Watanzania tunaompenda, kumjali na kumthamini bila kujificha Rais Samia

Mungu yupo pamoja nasi wala hatuna cha kusita au kisitisha harakati zetu.
 
Na mnatumia nguvu kubwa kumsafisha lakini hatakati, ukitaka kujua huyo bibi yenu hapendwi nenda kijijin zungumza kwa upole na kina mama wa huko utapata jibu
Nilidhani ni mimi tu nime notice hilo jambo, mwaka jana mwisho nilikuja kusalimia alooo, i didnt beleive wananchi wa kijijini, wamebadilika , wako so informed hawadanganyiki kirahis tena
 
Mnalibagaza sana neno na maana ya UZALENDO. Kutetea muovu na uovu kisa tu mnatoka kijiji kimoja, au chama kimoja au mna imani inayofanana huo SIYO uzalendo.

Semeni kweli hata kama ni kiongozi anakosea. UKweli unauma lakini Ukweli utawaweka HURU. Acheni kuwaza matumbo yenu, someni alama za nyakati.
 
Toa takataka hapa.... kazi kumshauri mwenyekiti wenu kuua badala ya maendeleo na haki
 
Toa takataka hapa.... kazi kumshauri mwenyekiti wenu kuua badala ya maendeleo na haki
CCM hatujakamilika lakini tunapigania usahihi toka mwanzo lakini usisahau wanaoongozwa wengine ni wa binafsi na wabaya na lengo lao ni kuona hata kuna vita hii nchi nao ndiyo waliowatumia gen z kwa Maslahi yao na wala siyo yako wewe Mwananchi.
 
Nilidhani ni mimi tu nime notice hilo jambo, mwaka jana mwisho nilikuja kusalimia alooo, i didnt beleive wananchi wa kijijini, wamebadilika , wako so informed hawadanganyiki kirahis tena
Wote nyie mnadhani riziki anawapa Mheshimiwa Rais Dkt Samia tengenezeni fursa wenyewe na ndiyo hapo Mungu kupitia Serikali ya Rais anakupa riziki.
AMKENI.
 
Hakuna asiyewaza tumbo lake hichi ni cha kwanza ujue na hakuna anayefanya kazi bila Maslahi.
Ukweli ninaopaswa kukupasha ni kwamba kuendesha nchi ni kazi ngumu Kutokana na watu kama wewe lakini tumezoea kosa ambalo tulifanya ni kuacha ujinga utambae hili ni kosa ambalo hatutafanya tena.
 
Hahahaha bwana ww sina time na personal attacks , psg hoyee
Watanzania tunapata taarifa tunizipokea haraka bila kuchanganua kwa kina na kuangalia uhalisia na kufanya maamuzi na matendo yasiyofaa kwenye Jamii kwa kuwa tu wapo kwenye changamoto na sehemu pa kuhegemea ni pabaya na kufanya maamuzi ya kuhegemea kwenye kutaka kupindia Serikali ya Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan .

Kwa hiyo matokeo ni Oktoba 2025 kitu ambacho ni dhahiri ni Sheria tu ilikua active deeply .

Baada ya mahesabu wapinzani wamejua kuwa hawawezi kufanikiwa,wamejificha na kunyamaza harakati zao na kubaki kuacha takataka zao asafishe Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na kumuita Muuaji juu.Hili jambo ni dhambi, tuache jamani.

Mimi binafsi namwambia Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kama anasoma hili kwamba kwangu mimi yeye ni Mastermind namtegemea kuhandle mambo yangu mengi kama Mwananchi wa Tanzania 🇹🇿 katika ulimwengu huu wa sasa na amefanya maamuzi mengi chanya kwa hiyo namuunga mkono kwa kutambua thamani ambayo ipo kwenye utawala bora na kuipigania na kushinda.

Hawa Mabepari wanaomfatilia ndiyo vibaraka wa shetani na ICC ni kifaa cha haki tu kwa hiyo wanaCCM hatuogopi tupo pamoja na Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan (Samia ni Mama ) na kesi hii anashinda.

Tume kaweka watu wake, sasa mlitaka Baba zenu ambao hawana ELIMU awaweke pale?,yeye kawaweka wasomi ambao wapo Serikalini wanaomuogopa Mungu .Kwani mnadhani hatujui hata Serikalini kuna vibaraka wa wapinzani?

Sincerely .
 
Ndiyo maana hamna UHALALI wa kuongoza NCHI. kumbe mnawaza matumbo yenu tu, mmepora MAMLAKA ya wananchi kuchagua viongozi tuwatakao. Nyinyi ndiyo WAHAINI wakubwa. Ni suala la muda mpate stahili yenu.
 
Ndiyo maana hamna UHALALI wa kuongoza NCHI. kumbe mnawaza matumbo yenu tu, mmepora MAMLAKA ya wananchi kuchagua viongozi tuwatakao. Nyinyi ndiyo WAHAINI wakubwa. Ni suala la muda mpate stahili yenu.
Wewe ulitaka Mheshimiwa Rais awe nani ?
 
Wewe ulitaka Mheshimiwa Rais awe nani ?
Yule ambaye amechaguliwa na wananchi, KATIBA inasema wazi Mamlaka yote itatoka kwa WANANCHI. Sasa tukiwa wakweli, chaguzi nyingi CCM imekuwa na tabia ya kupora MAMLAKA ya wananchi kwa kujitangaza washindi kupitia tume batili za uchaguzi.

Uzuri hadi makada wenu wameshakiri hili, mfano ni Nape aliposema wazi kuhusu goli la mkono na akarudia tena kwa kusema kutangaza mshindi inategemea ni nani anaye hesabu na kutangaza na wala siyo nani amepata kura nyingi. Huu ni UHAINI ila kwa kuwa ni chama dola kinacho tawala hakuna hatua zilizochukuliwa.

Tukija uchaguzi wa Oct.2025 ndiyo ulikuwa wa hovyo mno. Kwanza utakubali maeneo mengi uchaguzi ulivurugika kwa wananchi kuvunja na kuchoma kura na maboksi yake moto. Hilo tu kwa nchi inayojielewa ilikuwa sababu tosha kusitisha zoezi zima. Ila kwa dharau bado 'mshindi' akatangazwa, TUME hapa nayo ilifanya UHAINI.

Haya 'mshindi' akatangazwa kwa kupata 98% ya kura milioni 31, hapa inaonyesha wananchi zaidi ya milioni 30 (30,380,000) walimpigia kura. Kama idadi hiyo ni kweli ilikuaje akaenda apishwa ndani ya kambi ya jeshi na siyo uwanja wa Jamhuri au Uhuru kama ilivyo zoeleka.

Kwahyo mnavyo endesha kampeni sijui za kumtetea ni kujichoresha ila uzuri umekiri unapigania tumbo lako maana mnajua kwa hakika hakubaliki na idadi kubwa ya wananchi ni nguvu ya dola ndiyo inamkingia kifua
 
CCM hatujakamilika lakini tunapigania usahihi toka mwanzo lakini usisahau wanaoongozwa wengine ni wa binafsi na wabaya na lengo lao ni kuona hata kuna vita hii nchi nao ndiyo waliowatumia gen z kwa Maslahi yao na wala siyo yako wewe Mwananchi.
Naona utajiri wa abdul unakunufaisha hadi wewe?
 
Nilidhani ni mimi tu nime notice hilo jambo, mwaka jana mwisho nilikuja kusalimia alooo, i didnt beleive wananchi wa kijijini, wamebadilika , wako so informed hawadanganyiki kirahis tena
Tena Kama kwetu ni Wana CCM lakini wapo against na mambo yaliyotokea Kwa CCM yenyewe!
 
Tena Kama kwetu ni Wana CCM lakini wapo against na mambo yaliyotokea Kwa CCM yenyewe!
Changamoto iliyotokea inatokana na mfumo dume.Mpaka Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan anapata Urais matokeo yake sio wapinzani tu hata Wana CCM wengine hawakutaka Mama Samia aongoze kwa hiyo hilo jambo likawa nafasi nzuri kwa wapinzani na wanaomchukia kufanya mipango ya kumuondoa na wengine kuendelea kusisitiza aondoke madaraka ni kitu ambacho kimechochea sana yaliyotokea oktoba 2025 .
Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan sio alitaka kutawala kimabavu Bali alipigania haki yake kikatiba na matokeo yake yakawa mikakati ya kumpindua na yeye ni Kiongozi anajua nini Tanzania 🇹🇿 kinatufaa kwa hiyo haikuwezekana kuachia Madaraka kwa sababu anajua mpinzani ni muaribifu na Tanzania kwa sasa hakuna chaguzi linguine badala yake ndiyo maana akambana na sheria ikamuunga mkono.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…