Chagu wa Malunde
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 8,746
- 5,772
Ndugu zangu natoa hii rai kwa wananchi wote wa Tanzania huu ndio wakati wa kuwa na mshikamano wa pamoja, nasema hivi sababu tayari ni dhahiri kuwa Corona virus yupo ndani ya jamii yetu.
Kama kuna reported cases mpya 14 na zote ni zimetokea ndani ya nchi yetu basi ni wakati muafaka wa kuweka siasa kando na kupambana na hili janga kwa pamoja.
Tujifunze kwa wenzetu ambao pamoja na kuwa ni nchi tajiri na zimeendelea kwa kila namna huu ugonjwa umewavuruga kwa kila namna, fikiria nchi kama Usa au Uk inafikia kuwa na upungufu wa vifaa vya kukinga hata manesi na madaktari! Uchumi wa dunia nzima unaporomoka kama theluji inayoyeyuka.
Nashangaa sana pale mtu anapokuwa sio mfuasi wa chama tawala anapofurahia ati nchi yake wagonjwa wa Covidi -19 kuongezeka.
Unajua hili ni janga ambalo litamkuta nani? Ni ugonjwa ambao hauna tiba wala chanjo. Fikiria maisha yetu hapa Tanzania kama ikitokea mlipuko mkubwa tutaweza kukabilana na huu ugonjwa?
Tusilete ushabiki wa vyama vya siasa juu ya hili janga. Tupambane wote kama Taifa moja. Tupambane na hili janga kwa kuzingatia uzalendo na mapenzi ya nchi yetu. Tujipime kwa ufasaja je ni njia gani ambayo itatuepusha na hili janga kama taifa maskini? Total lockdown? Partial? Au kuzingatia usafi na umakini?
Nimeangalia CNN kwa mfano jimbo kama Arkansas nchini USA hawajafanya total lockdown kama New York na New Jersey na hoja yao kubwa na ni kuwa jimbo lao halina mrundikano wa watu sehemu moja kama New York.Na mpaka sasa wana vifo kama 25. (Natoa mfano tu)
Kwa hapa Tanzania kwa Jiji kama Dar es Salaam total lock down inawezekana? Partial lockdown inawezekana? Je, social distancing inawezekana? Kwa social distancing jibu ni hapana hata kwa macho. Maana hata uweke mpango wa level sitting huwezi dhibiti huu ugonjwa sababu unaambukizwa kwa chafya na kutoa mate yenye maambukizi. Maana kama kuna mtu anao akipiga chafya lazima asambaze ndani ya gari.
Kwa mujibu wa CDC ya Marekani, social distancing ndio suluhisho la huu ugonjwa, hauna tiba wala chanjo. Hivyo kama watanzania tujifunze kukabiliana na huu ugonjwa kwa umoja. Tuache siasa na ushabiki. Nashangaa sana bado hili suala la kukaa mbali hata mita 1.5 watu hawalizingatii.