Watanzania tunajifunza Nini kwa Vijana wa Bangladesh Waliomchagua Muhammad Yunusi Mwenye Umri wa Miaka 84 kuongoza Serikali ya Mpito?

Watanzania tunajifunza Nini kwa Vijana wa Bangladesh Waliomchagua Muhammad Yunusi Mwenye Umri wa Miaka 84 kuongoza Serikali ya Mpito?

Hawakunchagua yule kuiongoza Serikali ya mpito. Ile inahusiana na Katiba yao, kumtafuta mtu neutral kama kuna gap ya uongozi, usually huwa wanamweka Chief Justice,( ili asiingie madarakani mtu ambaye hajachaguliwa na wananchi aanze kuuza bandari,hifadhi za ardhi,na kila kitu).
Kwa hiyo,kwa makusudi,Katiba yao ina provision ya interim leader.
Umeelewa lakini hoja yangu?
 
Wewe pimbi si umeuliza kipaji changu ndiyo nimekuambia mimi ni kuhani,kumbuka sijasema padri,pastor au askofu nimesema ni Kuhani.
Kutukana mimatusi kama kichaa au mwendawazimu ndio kazi na kipaji ulicho nacho wewe.
 
Hoja yako sikuisoma. Nimejibu title tu.
Huko ni kukosa umakini na hufai kuwa kiongozi katika ngazi yoyote ile.Na huwezi ukawa na maarifa ya aina yoyote ile kwa kuwa hupo makini na husomi au kuchunguza au kufuatilia jambo kufahamu undani wake.
 
Hapa nawaulizeni watanzania mmejifunza nini Sauti za vijana kupazwaa na kutaka mzee huyu wa miaka 84 apewe nafasi kuongoza? Kwanini hawakutafuta kijana wa umri wao? Imekuwaje vijana tena wanafunzi waongoze maandamano ya kumuondoa kiongozi wao halafu wamependekeza mzee ambaye ni kama Babu yao kiumri kuwaongoza?
Ulianza vizuri... Nikajua unatoa hamasa vijana wafanye kweli... Lakini katikati ya maandishi yako ukapotea.
Mwisho niliposoma jina lako... ooops kumbe ni yule yule mwenye mambo yale yale!
Shame!
 
That is correct. Siwezi kuwa kiongozi katika ngazi yoyote.
Lakini nadhani,it proves my point.
Kama rais ana umri wa miaka 84, huyo ni rais wa mapambo.
 
Tanzania tuchukue hatua tuiondoe hii ccm ili tuweke wazalendo watakaoifanya iendelee Kwa kasi.
Hata mimi ndicho nilichojifunza. Maandamano ya Mikoa 5 tu ya Chadema sukari ilipatikana na muda wa mavuno ilikuwa bado. Umeme uliwashwa haraka sana. Tusingepiga kelele wangeendelea kusema wako kwenye MICHAKATO. Sasa hv tutaendelea kujiuliza kweli ni ngedere na bundi? Nchi nyingine nazo zenye huduma hiyo ngedere na bundi hakuna? Kama wapo wanasumbua?
 
Ikumbukwe pia ya kuwa Mzee wa Leo ni kijana wa jana na kijana wa leo ni Mzee wa kesho.kwa hiyo tujikite katika sifa za kiuongozi na uwezo wa Mtu kumudu majukumu ya nafasi husika. Mtu anaweza akawa kijana lakini akawa na fikiria mfu na za kizamani kabisa, lakini mtu anaweza akawa Mzee akawa na mawazo,sera, ajenda na maono ya kisasa na yenye kuendana na mahitaji ya wakati na kuleta matumaini, Kwa hiyo vijana wa Bangladeshi wametoa somo kwa watu wenye mawazo mabaya ya kutaka uongozi kwa vigezo vya kibaguzi kwa misingi ya aina yoyote ile.
1723240923260.png
 
Ndio maana serikali ya CCM inaendelea kusalia madarakani muda wote kwa sababu ni Sikivu kwa watanzania hususan katika mahitaji yao na kuiweka serikali mikononi mwao.
Ni mapema mno kuamini serikali mpya ya mpito kama itapasua njia ya kiuchumi ukilinganisha na serikali iliopita.
Kuna mambo mengi aliyafanya ya kuinua uchumi wa Bangladesh kutoka umaslkini uliokuwa umekithiri.
Lakini ili kufika hapa ilibidi wafunge mkanda.Ndipo ikaingia siasa za kuwahidi asali na maziwa tokea vyama vya upinzani wakati si kweli.
Hata pale serikali ilipokubali kutimiza matakwa ya upinzani bado waliendelea kuandamana ili aachie madaraka.
Subiri miezi mitatu wakikosa asali na maziwa watarudi barabarani,wajinga ndio waliwao.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kule Bangladeshi siku chache zilizopita vijana wa Taifa hilo hususani wanafunzi waliongoza Maandamano makubwa ya kumuondoa Madarakani Sheikh Hasina ,ambaye yeye na serikali yake walikuwa wanatuhumiwa na kushutumiwa kwa masuala mbalimbali ikiwepo kukithiri kwa Vitendo vya ufisadi na rushwa,kuongezeka kwa umaskini,ukosefu wa ajira, kutokuwepo usawa n.k.

Baada ya kufanikiwa kumuondoa Madarakani kiongozi huyo ikaja suala la nani ataongoza serikali ya mpito wa Taifa hilo. Ambapo hata hivyo katika hali ya kipekee na imani kubwa vijana wa Taifa hilo waliamua kupaza sauti na kumpendekeza na kumchagua Muhamad Yunusi.Huyu ni Mzee mwenye Umri wa Miaka 84.

Ni mshindi wa Tuzo ya Nobel Mwaka 2006,Ambapo alipata tuzo hiyo baada ya kuanzisha Benki ya Grameen ,ambayo ilifanya kazi kubwa sana ya kupambana na umaskini kwa kutoa mikopo midogo midogo kwa watu ili waitumie kuanzisha shughuli za kiuchumi na kujikwamua kiuchumi.

Ambapo Mkuu wa Majeshi wa Taifa hilo Jenerali Waker-Uz-Zaman lenye watu takribani Millioni 170,amekubali na kuheshimu sauti za vijana na kusema kazi yake ni kulinda demokrasia.

Ikumbukwe ya kuwa mzee huyo amerejea tu kutoka Ufaransa alikokuwa amekwenda baada ya kupewa dhamana katika mfululizo wa kesi zaidi ya 100 ambazo amekuwa akifunguliwa kwa nyakati tofauti tofauti kutokana na ukosoaji wake mkubwa kwa serikali iliyokuwepo madarakani.

Mzee huyu ambaye ni Mwana uchumi amesema ya kuwa kipaombele chake ni kurejesha Utulivu,kuifanya Bangladeshi kama familia na kuwa ni lazima Bangladeshi iungane.

Hapa nawaulizeni watanzania mmejifunza nini Sauti za vijana kupazwaa na kutaka mzee huyu wa miaka 84 apewe nafasi kuongoza? Kwanini hawakutafuta kijana wa umri wao? Imekuwaje vijana tena wanafunzi waongoze maandamano ya kumuondoa kiongozi wao halafu wamependekeza mzee ambaye ni kama Babu yao kiumri kuwaongoza?

Jibu ni kuwa uongozi na suala la uongozi si suala la uzee na ujana. Uongozi ni suala la mtu kuwa na hekima,busara, unyenyekevu,upole,uungwana,utu,hofu ya Mungu,Maono,akili, Usikivu,utulivu na kushirikisha watu na kuongoza Watu kulingana na mahitaji yao. Siyo suala la uzee wala ujana .ndio maana kuna wazee wanafanya vyema na wamefanya vyema sana katika utumishi wa umma na kila wanapoaminiwa kufanya kazi.lakini pia kuna wazee wamefanya vibaya na kuharibu sana katika kazi.

Vivyo hivyo kuna vijana wamefanya vizuri na vyema sana kila walipopewa nafasi na kuaminiwa kufanya kazi.vivyo hivyo kuna vijana wameharibu sana tena sana mpaka watu kujuta na kutotamani kuwapa vijana nafasi fulani fulani kutokana na baadhi ya vijana kuharibu kazi na kujenga taswira mbaya kwa jamii.kutokana na baadhi yao kufanya kazi na maamuzi kwa mihemuko,jazba,kukomoana,visasi, chuki,tamaa ya pesa ,mali,ubabe ,kukosa hekima , Busara,usikivu n.k.

Nimesema hivyo kwa kuwa kuna jambo nimewahi kusikia siku za nyuma baadhi ya vijana wakiomba uongozi hasa Uraisi kwa gia kuwa wao ni vijana na Taifa letu lina vijana wengi sana na hivyo wamchague yeye.jambo ambalo mimi binafsi Mwashambwa nilikuwa siliungi mkono kuchaguliwa kiongozi kwa misingi ya kibaguzi ya umri.mimi nilichokuwa nazingatia na nachoendela kuamini ni kuwa ni lazima tuchague kiongozi kwa kuangalia uwezo wake wa kiuongozi,maono yake, upeo, rekodi yake kiutendaji. Yaani tuangalie kazi iliyopo mbele yetu na yule atakayekidhi mahitaji ya kazi hiyo. Kwa sababu haiwezekani unakuta mtu ameharibu kazi kila alipokuwa anatumikia halafu anataka Urais kwa gia ya Ujana au Umri wake.

Ikumbukwe pia ya kuwa Mzee wa Leo ni kijana wa jana na kijana wa leo ni Mzee wa kesho.kwa hiyo tujikite katika sifa za kiuongozi na uwezo wa Mtu kumudu majukumu ya nafasi husika. Mtu anaweza akawa kijana lakini akawa na fikiria mfu na za kizamani kabisa, lakini mtu anaweza akawa Mzee akawa na mawazo,sera, ajenda na maono ya kisasa na yenye kuendana na mahitaji ya wakati na kuleta matumaini, Kwa hiyo vijana wa Bangladeshi wametoa somo kwa watu wenye mawazo mabaya ya kutaka uongozi kwa vigezo vya kibaguzi kwa misingi ya aina yoyote ile.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.

Swali la kizuushi, Lucas Hebel Mwashambwa una kipaji cha kuandika documents ndeeefu japo hoja inakuwa kijiko cha chai, anyway nauliza unatumia kigezo gani kuflow namna hii paragraph za kutosha japo hamna anayesoma zaidi ya mistari michache tu, then unatumia tena kigezo gani kujua sasa imetosha nafunga para ya mwisho!

Kujifunza hakuna kuchagua, naweza kupata kitu kwenye uandishi mwingi hata km nakosa hoja yako, na kuweka ile signature yako pendwa ya mama!
 
Ulianza vizuri... Nikajua unatoa hamasa vijana wafanye kweli... Lakini katikati ya maandishi yako ukapotea.
Mwisho niliposoma jina lako... ooops kumbe ni yule yule mwenye mambo yale yale!
Shame!
Vijana wa Tanzania wana imani na matumaini makubwa sana na uongozi wa Rais Samia
 
Ni mapema mno kuamini serikali mpya ya mpito kama itapasua njia ya kiuchumi ukilinganisha na serikali iliopita.
Kuna mambo mengi aliyafanya ya kuinua uchumi wa Bangladesh kutoka umaslkini uliokuwa umekithiri.
Lakini ili kufika hapa ilibidi wafunge mkanda.Ndipo ikaingia siasa za kuwahidi asali na maziwa tokea vyama vya upinzani wakati si kweli.
Hata pale serikali ilipokubali kutimiza matakwa ya upinzani bado waliendelea kuandamana ili aachie madaraka.
Subiri miezi mitatu wakikosa asali na maziwa watarudi barabarani,wajinga ndio waliwao.
Ngoja tusubiri tuangalie nini matokeo ya hicho walichokifanya. Pia ikumbukwe ya kuwa katika uongozi huwezi kumridhisha kila kitu. Na ukijaribu kufanya hivyo kutaka kumridhisha kila mtu ni lazima uharibu tu
 
Tanzania Iko katika kesi ya madai nyingine. Inadaiwa 1.2 billion dollars.
Inahusu gas field exploration.
Halafu Ile habari kama inafichwa na watu wanaodhibiti internet.
 
Back
Top Bottom