Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Juzi hapa niliweka thread ikiishauri serikali, hususa Raisi Samia, kutoa tamko ambalo lingezuia mara moja utekaji na uuaji. Kama kawaida ya hii serikali yetu, naona hawajali kuchukua hatua kama hizi.
Sasa basi, kama Raisi Samia au serikali kwa ujumla hawana nia ya kuchukua hatua thabiti na rahisi kukomesha utekaji na uuaji, acha jukumu hili tulichukue sisi wananchi wenyewe. Maisha yetu ndio yako hatarini tunapaswa kujilinda.
Natoa wito na hima kwa Watanzania wote, popote pale ambapo unaona watu wasio na uniform wanamkamata mtu, tushirikiane kuzuia hilo kwa kila namna. Tuwazuie watu hao kwa kila njia na kuwaambia wasubiri hadi polisi wafike, wakiwa na uniform na magari yanayoeleweka kuwa ni ya polisi. Hadi sasa hili limeshafanyika kwa mafanikio makubwa! Tusiwe kondoo tena wa kuona mwenzetu anaenda kuchinjwa na kusubiri zamu yetu au ya ndugu yetu.
Umati wa watu ukiwazunguka watekaji, pamoja na magari na bodaboda kufunga barabara, watekaji hawawezi kufanikiwa. Tushirikiane Watanzania, hili linawezekana. Hata kama watekaji wana silaha, sio rahisi kwamba wataanze kuufyatulia risasi umati mkubwa wa watu.
Ukiona watekaji wana nia ya kumchukua mtu, piga kelele, na wale wenye magari na boda boda pigeni honi kukusanya umati wa watu. Tutafanikiwa kukomesha tabia hii ya kinyama inayotuondolea ndugu zetu wapendwa.
Na ikitokea kwamba watekaji wanaingia kwenye basi, abiria wote ndani ya basi tusimame katikati ya njia (aisle) na kutoruhusu mtu kupita, na kuamuru dereva wa basi aendeshe basi hadi kituo cha polisi.
Tafadhali saidia kusambaza huu ujumbe kwa watu wote, kwa email na hata magroup ya WhatApp na mengineyo
Angalia pia
View: https://www.youtube.com/watch?v=C_ahzCLMzrw
www.jamiiforums.com

Kama Rais Samia ana nia ya kukomesha mara moja watu kutekwa na kuuawa, atoe tamko hili
Ngoja tuone... Cc: Mahondaw