Hii ni fursa kwa Watanzania tunaompenda,kumjali na kumthamini bila kujificha Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan .Tunajua Taifa letu la Tanzania 🇹🇿 chini ya Chama cha Siasa tawala ambacho kimejenga msingi ambayo ndiyo ni Tanzania toka mwaka 1961.
Kutokana na maendeleo CCM imekutana na changamoto nyingi ambazo tumshukuru Mungu chama hichi kimeweza kuzidhibiti ,lakini bado changamoto hiziishi kwa sababu utawala ni mmiliki ya Mali pia kwa hiyo kuna UTU ambao unania kufaidika na utawala kwa kuiletea changamoto CCM ambayo toka Uhuru imekua ikifanya maendeleo na kufanya msingi mipya ya kimaendeleo.
Tunajua Mwenyezi Mungu ilibidi amchukue mtu wake Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli na kumpa nchi Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan .Hatusemi Samia ni bora kuliko Magufuli ila Mungu anamipango yake na aliona Rais Samia Suluhu Hassan anatufaa pia.
Rais Samia Suluhu Hassan akachukua Utawala na hadi sasa tunadumu naye.Ila yeye ni mtu Mashuhuri kwa amekutana na changamoto nyingi na sasa kwa kuwa alifanya maamuzi magumi maadui zake wanatumia mfumo Dume kupigana naye vita ili nchi itetereke na ikiwezekana wao watawale kwa mawazo finyu,tamaa na ukosaji uzoefu wakitumika na mataifa ya kigeni ambayo agenda zao ni kupata fursa ya kuinyonya Tanzania.
Kwa hiyo kuna kampeni tunayotaka kuifanya sisi Wana CCM na Watanzania wanayoikubali CCM ya kusimama na kumtetea Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan Tanzania na katika uwanja wa kimataifa .
Kwa hiyo tujumuike kwa pamoja katika mpango kazi huu wa kimaendeleo yetu sisi wenyewe Watanzania wa kupinga propaganda za wapinzani na mabepari wanyonyaji dhidi ya tuhuma hizi ambazo zinatusumbua nchi nzima.
Mpango ni Mheshimiwa Rais kukutana nasi na kuzidi kutupa sababu zaidi za kuendelea kumfuata na kupata muongozo wa nini cha kufanya katika kusimama naye.
Karibuni sana sana katika hii adventure ,sio ya kuikosa.