Pre GE2025 Watanzania tunajua kuwa mfumo wa uchaguzi umeundwa kihuni hivyo hakuna uchaguzi huru na wa haki ila kuna kujiteua

Pre GE2025 Watanzania tunajua kuwa mfumo wa uchaguzi umeundwa kihuni hivyo hakuna uchaguzi huru na wa haki ila kuna kujiteua

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Genius Man

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2024
Posts
1,012
Reaction score
2,317
Watanzania tunajua kuwa kwa mifumo ya kiuchaguzi iliyopo hakuwezi kuwa na uchaguzi huru na wa haki bali kuna kujiteuwa na kujipitisha.

Moja ya mifumo hiyo ni pamoja na huu utaratibu wa tume huru ya taifa ya uchaguzi kuundwa na mgombea wa chama tawala hapa hakuwezi kuwa na demokrasia wala haki kwa wagombea wengine wa vyama vingine bali kuna kujiteuwa na kujipendelea kwa aliye iunda hiyo tume.

Nilipendekeza kwamba lazima kuwe na usawa kwanza kwa wagombea wote ili tupate uchaguzi huru na wa haki kwa wagombea wote.

Nilishauri tume huru kuundwa na wataalamu watakaotokana na vyama vyote vya siasa nchini na sio na chama kimoja wala na mgombea yoyote hapa ndipo tutasema tuna tume huru.
 
Wakati nasikia kukurukakara za hiyo inayojiita "Tume Huru ya Uchaguzi" kuandikisha wapiga kura,kutoa mafunzo kwa waandikishaji nk huku matokeo wanayo mfukoni naona komedy ya kijinga sana.
 
Back
Top Bottom