Marais waliofuata wangesimamia Misimamo kama ya Magufuli tungekuwa mbali sana kimaendeleo, japo ufisadi haujaisha kabisa
 
Dhulma ipi wewe ni Lijizi tu huna lolote
Watanzania waipendayo nchi hii lazima wamkumbuke Raus Magufuli
Acha zako wewe. Unajifanya hujamsikia Polepole akisema CCM ina majizi ambayo yanalindwa na wakubwa zake? Yaani Katibu Mkuu na manaibu zake, Makamu mwenyekitì Bara na Visiwani pamoja na Mwenyekiti wenu. Hao ndo wakubwa wa Polepole na bila shaka ndio wanaolinda wezi wasitajwe.
 
Wengi tutamkumbuka kwa dhuluma anazowafanyia watu.
Amewadhulumu wafanyakazi salary increments;
Amewadhulumu wakulima pesa zao;
Amewadhulumu wafanyabiashara kupitia TRA;
Sasa hivi ameanza kuwadhulumu wafanyabiashara wanaoidai serikali kihalali kutokana na huduma au bidhaa walizoiuzia serikali;
Anawadhulumu watoto wa nchi hii kwa kutoa elimu ya hovyo yeye akiita "elimu bure".
Mkuu kwenye kodi,watu walikuwa hawalipi kodi,wanafanya biashara kwa ujanja ujanja na kukwepa kulipa kodi kubwa huku wakihonga watumishi wa TRA.Yeye kaamua kwamba kila mtu alipe kodi ili nchi ipate mapato halali sidhani kama unaelewa hilo mkuu.
 
Wengi tutamkumbuka kwa dhuluma anazowafanyia watu.
Amewadhulumu wafanyakazi salary increments;
Amewadhulumu wakulima pesa zao;
Amewadhulumu wafanyabiashara kupitia TRA;
Sasa hivi ameanza kuwadhulumu wafanyabiashara wanaoidai serikali kihalali kutokana na huduma au bidhaa walizoiuzia serikali;
Anawadhulumu watoto wa nchi hii kwa kutoa elimu ya hovyo yeye akiita "elimu bure".
Wafanyabishara gani ambao hawajalipwa na serikali?Wale ambao wanato rushwa ili wapate tender kisha wanatoa huduma ambazo ni substandard kwa sababu wana wau wao kwenye system na kisha wanpobanwa ndo wanaanza kudai kwamba serikali inataka kuwadhulumu?
 
Nitamkumbuka kwa kumshambulia TL kwa risasi 38
Mkuu swala la Tundu Lisu bado halijathibitika kwa hakika ni nani waliohusika.Binafsi nafikiri inawezekana kabisa waliofanya hivyo walitaka ionekane kwamba ni serikali ilifanya tukio hilo.Kulikuwa na njia nyingi za kumnyamazisha bila kutumia nguvu kubwa ila kwa sababu lengo lilikuwa kuleta taharuki waliamua kutumia mbinu hio chafu.Ni namna moja ya kulitazama hilo
 
Kweli wewe small mind

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kila mmoja ana mapungufu yake. Kiukweli, ukiacha suala la kukanyaga upinzani, this man is doing the best. Ni mmoja kati ya rais bora kabisa nchi yetu imewahi kupata tangu uhuru.
 
Najua kuna watu ambao hawataelewa ninachotaka kusema ila wacha niseme tu.

Tangu wamau ya kwanza watu wamekuwa wakisubiri tu siku watakapopata kiongozi bora atakayeleta neema.Enzi za baba wa taifa watu hawakumtumia vizuri alipoondoka akaja Mzee ruksa akafanya yake naye watu hawakumtumia vizuri akapita akaja Mzee Mkapa,kisha Kikwete na sasa Magufuli.

Viongozi wote hao walikuwa na mazuri na mapungufu yao ila sasa wengi wetu badala ya kutumia yale mazuri yao vizuri ila kuhakikisha tunapiga hatua kati a maisha yetu na taifa letu tulifanya makosa tunayofanya sasa ya kubeza bila kutumia fursa zilizopo

Niseme tena jamani watanzania,Rais wa sasa ndo huyu, changamoto zake tumezijua na fursa zake tumeziona kwa hio basi ili tusonge mbele ni vyema tukamtumia ipasavyo.Kama tuna mambo tunataka yanyooke katika biashara, sheria, haki, uchumi n.k. na ambayo hayana majungua majungu na kejeli basi ni wakati wa kuyafikisha kwake kwa njia yoyote ile ili ayafanyie kazi.

Kama ni suala la elimu basi tujenge hoja ya kile tunataka kifanyike kuboresha elimu yetu na kwa hakika atachukua hatua.Kama ni huduma za afya, ulinzi na usalama,mawasiliano,biashara,uchumi n.k..tuseme kwa nguvu kubwa na sauti kubwa kile tunachotaka ambacho kitafanya maisha yako,ya watoto wako na taifa kwa ujumla wake liwe bora zaidi tuseme.

Kama kuna kero ya barabara mtaani kwenu simameni kwa pamoja mseme,jengeni hoja tumieni mitandao ya kijamii kuonesha tatizo na kushauri nini kifanyike na Rais wetu atafanya.kama ni tatizo la ajira jiungeni pamoja,ibueni miradi semeni changamoto zenu na rais wenu atafanya.Narudia tena kusema kwamba MTUMIENI HUYU MZEE KABLA HAJAONDOKA KWANI MTAMKUMBUKA SANA.

Msikae tu ksema kuhusu madhaifu yake na kumfrustarte kwa sababu ana ngozi laini kwa sababu hiyo haitaleta maendeleo yoyote.Narudia tena ibukeni semeni kila mnachotaka na mpendwa wetu JPM atafanya. Akiondoka Mtamkumbuka kwani hamjui ataekuja baada yake atakuwa na wajihi gani.

Mimi nimesema tu kwa atakenielewa anajua nini cha kufanya kwa wale ambao wanafikiri kila kitu ni siasa au mapenzi piteni kimya wala msisome huu uzi wa la kuchangi ila kwa wale mnaojua maana chukueni hatu mapema kwani akiondoka ni vigumu kumpata mwingine kama yeye na kwa hakika mtatamani arudishwe ila ndo basi tena awamu yake itakuwa imepita.

Wenu

SM
Kwa kweli moja kati ya vitu ambavyo hatutakuja kumsahau ni

Bomoa bomoa kwa wakazi wa kimara na mbezi watu wengi wamekufa kwa presha
 
Mkuu mbona watu wanapewa increments za performance na kupandishwa madaraja kama kawaida?Ambacho ameondoa ni ilie ya kupandiha kima cha chini cha mshahara ambayo ilikuwa inasukuma sana inflation.Kama kuna uongo kwenye hili naomba mfanyakazi yeyote wa serikali aseme hapa kama watu hawapandishiwi mishahara kwa kutumia madaraja na utendaji kazi.
Si kweli mi mwenyewe ni muhanga pambafu
 
Back
Top Bottom