Watanzania tunahitaji maji, umeme wa uhakika, huduma bora za kijamii na uchumi imara siyo kutafuta sifa za kisiasa kwa kufurahisha magenge

Watanzania tunahitaji maji, umeme wa uhakika, huduma bora za kijamii na uchumi imara siyo kutafuta sifa za kisiasa kwa kufurahisha magenge

Abraham Lincolnn

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2018
Posts
2,754
Reaction score
4,975
Nyerere aliwahi kutamka wazi, Kwamba maadui watatu wa taifa letu ni maradhi,ujinga na umasikini.Hivi vinapaswa kuwa kipimo kwa kiongozi yeyote aliyepo madarakani.

Ni ukweli kwamba siasa zina umuhimu na nafasi ya kipekee katika kuwaletea wananchi maendeleo ya kweli, Lakini porojo zisizo na utekelezaji ni ishara ya uongozi uliofeli.

Nyuma ya siasa kuna wananchi wanaohitaji huduma bora za afya, miundonbinu bora, maji, umeme wa uhakika n.k hivi ndivyo vipimo halisi vya kiongozi yeyote aliyepo madarakani kama anatosha au hatoshi.

Endapo itatokea kiongozi akafeli katika hayo na kuona hakubaliki katika jamii kisha akaamua kutafuta mbadala wa kujichukulia point tatu zingine kufurahisha baadhi ya vikundi huku watanzania wakiendelea kusota na huduma duni za kijamii, Kiongozi huyo HAFAI.

NB: Natambua uwepo wa siasa safi ni muhimu tena ni haki ya msingi, Lakini isitutoe katika ajenda kuu ya hali ya uchumi kwa watanzania ilivyo, huduma za afya, elimu, miundombinu n.k na tusisahau kwamba hiyo ni haki ya msingi hivyo haipaswi kutumika kama mbinu ya kujinyakulia point 3 kisiasa.
 
Nchi yeyote ili iendelee inahitaji Watu, Ardhi na siasa safi!!

Hayo maji kuna sehemu hawana na muda wa kutoka kuyachota kwa sababu ya political instability!!!
 
Nyerere huyo huyo alisema ilituendelee tunahitaji watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora.
 
Mataga msiwe na roho mbaya hivyo, hii nchi yetu sote.
 
Hata mikutano ya hadhara ni haki yetu wananchi pia, acha kila jambo likae kwenye nafasi yake
Na mmeambiwa msitukane.
Maana yake mkimkosoa ni sawa na mmemtukana sasa huko jukwaani mtaongea nini zaidi ya kusifia?
 
Sababu za Lema na Lisu kujibanza kwa wazungu zinadhidi kumalizwa, mikutano ya siasa imeruhusiwa, madai yote ya Lisu yamelipwa, kesi yenye kila aina ya ushahidi ya gaidi wa kuuwa viongozi wa serikali imefutwa.
Ngoja tuone kiki mpya watakayokuja nayo .
Wengine huwezi kujua wamelaaniwa au vipi. Hivi mtu aliyepanga kuwa viongozi, na ushahidi dola inao, anaweza akasamehewa?! Rais Samia anajitahidi kusahihisha makosa ya magufuli na genge lake, ila anakosa lugha nzuri ya kuzungumza. Hii ni Kwa sababu masalia ya shetani ni mengi na yanaweza kumdhuru asipokuwa makini.
 
Back
Top Bottom