1000 digits
JF-Expert Member
- Oct 16, 2012
- 7,802
- 10,307
Jambo linaloleta mambo ya udini ,ukabila,ukanda,n.k ni sababu ya umaskini.
Afrika bado kuna udini,ukabila na kila aina ya upendeleo kwa sbabu ya umasknia.
Siasa na madaraka Afrika ni njia ya kutajirika haraka.
Mtu akiteuliwa uwaziri ni kama vile kumtoa Paka Jalalani na kumweka sebuleni kwenye sofa.
Kila mtu anawaza uteuzi au uwaziri ili apate maslahi ya uhakika.
Afrika hata Kama uchumi wa nchi unayumba vipi kamwe hutasikia kuwa Mawaziri wamekatwa mishahara yao ili kulinda uchumi wa nchi.
Aisee ingekuwa Mimi ndio Rais kitu ukabila,upendeleo ,udini n.k . Ningekifyekelea Mbali kwa kufyeka mishahara ya Watawala wote wa kuteuliwa . Hata wabunge ningefyeka mishahara yao.
Kama mtu ni Daktari atalipwa sawa na Daktari anayetibu hospitalini.
Kama ni mwalimu atalipwa kama yule aliyebaki Kule shuleni
Kiwango cha Elimu na ujuzi kitalipwa sawa kwa wote.
Waziri atalipwa ziada za safari na safari tu lakini mshahara ni kulingana na Elimu yake sawa na idara nyingine.
Sio sawa kulimpa mshahara Mlevi kama Waita yule naibu zaidi ya Mara kumi ya mtu mwenye elimu sawa na ya kwake kwa sababu tu yupo mfano wizara ya Elimu au ni hakimu au nesi n.k.
Hii ingesaidia watu kutumikia nafasi za utawala na uongozi kizalendo na kujitoa ili kujenga taifa na sio kujenga maisha yao tu huku Nchi ikizidi kuwa maskini na wafanyakazi wakizidi kudidimia kwa kulipwa mishahara duni.
Mtu akichaguliwa kuwa waziri angeona wazi kuwa sio dili bali ni mzigo amepewa kuubeba kwa uaminifu na sio ya kujinufaisha.
Kila mtu angeridhika na nafasi aliyo nayo kwenye jamii.
Ilivyo sasa kwa kweli kila mtu anatamani dini yake, au kabila lake au rafiki yake au ndugu yake ateuliwe au apate ubunge au apate uwaziri au apate urais au apate uwaziri mkuu mana umaskini ndio utakua bye bye forever. Yaani kwenye eneo moja wakitoka mawaziri mawaziri wengi au wateuliwa wengi ujue ndio pato la nchi limehamia huko mana kwa miaka mitano jumla ya mishahara na marupurupu yao yote ni mabilioni ya kodi za wote ikiwemo wasomi na wabobevu kuwazidi ambao watatumikia taifa mpaka wastaafu hata robo ya kipato chao hakitafikia.
Kwa hiyo kelele zote za udini sijui ,ukabila ,ukanda ,urafiki n.k ni kwa sababu ya maslahi makubwa yaliyokuwa yamewekwa na makada wa CCM waliotangulia huko nyuma na sasa yanalipeleka taifa kubaya.
Ni vyema sasa watanzania wote tulijenge Taifa bila kujali dini ,kabila,urafiki,ukanda n.k . kwa kupunguza Mapesa mengi wanayolipwa wanasiasa hasa watawala na wabunge . Hakuna kazi ngumu kama za majeshi kote duniani lakini kwenye nchi maskini wao wanatumika kwa mishahara midogo na wanakua watiifu kwa uzalendo mkubwa. Sasa iweje wanasiasa wasio na silaha wala wala ngao zaidi ya kutumia hayo majeshi kama ngao zao na nguvu za kujiwekea wao mamishahara makubwa huku wanaotumikia nchi kwa kutoa nafsi zao wakiwa na mishahara kiduchu kwa uaminifu?
Nchi za Dunia ya tatu hasa Afrika wanapaswa kubadikika.
Na Tanzania mabadiliko ya kweli yasipopatikana awamu ya hii ya JPM kwenye utawala wa CCM ndio basi hayatatokea tena labda mana hata vyama vya upinzani havina Sera za kujenga uzalendo na kulijenga taifa hili la kijamaa.
Sijui ni vipi Viongozi wanaendelea kuwa madarakani kwa Katiba inayolitaja taifa hili kuwa ni la kijamaa huku wao wakiwa mabepari.
Hatuwezi kuendelea kutegemea misaada toka kwa mababeru au kuwakamua wananchi kodi kubwa na wafanyabiashara kufilisika ili tu watawala wawe mabepari kwenye nchi ya Kijamaa.
Nchi hii mtu hapaswe kutumia madaraka kwa ajili ya kujitajirisha lakini sheria za mafao zimewapa watawala nafasi ya kuwa mabilionea kupitia kodi za wanyonge kwenye nchi maskini ya kijamaa.
Kazi iwe ni moja tu asiyekubaliana na kutumika kama wengine kwenye ujamaa wetu aachie ngazi akafanye kazi nyingine .
Haiwezekana Mkurugenzi anatembelea gari la mil. 400 kwenye nchi ya kijamaa.
Hivi nani angeweza kulipwa mshahara halali kwa Elimu yake angeenda kununua gari ya kutembelea ya sh. Mil 400 badala ya kutumia kusomesha watoto wake na kuwekeza kwa ajili ya kukuza kipato. Wanafanya ufahari bila huruma kwa sababu hakuna anayejali maslahi mapana ya jamii kwenye nchi hii ya kijamaa.
Mil. 400 inaweza kujenga nyumba za madaktari na kumi kwenye hospitali ya wilaya zenye thamani ya mil. 40 kila moja.
Watawala waitumikie nchi yetu wakitambua kuwa hii ni nchi ya kijamaa na tena bado ni nchi maskini inayohitaji kujwengwa na wote kwa moyo. Anayeona kuwa hawezi kufanya kazi kwa kulipwa kama wengine akae pembeni watu waaminifu wapo wengi sana lakini hawana wa kuwapa hizo nafasi ili kuonyesha uaminifu wao zaidi ya wasanii wanaokabidhiana ulaji kwa awamu.