Watanzania tupende vya kwetu

Watanzania tupende vya kwetu

kyata

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2015
Posts
2,535
Reaction score
2,499
Imekuwa ni jambo LA kawaida kwa watanzania kutopenda kuvitukuza na kuvipenda vitu vyetu wenyewe ambavyo asili yake ni hapa hapa nchini kwetu. Imekuwa ni ya wapenzi na mashabiki wa mpira wa miguu kutokuthamini timu zetu zinazotuwakilisha kwenye mashindano ya kimataifa kwa kisingizio cha utani wa jadi. Hii dhana ya utani wa jadi tumeiharibu kiasi kwamba sasa si utani wa jadi Bali ni kama uadui Fulani hivi. Nakubaliana na suala LA utani wa jadi maana limekuwepo, lipo na litaendelea kuwepo kwa mechi zetu za hapa nchini. Ila linakuja suala timu mojawapo inacheza na timu ya nje ya nchi yetu haileti maana kukuta nusu ya uwanja wanaisapoti timu hiyo toka nje. Bali hii uwaga inashamgaza sana hata timu wsgeni wetu utushangaa kwelikweli. Nimekuwa nikifuatilia mechi za timu zetu ziwapo nje ya nchi, sijawahi on a hata Sikh moja timu zetu zikipata support ambazo wao upata kwetu. Mfano Simba mwaka Jana imecheza mechi nyingi za kimataifa kwenye viwanja vya wageni, lakini hakuna hata sehemu moja ilipata support zaidi ya kuzomewa na mashabiki wa nchi zile. Sasa najiuliza hivi sisi tunapojitia kimbelembele kushabikia timu ngeni uwaga tunapata nini? Jibu hakuna. Swali jingine hivi huko nchi za wenzetu halunaga timu hasimu (watani)? Jibu ni zipo, sasa he mbona sionagi wapenzi wa timu pinzani huko wakizipa support timu zetu? Jibu ni moja tu, wenzetu neno uzalendo kwa vitu vyao limewakaa, hakuna kusalitiana. Hivyo basis nasi tuige, tuwe wazalendo kwa timu zetu zinazotuwakilisha sasa na zitakazotuwakilisha muda ujao, utani ubaki kwenye ligi yetu, mechi baina yetu, ila tukitoka nje tushikamane. Bila shaka mmenielewa na Jumamosi wote tupige Uzi wa Yanga, jumapili tupige Uzi wa Azam fc, tuzipe joto timu zetu kwa mstakabali wa maendeleo ya vilabu vyetu kimpira na taifa kwa ujumla. Twende pamoja. Asanteni.
 
Tatizo ni ukosefu tu wa uzalendo na pia deaturi ya baadhi ya mashabiki kuendekeza ushabiki maandazi.
 
Back
Top Bottom