Watanzania tumuombee Dkt. Tulia Ackson Mwansasu ashinde Urais wa IPU

Halafu inamsaidia nini mtu wa kawaida kama mimi ?
 
Tulia ni Spika wa hovyo kuwahi kutokea katika historia ya nchi yetu. Kama kuna maombi yoyote ni kumchosa Mungu tu! Niambie lolote jema alilolifanya huyu Chawa wa serikali! Usituchose buree!
Kwani Ni spika yupi amewahi kuwa Bora kwenu? Maana kila spika akija na kuchaguliwa huwa mnasema maneno hayo hayo
 
Utadhani ni kama aliyeandika hapa ni Tulia mwenyewe! Hata hivyo haihitaji kumwombea ila ni jinsi gani atakavyojieleza mbele ya wale watakaompigia kura.

Ajinoe tu katika lugha ya Kiingereza! Harafu aachane na ndoto za kupita bila kupingwa kama siasa za huku Tanzania!

Harafu kule hakuna NEC itakayopindua matokeo ya kura na kumtangaza Yeye!
 
Uwezo wa Dr Tulia kujieleza Hilo ondoa Shaka kabisa,hawezi kutuangusha
 
Tutamuombea. Ila ndugu yangu uwe unafupisha habari zako. Ni ndefu sana huenda wanaosoma ni watu wachache.
Kuna watanzania wengi hawajui jinsi ya ku-transmitt message. Maneno mengi ujumbe mdogo tu. Kwa mfano huwa nafuatilia Youtube Channels za kitanzania unakuta wanaanza na maneno mengi irrelevant mpaka unachoka na kuhama channel kabla hata ya kusikia kilichokupeleka pale.
 
Utaratibu wa kumpigia kura upoje? Je wagombea wenzake ni wakina nani, sifa zao za utumishi wa umma zipoje, na wanotoka katika nchi zipi?

Tumuombee tu wapiga kura wasiweze kufahamu lolote lile kwa kina kuhusu umakini wake juu uendeshaji na usimamizi wa shughuli za kila kikao na mikutano ya Bunge letu. Bado hajafikisha hata miaka mitano ya kuwa Spika kamili wa Bunge. Asiingie katika kimyang'anyiro hicho kwa msukumo na vigezo vya wa uanamke wake ama elimu yake, bali kwa kipimo cha uzoefu, ufanisi, na umahiri wake katika nafasi hiyo anayoigombea, na pia kwa kujilinganisha na watia nia wengine.

Akitokea mpiga kura ambaye atamuhoji kuhusu anavyolishughulikia suala la uwepo wa COVID 19, umakini kuhusu azimio la Bunge juu ya mkataba na DPW lilivyoshughulikiwa, ama madudu yaliyosheheni katika ripoti ya CAG na umuhimu kuhusu haja ya kuwepo kwa dharura ya majadiliano juu yake bungeni.

Nia ipo, Je! Vipi kuhusu uwezo? Si kila mchungaji ana uwezo wa kukemea pepo na magonjwa vikamtii, ijapokuwa wote hufahamika kwa cheo ni wachungaji.
 
Itakuwa laana akishinda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…