Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Leo ni siku ya Sensa. Hata hivyo mpaka kunakucha leo bado sikuwa na taarifa sahihi za sensa. Sikujua leo nisitoke nyumbani au nikitoka niache nini na nini. Tabia yangu huwa sifungui tv wala redio nyumbani na kwenye simu siangalii sana ujumbe mpaka nione ni wa kampuni za simu wenye neno pesa.
Kwa namna hiyo wangenipatia kunielimisha kama wangetoa matangazo mitaani kwa muhtasari na kunielekeza nini cha kufanya leo. Bahati mbaya niliwahi kuona msafara wa magari unaotoka ofisi ya mkuu wa wilaya lakini zaidi ilikuwa ni kutaja siku ya sensa na kibwagizo. Mimi niko tayari kuhesabiwa. Wewe Je?
Kwa mara nyengine niliwahi kuona kikundi cha wangenguaji na yawezekana walilipwa kwa kazi hiyo. Nilikutana nao nje sokoni wakiwa wameshuka kutoka kwenye gari lao. Wanacheza kwa kurusha miguu, mikono na kukatika viuno bila kutoa ujumbe wowote.
Matokeo yake mpaka nawapita na kuendelea na safari sikusikia chochote cha kufanya siku ya sensa.
Nimesikia kwa wapita njia kuwa sensa itaendelea kwa siku 7. Siku ya kesho mpaka siku ya 7 wakipita sitakuwa na majawabu ya leo. Vilevile ama hawatonikuta hapa nyumbani tena au tutakutana kwengine mbali.
Mimi niko tayari kuhesabiwa,lakini nina wasi wasi ama hawatonihesabu au watanihesabu mara zaidi ya moja.