Idimi
JF-Expert Member
- Mar 18, 2007
- 15,328
- 11,192
Kwa kutoa hivyo vithibitisho naamini Watahatarisha amani na utulivu wetu tuliojijengea maana imeshasemwa wazi hali ni tete.
Hapo sasa! Vikiletwwa huenda watu tusitazamane usoni!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa kutoa hivyo vithibitisho naamini Watahatarisha amani na utulivu wetu tuliojijengea maana imeshasemwa wazi hali ni tete.
Hivi mkubwa na wewe hutaki katiba mpya? Acha ushabiki usiokuwa na kichwa wala miguuNi kweli ingawa pia tunapoingiza wachungaji kwenye siasa inadhihirisha na kuonyesha jinsi tulivyo. Ni kweli lakini pia makanisa yanapojitokeza hadharani na kuipigania chadema inadhirisha kuwa kina ajenda ya UDINI. Ni kweli lakini pia ZITO anapoandamwa sana ndani ya chama ni dhahiri udini unafanya kazi yake. ni kweli lakini pia unaposimamisha mgombea mwenza muislamu mbumbumbu (darasa la saba) ni kielelezo tosha cha kuonyesha waislam watakuwa wakubruzwa tu katika serikali ambayo ingeundwa na chadema. NA HUU NDIO UMAKINI WA VIONGOZI WA CHADEMA. Ni kweli pia hata wana JF wanaoshabikia chadema wana msimamo hasi dhidi ya Waislamu. Ni kweli lakini pia jinsi chadema ilivyojipanga kupambana na CUF inadhirisha na kuamsha maswali mengi. NA HII YOTE HAIHITAJI KUPIGIWA PROPAGANDA NA CCM. Ni ukweli usiofichika. Bado ni kweli hata kadiri tunavyokwenda inadhirisha uchanga wa wanasiasa wa chadema. Bado nasisitiza kuwa UBINAFSI NA UZANDIKI NA UKABILA PAMOJA NA KUKOSEKANA UZALENDO ni miongoni mwa vipaumbele vya viongoi wa chadema. Bado haya yote hayahitaji kupandikizwa na CCM.
Twende mbele turudi nyuma bado wanasiasa wa Chadema hawana vision ya Utaifa bali wanataka kutumia silaha na umasikini pamoja na katiba kufika Ikulu kwa gharama yoyote hata ikigharimu maisha ya watu wengi.
Ningeshawishika kidogo madai ya kusema CCM wamechakachua matokeo ya URAIS ikiwa chadema wangekuja na DATA kamili ya idadi kwa majimbo ya kila mgombea aliyopata - mwezi mmoja sasa baada ya uchaguzi kuisha. TUTAWAAMINI VIPI WAKIYALETA SASA KAMA SI YA KUCHAKACHUA?. JE, KATIKA HILI CCM SI WATAONEKANA BORA ZAIDI ??
NACHANGIA HOJA.
Article nzuri.
Nyongeza: Tusikubali pia propaganda za Dr. Slaa kuwa kura zake zimeibiwa mpaka atuonyeshe vidhibiti.
Nikiwa kama mtanzania wa kawaida ambae ninaipenda nchi yangu,sina budi nikitoa maoni yangu.
Nimejaribu kufatilia sana siasa za Tanzania tokea uchaguzi wa vyama vingi mwaka 1995 kipindi cha kampeni. Nakumbuka uchaguzi wa mwaka huo chama kikuu cha upinzani kilikuwa ni Nccr mageuzi
ya akina Mrema against chama tawala ccm ambacho mgombea wake alikua Benjamini mkapa.
Ukiachilia vyama vyote vya upinzani wakati huo,chama ambacho kilikubarika na watu ni Nccr mageuzi
Ccm walipogundua kuwa Nccr ni hatari na nitishio kwao,wakaenda mafichoni,waliporudi wakaja na pro
paganda ya kuwa Nccr mageuzi ni chama cha kikabila [wakimaanisha wachaga] na maana ya NCCR ni
Ni Chama Cha Rabsha. Kwakua kipindi hicho baadhi ya watanzania wengi tulikuwa na mawazo mgando
tukainyima kura Nccr na Mrema wake. Tukaipa kura ccm na mkapa akashinda japo si kwa kishindo.
Uchaguzi wa mwaka 2000 ikatokea chama kingine chenye nguvu na sera mzuri against ccm nacho ni
CUF,kikiongozwa na mh.Lipumba kwa huku Bara na visiwani kikiwakirishwa na Seif sharif Hamadi.
Ccm kama kawaida yao walipoona CUF inakubarika na wananchi,wakaingia tena mafichoni, waliporudi
tu wakaja na bonge la propaganda ya kuwa CUF ni chama cha kidini [hapa walilenga uwislaam].
Haitoshi wakaagizia mapanga nje ya nchi na yakaja kwenye contena yakiwa yana bendera za CUF.
wakaviita vyombo vya habari kuja kushuhudia ugaidi wa Cuf! kumbe si kweli bali propaganda tu!.
Kwahiyo yale ya mwaka 95 yaliyomkuta Lyatonga na Nccr yake,ndio yaliyemkuta mh.Lipumba na
cuf yake. Watanzani tukaigopa Cuf kama ukoma na kura zote tukaipa ccm,na wakashinda tena kwa
propaganda zao
Uchaguzi wa mwaka 2005 nao ukaja na vitukovyake. kwanza wapinzani hawakuwa na nguvu kama
chaguzi zilizopita. kwahiyo ccm kama kawida yao wakazama mafichoni,walivyorudi huko wakaja na uo
ngo unaofanana na propaganda kwa wadanganyika [walikuja na vitu 3] ili tuwachague tena.
Kwanza walisema chagua ccm maisha bora kwa kila mtanzania.Pili wakasema mgombea wao [mh.kikwete] ni 'handsome'yaani ni mzuri ki umbo. Tatu wakasema kikwete ni chaguo La mungu. Wadanganyika tukaichagua ccm,na kikwete akashinda kwa kishindo.kumbe uongo mtupu!
Lakini mambo yaliyotokea ndani ya miaka hiyo mitano hakuna asiyejua! ni vurugu tupu hakuna cha
maisha bora wala babu yake maisha tamu! Badala yake tukashuhudia ufusadi wa kutisha na maisha
kuendelea kuwa magumu kwa watanzania tulio wengi.
Uchaguzi uliyopita wa mwaka huu 2010 ulikuwa wa aina yake kwa wananchi wengi kuwa na mwitikio.
Pamoja na vyama vyote vilivyoshiriki uchaguzi huo,chama ambacho kilikuwa na nguvu ya ajabu na kukubarika na wanchi kwa kasi ya ajabu ni Chadema ambacho kwenye kampeni zake kiliongozwa na
Dr Slaa na timu yake iliyo makini. Hakika hiki ni Chama cha upinzani ambacho hakijawai tokea Tanzania. Chama ambacho kilikuja na sera mzuri,viongozi imara,wasomi na wenye uchungu wa Tanzania na raia wake! Hakika waliichambua serikali ya ccm kuanzia utosini hadi unyayoni na watanzania tukaamka for first time.
Lakini kama kawada ya ccm,wakaenda mafichoni waliporudi huko wakaja na bonge la propaganda lenye sumu kali. Wakasema Chadema ni chama cha kidini [hapa walilenga ukristo]na ukabila.
Kwa watu kama sisi ambao tunazijua propaganda za ccm tukasema Nooo! thiz time we have to vote for change,na tukaipa kura chadema. Ila kwa wale waliokuwa teyari kuipa kula chadema wakati huo huo hawazijui propaganda za ccm 'hasa vijijini' waliposikia sumu za ccm wakabadilisha mawazo na wakaipa kura ccm au hawakwenda kabisa kupiga kura. kwahiyo ikawa faida na neema kwa ccm na
hasara kwa Chadema. ccm ikashinda tena japo si kwa kishindo kama chaguzi zilizopita.
Narudia tena, Chadema ni chama ambacho hakijawahi tokea Tanzania bara! kimetuonyesha kina
sera mzuri,uongozi imara,na kina future ya Tanzania tunayoitaka! kimepata wabunge wengi bara kuliko chama chochote cha upinzani. Ni chama ambacho kimekubarika pande zote za Tanzania bara!
Na isingekuwa propaganda za ccm,basi Chadema ingeshika Dola na leo ingekuwa story nyingine.
Hitimisho langu ni-
Watanzania tusikubari propaganda hizi za Ccm! Ni hatari sana hawa watu hasa wanapoona kuna chama cha upinzani makini na chenye uongozi imara,hapo wao wako teyari waivuruge nchi kwa
propaganda za sumu ili mladi waendelee kutawala! Camooon guys tuamkeni watanzania! hii ni
nchi yetu wote na tunawajibu ya kuipigania kwa manufaa ya walio wengi! Ahsanteni.
Nawakilisha.
Nashukuru kwa michango yenu ambayo imejali maslahi ya Utaifa Zaidi kuliko udini. ingawa pia nashangazwa na michango yenu pahala pengine ambapo mnajidhirisha mlivyo na chuki dhidi ya dini zingine na hasa Uislamu. Binafsi sioni tatizo la nani atawale nchi hii. Hii ni nchi yetu sote. Pengine tatizo ni dhamira inayojitokeza wakati wa kufanya maamuzi MUHIMU NA NYETI na jinsi tunavyosifia Umakini wa viongozi tunao washabika bila kupima upande wa pili. Hebu tuendelee kujadili.
1.0 Suala la mgombea mwenza wa chadema kuwa mbumbumbu ingawa kweli kuna tatizo la kikatiba hapo je, hamkuona kama kumchagua huyo ilikuwa ni Kuwatenga Wazanzibari na Waislamu???. je, hamuoni kwa kufanya hivyo mumekosa kura muhimu za wenye kuyatazama majambo kwa uelewa mzuri??
2.0 Je, Suala la wana JF waliowengi wanaoshabikia Chadema kubeza waislamu hamuoni linahatarisha msingi wa umoja wa Taifa letu?. Je, Chadema inajipambanua vipi kitaifa? mdharau mwiba mguu huota tende! kalagabaho!!!
3.0 Je, suala la Chadema na wanachadema kupambana na CUF hamuoni haileti picha nzuri Kitaifa?
4.0 Madai ya kusema CCM wamechakachua matokeo ya URAIS . Na BADO chadema wameshindwa kuleta DATA kamili ya idadi kwa majimbo ya kila mgombea aliyopata - mwezi mmoja na ushee sasa baada ya uchaguzi kuisha. TUTAWAAMINI VIPI WAKIYALETA SASA KAMA SI YA KUCHAKACHUA?. UMAKINI WA VIONGOZI WAPAMBANAJI UKO WAPI???????????????!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Haya mambo manne muhimu tujadili kwa kina bila ushabiki. Penye tatizo tuthubutu kusema. Nafahamu wazi CCM wamekuwa na tabia ya kupandikiza propaganda za kuuwa chama chenye nguvu. lakini pia naomba michango yenu katika haya mambo manne. je, CCM inahusika vipi?
Na kama ni kweli basi kuna tofauti gani kati ya CCM na CHADEMA?
Iam more RATIONAL than EMOTIONAL instigated!
Mi ni muislam tena swala tano ila kuliko niishabikie au kuchagua ccm bora nile nguruwe japo hacheuwi.ccm ni kama nguruwe hakicheui kile chama wao ni kula tu.ikumbukwe pia nguruwe hula hadi wanae aliowazaa mwenyewe.same like happen to ccm wana sema eti elimu bure haiwezekani wakati wao walisomeshwa na hiyo hiyo ccm bure.SHAME ON YOU CCM NA TEAM NZIMA.