Watanzania tunajifunza nini kwa yanayoendelea Israel na Gaza?


Pata muda kidogo upitie hii video.
Jerusalem: City of Peace or Conflict.
Bila Shaka utajifunza Jambo
 
Tumejifunza
1. Israel sio taifa teule wanachofanya Gaza ni unyama
2. Hakuna taifa linaitwa Israel bali Palestine
3.Vita inayoendelea haina uhusiano na udini bali ugomvi wa ardhi
4. Marekani ni vigeugeu na iko siku sifa ya kuwa taifa lenye nguvu itafika kikomo
5.Hamas watawazidi nguvu IDF
6.China ni taifa la hovyo na halipaswi kuitwa taifa lenye nguvu kwasababu ya kushindwa kukemea uovu wa Wazayuni zidi ya Wapalestina
7. Israel inashambulia raia wa Gaza na si Hamas
9.Hamas wanatumia raia Kama ngao
10. Siku za mwisho zimekaribia KWA wale tunaoamini

Sent from my Infinix X656 using JamiiForums mobile app
 
Huku kwetu angesharambwa risasi!
 
🤣🤣🤣Mna kaz san yaliyokua na tija na ukwel ndan yake yatafanyiwa kaz, hayo mengine ya cherehani nne ni kiwanda noo.
 
Tz tuna tabia ya Kwann huyu asifanye hili, kwann yule asifanye vile ila binafsi hakuna tunalofanya.
 
Haya unayofikiria yanafanyika katika research centres na yanagharimiwa na serikali. Hapa kwetu serikali inashindwa kugharimia hata kituo cha utafiti wa korosho cha Naliendele kilochopo Mtwara au kile cha malaria kilichopo Kilombero ambavyo vinagusa maisha yetu ya kila siku sembuse kugharimia masuala ya anga na ulinzi!

Vituo vyote vya utafiti vilivyoazishwa enzi ya Mwalimu Nyerere vimebaki magofu matupu na kama vipo bajeti ya kuviendesha ni kiduchu mno hata mtu hatamani kwenda kufanya kazi huko. Angalia Ukiliguru, Nyumbu, Uyole, Mang'ula, vyuo vikuu vya DSM na Sokoine, nk vinashindwa kutekeleza yale yaliyokusudiwa. Tumebaki tukijisifia kuagiza finished goods.

Miradi yote mikubwa hata ujenzi wa nyumba na madaraja tunatumia wataalam kutoka nje. Kumbuka hawa wataalam kutoka nje wamefundishwa na kuwezeshwa kimazingira na kifedha hadi wakafika hapo walipo.

Bado tuna safari ndefu katika kujijengea uwezo kitaalamu. Tunapaswa kupitia upya sera zetu na mipango ya utekelezaji wake vinginevyo tutabaki kuwa soko la bidhaa na teknolojia kutoka nje na wananchi wetu kuwa vibarua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…