Na Shilatu E.J
Mmojawapo wa watarajiwa kugombea urais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amekuja na kauli mbiu ya "Ni yeye", Mwambieni Watanzania tunajua na tunatambua kuwa ni yeye yeye.
Twende pamoja hapa. Wakati wa utawala wa awamu ya nne ni yeye akiwa Dar alisema "Nchi hii inahitaji Rais Dikteta na si vinginevyo". Lakini ni yeye yeye aliibuka tena kwenye utawala wa awamu ya tano akasema Rais Magufuli anaendesha nchi kidkteta. Huyo ndio yeye kiongozi kigeugeu wa nyakati zote.
Watanzania tunajua ni yeye wakati Rais Magufuli anazunguka Tanzaania nzima kuhakikisha kuna maendeleo, ni yeye yeye wakati huo huo yupo huko Duniani akizunguka kuisema vibaya Tanzania kwenye vyombo vya habari vya kimataifa. Ni usaliti kuzidi kiwango cha lami.
Ni yeye huyo huyo gari lake likisadikiwa kupigwa risasi upande wa kushoto aliokuwa amekaa lakini risasi ikaruka isipige upande huo wa kushoto na ikaenda kupiga upande wa kulia wa mguu wake pasipo dereva wake kupigwa hata risasi moja.
Ni yeye wakati Rais Magufuli akileta matokeo chanya ya kimaendeleo, yeye alikuwa akileta dhihaka na matusi. Bado tunakumbuka ni yeye.
Ni yeye wakati Watanzania wakishikamana na viongozi kuleta maendeleo yeye alikuwa akishikamana na Watu wa mataifa (Mabeberu) sijui kwa maslahi ya Taifa au yake binafsi? Hilo atajua yeye, sisi Watanzania tunajua yeye hatukuwa naye pamoja.
Wakati Rais Magufuli akipiga vikali wanyonyaji wa rasilimali na kuzilinda ni yeye tulimsikia akipinga vikali jitihada hizo. Nyakati zote atabakia kuwa yeye anayefurahia rasilimali zetu kuwanufaisha Wageni kuliko Watanzania wenyewe Wazawa?
Nitarudi tena baadae, ila kwa Sasa yatosha kusema ni yeye yeye na atabaki kuwa yeye kigeugeu, mnafki, msaliti, mpinga maendeleo na anayependa mshikamano na Mabeberu.