Watanzania tupaze sauti zetu kunusuru uhai wa maelfu ya vifaranga visivyo na hatia vinavyoenda kuangamia

Watanzania tupaze sauti zetu kunusuru uhai wa maelfu ya vifaranga visivyo na hatia vinavyoenda kuangamia

Swali mtajuaje jibu lake ni kupima.Na ndio maana hata kwa Covid watu wakiingia wanapimwa kwanza au angalau kupiga marufuku wasiingie na hata wakiingia kwa njia za panya wakikamatwa hawauwawi hao watu watakamatwa watapimwa kwa lazima kwa gharama zao kisha wanafungwa.
Kwa wanyama ni kutokuwatendea haki kabisa sijui hapa Tanzania lile shirika la kutetea haki za wanyama nakumbuka linaitwa TSPCA(Tanzania Society for Prevention of Cruelty to Animals) linasemaje nakumbuka zamani niliona ofisi yao pale karibu na Muhimbili.
Mbona hata askari polisi traffick wanajua hii sheria?.Siku moja nilimpakiza Mbuzi kwenye pikipiki nikawa nimembeba vibaya nikapita tukakutana na Traffick japo ilikuwa kijijini alitusimamisha akatuambia mnamtesa bure huyu mnyama kwa njia hii tumieni njia nyingine nilitii maagizo hayo nikaamua kumswaga na tulifika tunakokwenda.
Kwanini aingize kuku illegally??
 
Waambie waviangamize kama vile vya Kenya halafu wangojee majibu yao
 
Leo katika taarifa ya habari ya ITV saa 08:00pm wametoa taarifa ya mfanya biashara huko Morogoro kukamatwa na mabox 200 yenye vifaranga vyenye thamani ya TZS 40M vilivyoingizwa nchini kinyemela kutoka Kenya.

Mwandishi amemhoji mtaalam husika wa serikali Ni nini kitafuata baada ya ukamataji huu, mtaalam akawa na jibu moja tu "Tutaviteketeza kwa mujibu wa sheria"

Ningekuwa mimi ndio nmeulizwa hilo swali ningejibu "Tutachukua hatua mbalimbali ikiwemo kuvipima kuangalia Kama vimebeba vimelea vya magonjwa then mamlaka husika itaona Ni hatua gani zaidi zichukuliwe baada ya kushauriana.

Hii ni kwa sababu, endapo vitachomwa na ikaja kutthibitika havina magonjwa, kwanza ni kukiuka haki ya ya kuishi kwa viumbe hai, pili kupotezea nchi mapato ambayo yangeweza kupatikana endapo muingizaji angetozwa faini, tatu kupoteza Kodi ya mapato kutoka kwa muingizaji na mwisho wa siku kuua uchumi wa wafanyabiashara.


Kuliko vichomwe Kama itathibitika havina ugonjwa bora vigawiwe bure hata kwenye majeshi yetu kuongeza tija.

Kwa sababu tajwa hapo juu, nawaomba wana jf wote na watanzania kwa ujumla tuungane kwa pamoja kupinga kitendo hichi kisitekelezwa kwa Hawa viumbe hai wenye Tina kubwa kiuchumi.

Roho inaniuma Sana kwa kweli!
achana nao, endelea na shughuri zako
 
Kwa mujibu wa sheria ya magonjwa ya wanyama ya 2003( animal disease act 2003 ) unaweza google na kuipitia ,vifaranga inabd wateketezwe .ilaa kwa mujibu wa sheria za haki za wanyama 2008 vifaranga inabd wasiteketezwe (kuwapa haki za chakula ,kuwatibu ,kuwapa haki ya kuishi na kuwapunguzia maumivu)

Hapa inahitajika busara ya mkamataji ,ilaa njia rahisi sana kwake ni kuviteketeza maana vikiwa na magonjwa ambayo hayatajulikana kwa sasa ilaa baadaye hao kuku wakikua na watu wakiwatumia na wakapata madhara eg .kuvimba uso, kuharisha ,kutosimamisha lawama zotamfikia mkamataji .

Namalizia kwa kusema vifaranga viteketezwe.
 
Tatizo watu wanatatua na kutoa maamuzi kwenye hili jambo kwa kuangalia ukenya na utanzania...kwanza sakata la mahindi liliishia wapi?

Kuteketeza hao vifaranga kwa vyovyote vile hasara ni kwa Tanzania. Wasitie madoa yadiyoya lazima utawala wa Mama.
Kwa mtindo huo wanaweza kufikiri njia nyingine za kupata kodi kweli? I doubt! Mawazo yao mgando hadi lini? Wataanza kutumia akili lini?
 
Sidhani kama umefikiria kuhusiana na Afya ya watanzania ambayo iko hatarini??

Tutajuaje kama hao wanyama wanafaa kwa matumizi ya binadamu wakati hawajaingizwa kwa kufuata taratibu.

Si umeona Kenya walivyo ban mahindi yetu kwa kigezo cha afya za wananchi wake??

Badala ya kufanyia siasa kila jambo, tumia akili pia.
Kwa nini wakimbilie kusema watswateketeza badala ya kusema tutawapima wote kuona kama wana magonjwa halafu kama hawana magonjwa yoyote mhusika atatakiwa kulipa faini, na akishindwa tutawapiga mnada..
 
Wawapime na kama hawana magonjwa wapige mnada kama mwenye mali hana hela ya Kodi, tuache kutumia nguvu kila siku wakati tunahitaji pesa. Hii hata tukiwachoma haitusaidii kitu. Halafu najiuliza kuna nini Kenya mbona watu wanapenda mbegu ya vifaranga vya huko?
Mama Samia alishasema, mamlaka waache kutumia nguvu badala ya kutumia akili, kisa tu sheria inaruhusu! Lakini naona hii mijamaa ni mibichwa migumu!! Mibishi, mama Samia achukue hatua
 
Kwani Sheria inasemaje kuhusu hilo, kwanini hawataki kufuata Sheria?
Mama Samia ameshaelekeza, mamlaka waache kutumia nguvu na badala yake watumie akili, na sio tu kwamba sheria inaruhusu, basi unafanya kama roboti, maendelea hayaji hivyo, sheria zimewekwa for extreme cases, kwamba wamegundulika na magonjwa nk.
 
Basi kama wana ulazima wavitoe uhai ndio iwe kwa moto?!!! Atakehusika kuvichoma moto basi namuomba Mungu nae siku moja ampe ajali ya moto huyo mtu aone utamu wa moto.
 
Ni kwamba hizi nchi zetu hatuwezi kuweka utaratibu wa kuuziana bidhaa kama hizi, na vipimo vikafanyika kuthibitisha ubora?
Serikali hii inawatendaji baadhi ni kama wendawazimu kwa kweli
 
Sidhani kama umefikiria kuhusiana na Afya ya watanzania ambayo iko hatarini??

Tutajuaje kama hao wanyama wanafaa kwa matumizi ya binadamu wakati hawajaingizwa kwa kufuata taratibu.

Si umeona Kenya walivyo ban mahindi yetu kwa kigezo cha afya za wananchi wake??

Badala ya kufanyia siasa kila jambo, tumia akili pia.
Kwani unapoambiwa vipimwe ili kujua hali ya afya unakuwa unaelewa nini labda?
 
Back
Top Bottom