Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Watanzania,
Kule Bangladeshi siku chache zilizopita vijana wa Taifa hilo hususani wanafunzi waliongoza Maandamano makubwa ya kumuondoa Madarakani Sheikh Hasina ,ambaye yeye na serikali yake walikuwa wanatuhumiwa na kushutumiwa kwa masuala mbalimbali ikiwepo kukithiri kwa Vitendo vya ufisadi na rushwa,kuongezeka kwa umaskini,ukosefu wa ajira, kutokuwepo usawa n.k.
Baada ya kufanikiwa kumuondoa Madarakani kiongozi huyo ikaja suala la nani ataongoza serikali ya mpito wa Taifa hilo. Ambapo hata hivyo katika hali ya kipekee na imani kubwa vijana wa Taifa hilo waliamua kupaza sauti na kumpendekeza na kumchagua Muhamad Yunusi.Huyu ni Mzee mwenye Umri wa Miaka 84.
Ni mshindi wa Tuzo ya Nobel Mwaka 2006,Ambapo alipata tuzo hiyo baada ya kuanzisha Benki ya Grameen ,ambayo ilifanya kazi kubwa sana ya kupambana na umaskini kwa kutoa mikopo midogo midogo kwa watu ili waitumie kuanzisha shughuli za kiuchumi na kujikwamua kiuchumi.
Ambapo Mkuu wa Majeshi wa Taifa hilo Jenerali Waker-Uz-Zaman lenye watu takribani Millioni 170,amekubali na kuheshimu sauti za vijana na kusema kazi yake ni kulinda demokrasia.
Ikumbukwe ya kuwa mzee huyo amerejea tu kutoka Ufaransa alikokuwa amekwenda baada ya kupewa dhamana katika mfululizo wa kesi zaidi ya 100 ambazo amekuwa akifunguliwa kwa nyakati tofauti tofauti kutokana na ukosoaji wake mkubwa kwa serikali iliyokuwepo madarakani.
Mzee huyu ambaye ni Mwana uchumi amesema ya kuwa kipaombele chake ni kurejesha Utulivu,kuifanya Bangladeshi kama familia na kuwa ni lazima Bangladeshi iungane.
Hapa nawaulizeni watanzania mmejifunza nini Sauti za vijana kupazwaa na kutaka mzee huyu wa miaka 84 apewe nafasi kuongoza? Kwanini hawakutafuta kijana wa umri wao? Imekuwaje vijana tena wanafunzi waongoze maandamano ya kumuondoa kiongozi wao halafu wamependekeza mzee ambaye ni kama Babu yao kiumri kuwaongoza?
Jibu ni kuwa uongozi na suala la uongozi si suala la uzee na ujana. Uongozi ni suala la mtu kuwa na hekima,busara, unyenyekevu,upole,uungwana,utu,hofu ya Mungu,Maono,akili, Usikivu,utulivu na kushirikisha watu na kuongoza Watu kulingana na mahitaji yao. Siyo suala la uzee wala ujana .ndio maana kuna wazee wanafanya vyema na wamefanya vyema sana katika utumishi wa umma na kila wanapoaminiwa kufanya kazi.lakini pia kuna wazee wamefanya vibaya na kuharibu sana katika kazi.
Vivyo hivyo kuna vijana wamefanya vizuri na vyema sana kila walipopewa nafasi na kuaminiwa kufanya kazi.vivyo hivyo kuna vijana wameharibu sana tena sana mpaka watu kujuta na kutotamani kuwapa vijana nafasi fulani fulani kutokana na baadhi ya vijana kuharibu kazi na kujenga taswira mbaya kwa jamii.kutokana na baadhi yao kufanya kazi na maamuzi kwa mihemuko,jazba,kukomoana,visasi, chuki,tamaa ya pesa ,mali,ubabe ,kukosa hekima , Busara,usikivu n.k.
Nimesema hivyo kwa kuwa kuna jambo nimewahi kusikia siku za nyuma baadhi ya vijana wakiomba uongozi hasa Uraisi kwa gia kuwa wao ni vijana na Taifa letu lina vijana wengi sana na hivyo wamchague yeye.jambo ambalo mimi binafsi Mwashambwa nilikuwa siliungi mkono kuchaguliwa kiongozi kwa misingi ya kibaguzi ya umri.mimi nilichokuwa nazingatia na nachoendela kuamini ni kuwa ni lazima tuchague kiongozi kwa kuangalia uwezo wake wa kiuongozi,maono yake, upeo, rekodi yake kiutendaji. Yaani tuangalie kazi iliyopo mbele yetu na yule atakayekidhi mahitaji ya kazi hiyo. Kwa sababu haiwezekani unakuta mtu ameharibu kazi kila alipokuwa anatumikia halafu anataka Urais kwa gia ya Ujana au Umri wake.
Ikumbukwe pia ya kuwa Mzee wa Leo ni kijana wa jana na kijana wa leo ni Mzee wa kesho.kwa hiyo tujikite katika sifa za kiuongozi na uwezo wa Mtu kumudu majukumu ya nafasi husika. Mtu anaweza akawa kijana lakini akawa na fikiria mfu na za kizamani kabisa, lakini mtu anaweza akawa Mzee akawa na mawazo,sera, ajenda na maono ya kisasa na yenye kuendana na mahitaji ya wakati na kuleta matumaini, Kwa hiyo vijana wa Bangladeshi wametoa somo kwa watu wenye mawazo mabaya ya kutaka uongozi kwa vigezo vya kibaguzi kwa misingi ya aina yoyote ile.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.