Kuna watu ni kama hua wanaiona kesho. Nimeona huu uzi nimemkumbuka bro flani alinitengenezea gari la kuchezea mwaka 99 lilikuwa na mota ya redio za kanda(kaseti) imefungiwa betri ya ABC kwa ndani kuna namna kaiunga ile mota na tairi za lile gari so ulikuwa ukiiunga ile mota na betri gari linajiendesha. Jamaa alikuwa mvumbuzi sana sijui saizi yuko wapi.