Watanzania tumuombee Dkt. Tulia Ackson Mwansasu ashinde Urais wa IPU

Maskini, kumbe unalishwa na Tulia ndio maana kutwa kucha kuandika utumbo
Nalishwa na mikono yangu kupitia kazi za mikono yangu kwa kujituma na kufanya kazi kwa juhudi, maarifa na bidii.
 
Jimboni Hana mpinzani kabisa maana Wana Mbeya walishaamua kumsimka katika mioyo yao kuwa mbunge wao bilaa kikomo
Kumbe hata hapa Mbeya hujawahi kufika.
Kumbuka teuzi siku hizi kipaumbele Ni wa upande ule. Endelea kuwa chawa.
 
Jamani tusipoteze kura na spika ambaye ameiba kura tuwaachie wenye demokrasia ya kweli na waliochaguliwa kihalali badala ya kupoteza muda na huyu mapepe!

Bandari tu hapa mkataba kapitisha kwa kura ya ya jumla badala ya kura moja moja🤔 yaani mnatupotezea muda na watu ambao ni mudilisi wa nchi🤔

Sasa tuulize kafanya cha ajabu kipi bungeni mpaka tumpigie kura kwa lipi hasa??

Hivi huyu mapepe unaweza kumlinganisha na Dr Nshala kweli tukasema ni sawa. Tatizo tuna wanasheria vibaraka kama huyu dada
View attachment 2683525
Dr Tulia Ni zaidi ya mwanasheria ,Ni zaidi ya wakili. Huyu Dr Tulia Ni nguli kweliiii kweliiii katika uga wa Sheria.Ndio maana unaona akilisaidia Sana bunge na serikali katika masuala ya Sheria
 
Sisi sio punguani kama wewe usiye na akili hata moja, unawadhalilisha Wanyiha wote na ukoo mzima wa Mwashambwa kwa kuwa asshole sucker wa watawala.
Kupita na kushinda kwa Dr Tulia Urais wa IPU itakuwa Ni heshima kwetu Kama Taifa.ondoa Roho ya chuki na wivu wa kijinga
 
Tutamuombea. Ila ndugu yangu uwe unafupisha habari zako. Ni ndefu sana huenda wanaosoma ni watu wachache.
Anapalilia ili waone kumbe anapoteza muda kwa maneno mengi yasiyo na maana yoyote!

Kwa kifupi hizi ni mojawapo ya sifa za machawa. Kuongea sana na kuandika sana bila content yoyote ya maana.
 
Mwanangu huna vitu vya maana vya kuombea?
Kwani yeye hawezi kujiombea?
 
Ndugu zangu watanzania,

Kwa unyenyekevu na heshima kubwa Sana nawaombeni watanzania kila mmoja kwa Imani Yake Tumuombee Mh Dr Tulia Ackson mwansasu Ashinde Urais wa IPU yaani umoja wa mabunge Duniani. Dr Tulia Ni spika wa bunge letu ,mpaka Sasa anaendelea kupata uungwaji mkono kutoka maeneo mbalimbali ndani ya Bara la Afrika.

Dr Tulia Ackson mwansasu Ni Dada msomi wa Kiwango Cha juu na nguli wa Sheria ambaye amekuwa Naibu mwanasheria mkuu wa serikali nafasi aliyoitumikia kwa uaminifu na weledi wa Hali ya juu Sana.Nyota yake kisiasa ilianza kung'ara Mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa 2015 ,Ambapo alipata bahati ya kuteuliwa ubunge na aliyekuwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania awamu ya Tano Hayati Dr John Pombe Joseph Magufuli,Ambapo baada ya kuingia Bungeni kupitia mlango huo akapata bahati ya kuaminiwa na chama Cha mapinduzi kusimama Kama mgombea pekee ndani ya Bunge kuwania nafasi ya unaibu spika wa bunge letu na kufanikiwa kushinda kwa kishindo.

Aliongoza kwa mafanikio makubwa Sana,Ambapo ilipofika mwaka 2020 alitupa karata yake ndani ya CCM na kufanikiwa kushinda kwa kishindo katika kura za maoni ,na kupitishwa na kamati kuu ya CCM Taifa kupeperusha Bendera ya CCM Jimbo la Mbeya mjini,Ambapo alipita kwa kishindo kikuu na kurejea Bungeni Kama mbunge wa kuchaguliwa na wananchi na kupita Tena katika nafasi ya unaibu spika, na baadaye kuja kuwa spika wa bunge baada ya kujiuzulu kwa mh Job yuston Ndugai.

Dr Tulia Ni kiongozi mnyenyekevu Sana na mwenye moyo wa huruma na upendo Sana,ndio maana ukienda katika mkoa wa Mbeya hakuna mahali ambako hutakuta Alama za Dr Tulia,kila eneo utakutana na mikono ya Dr Tulia,kila sehemu utaona na kuonyeshwa juhudi na alama zake, Ni kiongozi aliyegusa maisha ya watu wengi Sana kuanzia yatima,watu wenye ulemavu ,wajane na wazee ame wasaidia Sana bila mipaka Wala kikomo,.vijana wengi Sana Mkoani Mbeya wamenufaika na kupata matumaini kupitia Dr Tulia,Ni yeye aliye wawezesha mamia kwa maelfu ya vijana mitaji ya kufungua biashara,ni yeye amewezesha mamia ya vijana kujipatia pikipiki mpya pamoja na bajaji bure kabisa kwa ajili ya kufanyia biashara na kusaidia familia zao na kuondokana na utegemezi wa kipato, Ni kupitia Dr Tulia vikundi vingi vya akina mama,vijana na watu wenye ulemavu walipatiwa mitaji ya kutosha,Dr Tulia ameleta nuru na Tabasamu kwa maelfu ya Wana Mbeya.

Dr Tulia ni Dada na kiongozi mwenye huruma Sana na msikivu wa Kiwango Cha juu Sana ,husaidia bila kujali eneo ,au Jimbo au mkoa .Ni kwa moyo wake huo wa upendo na huruma amewahi kusaidia mamia ya mabati katika shule ya msingi Mabatini inayopatikana katika mkoa wa songwe ,wilaya ya mbozi,mji mdogo wa mlowo,kitongoji Cha mabatini B.Alitoa msaada huo mkubwa kabisa bila kujali kuwa shule hiyo IPO katika mkoa na Jimbo jingine,akiwa na mh mbunge wa viti maalumu CCM mkoa wa songwe mh Juliana Daniel shonza walisaidia katika ukamilishaji wa vyumba vya madarasa yaliyo kuwa yanahitajika Sana kwa wakati huo.

Uongozi wa Dr Tulia umekuwa Ni kwa ajili ya kuwatumikia watu bila kujali itikadi za kisiasa,Wala eneo anakotokea mtu,maisha ya Dr Tulia yameleta furaha katika mioyo ya watu wengi Sana,amegusa maisha ya wengi Sana waliokuwa wamekata Tamaa na kuona Giza mbele Yao,siku zote amekuwa karibu Sana na watu,awapo jimboni au Mkoani Mbeya muda wote utamuona akiwa na wananchi wanyonge mitaani akitoa misaada ,utamuona muda wote akisaidia watu wenye Mahitaji maalumu,utamuona muda wote akisaidiana na viongozi wengine kutatua kero za wananchi,utamuona muda wote akiwatetea na kuwasemea Wananchi.

Ni kiongozi anayejuwa Nini maana ya maisha hasa kwa kuzingatia kuwa amekulia katika maisha magumu lakini akiwa na Imani IPO siku yatapita na Mungu atamgusa na kumuinua na siku moja atamfuta machozi mama yake na kugusa maisha ya watu wengine wenye kuhitaji msaada.Ni kiongozi asiye na kiburi Wala dharau wala ubaguzi na ndio maana husaidia Wote na kujumuika na wote ,Ni kiongozi mwenye kujishusha na kujinyenyekeza kwa watu,Ni mwenye hofu ya Mungu na mcha MUNGU Sana. Ni mwenye maadili mema na mwenye staha na heshima kubwa,anao uwezo mkubwa Sana wa kiuongozi na kiutendaji, anao uwezo wa kuwaunganisha watu na kujenga umoja na mshikamano,ndio maana kwa Sasa Mbeya haina mavurugu na badala yake inavuma na kusikika kwa maendeleo tu na miradi mbalimbali ya maendeleo inaendelea kuchipua na kufanyika .

Tufunge na kumuombea mtoto wetu, Dada yetu na kiongozi wetu Dr Tulia ili akashinde kwa kishindo na kutuletea heshima Kama Taifa kimataifa, Tuendelee kusimama Naye na kumpa faraja na nguvu za kusonga mbele. Itakuwa ni fahari kwetu watanzania akishinda uchaguzi huo unaofanyika mwezi October.Tumbebe katika mikono yetu na mioyo yetu kimaombi, Tumuombee kwa nguvu zetu zote na tuwashawishi wengine kutoka Mataifa mengine ili watuunge mkono kwa mtoto wetu wa kitanzania,Dada yetu imara ,msomi wa Kiwango Cha juu,mwenye msimamo usiyo yumba aweze kupita na kutuletea heshima.

Rai yangu Namuomba Dr Tulia dada yangu aendelee kumuomba mungu amtangulie katika safari hii ambayo sisi mamilioni ya watanzania tupo nyuma yake na tumembeba kimaombi, Aendelee kumtumainia na kumtegemea Mwenyezi MUNGU katika kila Hatua apigayo.viongozi wetu mbalimbali ngazi ya Taifa watumie ushawishi wetu kidiplomasia kumsaidia spika wetu kwa kila namna ikiwezekana hata viongozi wastaafu katika siasa katika ngazi mbalimbali wafanye ushawishi wa kidiplomasia kuhakikisha kuwa tunapata uungwaji mkono kwa Tulia wetu na kuzoa Kura za kutosha siku ya uchaguzi.mimi binafsi nitaendelea kumuombea Dada yangu kwa Imani yangu mbele za Mwenyezi MUNGU.

Kazi iendeleee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
Mxiew
 
Kwangu hii itakuwa matumizi mabaya ya maombi, yule Dada ana dharau sana. Je, akipata urais itakuwaje na katiba mbovu ambayo amekaa bungeni na wabunge wasio na chama na yupo very comfortable
 
Anawakilisha Taifa na hivyo Ni lazima Tumuombee,lakini pia maisha ya Dr Tulia kiutumishi yamegusa maisha ya watu wengi Sana na kuleta matumaini kwa mioyo ya wengi waliokuwa wamekata Tamaa,ndio maana anaendelea kuombea kila Kona ya nchi na Bara Zima la Afrika
 
Kwangu hii itakuwa matumizi mabaya ya maombi, yule Dada ana dharau sana. Je, akipata urais itakuwaje na katiba mbovu ambayo amekaa bungeni na wabunge wasio na chama na yupo very comfortable
Dr Tulia Ni kiongozi mnyenyekevu na mwenye hekima na busara ya Hali ya juu Sana,Hana ubaguzi Wala chuki na mtu,Hana makuu Wala Shari na mtu. Ni mtu wa watu na mwenye kuishi vyema na watu na kusaidia watu pasipo ubaguzi wa Aina yoyote Ile.
 
Ndugu zangu watanzania,

Kwa unyenyekevu na heshima kubwa Sana nawaombeni watanzania kila mmoja kwa Imani Yake Tumuombee Mh Dr Tulia Ackson mwansasu Ashinde Urais wa IPU yaani umoja wa mabunge Duniani. Dr Tulia Ni spika wa bunge letu ,mpaka Sasa anaendelea kupata uungwaji mkono kutoka maeneo mbalimbali ndani ya Bara la Afrika.

Dr Tulia Ackson mwansasu Ni Dada msomi wa Kiwango Cha juu na nguli wa Sheria ambaye amekuwa Naibu mwanasheria mkuu wa serikali nafasi aliyoitumikia kwa uaminifu na weledi wa Hali ya juu Sana.Nyota yake kisiasa ilianza kung'ara Mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa 2015 ,Ambapo alipata bahati ya kuteuliwa ubunge na aliyekuwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania awamu ya Tano Hayati Dr John Pombe Joseph Magufuli,Ambapo baada ya kuingia Bungeni kupitia mlango huo akapata bahati ya kuaminiwa na chama Cha mapinduzi kusimama Kama mgombea pekee ndani ya Bunge kuwania nafasi ya unaibu spika wa bunge letu na kufanikiwa kushinda kwa kishindo.

Aliongoza kwa mafanikio makubwa Sana,Ambapo ilipofika mwaka 2020 alitupa karata yake ndani ya CCM na kufanikiwa kushinda kwa kishindo katika kura za maoni ,na kupitishwa na kamati kuu ya CCM Taifa kupeperusha Bendera ya CCM Jimbo la Mbeya mjini,Ambapo alipita kwa kishindo kikuu na kurejea Bungeni Kama mbunge wa kuchaguliwa na wananchi na kupita Tena katika nafasi ya unaibu spika, na baadaye kuja kuwa spika wa bunge baada ya kujiuzulu kwa mh Job yuston Ndugai.

Dr Tulia Ni kiongozi mnyenyekevu Sana na mwenye moyo wa huruma na upendo Sana,ndio maana ukienda katika mkoa wa Mbeya hakuna mahali ambako hutakuta Alama za Dr Tulia,kila eneo utakutana na mikono ya Dr Tulia,kila sehemu utaona na kuonyeshwa juhudi na alama zake, Ni kiongozi aliyegusa maisha ya watu wengi Sana kuanzia yatima,watu wenye ulemavu ,wajane na wazee ame wasaidia Sana bila mipaka Wala kikomo,.vijana wengi Sana Mkoani Mbeya wamenufaika na kupata matumaini kupitia Dr Tulia,Ni yeye aliye wawezesha mamia kwa maelfu ya vijana mitaji ya kufungua biashara,ni yeye amewezesha mamia ya vijana kujipatia pikipiki mpya pamoja na bajaji bure kabisa kwa ajili ya kufanyia biashara na kusaidia familia zao na kuondokana na utegemezi wa kipato, Ni kupitia Dr Tulia vikundi vingi vya akina mama,vijana na watu wenye ulemavu walipatiwa mitaji ya kutosha,Dr Tulia ameleta nuru na Tabasamu kwa maelfu ya Wana Mbeya.

Dr Tulia ni Dada na kiongozi mwenye huruma Sana na msikivu wa Kiwango Cha juu Sana ,husaidia bila kujali eneo ,au Jimbo au mkoa .Ni kwa moyo wake huo wa upendo na huruma amewahi kusaidia mamia ya mabati katika shule ya msingi Mabatini inayopatikana katika mkoa wa songwe ,wilaya ya mbozi,mji mdogo wa mlowo,kitongoji Cha mabatini B.Alitoa msaada huo mkubwa kabisa bila kujali kuwa shule hiyo IPO katika mkoa na Jimbo jingine,akiwa na mh mbunge wa viti maalumu CCM mkoa wa songwe mh Juliana Daniel shonza walisaidia katika ukamilishaji wa vyumba vya madarasa yaliyo kuwa yanahitajika Sana kwa wakati huo.

Uongozi wa Dr Tulia umekuwa Ni kwa ajili ya kuwatumikia watu bila kujali itikadi za kisiasa,Wala eneo anakotokea mtu,maisha ya Dr Tulia yameleta furaha katika mioyo ya watu wengi Sana,amegusa maisha ya wengi Sana waliokuwa wamekata Tamaa na kuona Giza mbele Yao,siku zote amekuwa karibu Sana na watu,awapo jimboni au Mkoani Mbeya muda wote utamuona akiwa na wananchi wanyonge mitaani akitoa misaada ,utamuona muda wote akisaidia watu wenye Mahitaji maalumu,utamuona muda wote akisaidiana na viongozi wengine kutatua kero za wananchi,utamuona muda wote akiwatetea na kuwasemea Wananchi.

Ni kiongozi anayejuwa Nini maana ya maisha hasa kwa kuzingatia kuwa amekulia katika maisha magumu lakini akiwa na Imani IPO siku yatapita na Mungu atamgusa na kumuinua na siku moja atamfuta machozi mama yake na kugusa maisha ya watu wengine wenye kuhitaji msaada.Ni kiongozi asiye na kiburi Wala dharau wala ubaguzi na ndio maana husaidia Wote na kujumuika na wote ,Ni kiongozi mwenye kujishusha na kujinyenyekeza kwa watu,Ni mwenye hofu ya Mungu na mcha MUNGU Sana. Ni mwenye maadili mema na mwenye staha na heshima kubwa,anao uwezo mkubwa Sana wa kiuongozi na kiutendaji, anao uwezo wa kuwaunganisha watu na kujenga umoja na mshikamano,ndio maana kwa Sasa Mbeya haina mavurugu na badala yake inavuma na kusikika kwa maendeleo tu na miradi mbalimbali ya maendeleo inaendelea kuchipua na kufanyika .

Tufunge na kumuombea mtoto wetu, Dada yetu na kiongozi wetu Dr Tulia ili akashinde kwa kishindo na kutuletea heshima Kama Taifa kimataifa, Tuendelee kusimama Naye na kumpa faraja na nguvu za kusonga mbele. Itakuwa ni fahari kwetu watanzania akishinda uchaguzi huo unaofanyika mwezi October.Tumbebe katika mikono yetu na mioyo yetu kimaombi, Tumuombee kwa nguvu zetu zote na tuwashawishi wengine kutoka Mataifa mengine ili watuunge mkono kwa mtoto wetu wa kitanzania,Dada yetu imara ,msomi wa Kiwango Cha juu,mwenye msimamo usiyo yumba aweze kupita na kutuletea heshima.

Rai yangu Namuomba Dr Tulia dada yangu aendelee kumuomba mungu amtangulie katika safari hii ambayo sisi mamilioni ya watanzania tupo nyuma yake na tumembeba kimaombi, Aendelee kumtumainia na kumtegemea Mwenyezi MUNGU katika kila Hatua apigayo.viongozi wetu mbalimbali ngazi ya Taifa watumie ushawishi wetu kidiplomasia kumsaidia spika wetu kwa kila namna ikiwezekana hata viongozi wastaafu katika siasa katika ngazi mbalimbali wafanye ushawishi wa kidiplomasia kuhakikisha kuwa tunapata uungwaji mkono kwa Tulia wetu na kuzoa Kura za kutosha siku ya uchaguzi.mimi binafsi nitaendelea kumuombea Dada yangu kwa Imani yangu mbele za Mwenyezi MUNGU.

Kazi iendeleee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
Watamwombea majizi yenzie ya ccm na ma Dp world hakuna mwenye akili timamu anaombea mashetani kama hayo
 
Wewe ndiye shetani mwenye Roho ya wivu na chuki ya kijinga uliyekosa uzalendo na upendo kwa mtanzania mwenzetu.
 
Bado mamilioni ya watanzania wameamua kwa kauli moja kumuombea mtanzania mwenzetu,Dada yetu,spika wetu,mtoto wetu wa kitanzania na kiongozi wetu aweze kushinda
We mtoto wa kiume fanya biashara, fuga, lima n.k. ili ijitegemee upunguze utumwa wa kujikomba unatia aibu mtu unajikooomba utadhani ombaomba hata hivyo hachaguliwi na kama dsm huwezi jitegemea nakushauri rudi huko kweni kijijini KWAMPWIMBWILUKA usije jikuta waarabu wa mombasa wakapita na wewe
 
Back
Top Bottom