Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 17,048
- 22,790
Naona kama kuna idadi kubwa sana ya watanzania wanaopenda vitu hivyo, yaani Udaku (habari za kuhusu mambo ya watu wengine) na Nadharia za Njama (kuwa kuna jambo la njama linafichwa na serikali au taasisi yoyote). Ukitaka kula hela ya watanzania, jikite katika biashara ya kuuza udaku na nadharia za njama; utachuma kweli kweli kweli.
Mkapa alitututakana kuwa tuna uvivu wa kufikiri, maneno ambayo aliyakopi kwa mgriki mmoja wa zamani sana nadhani Alistotle, lakini ndio ukweli kuwa hatutaki kufikiri badala kupokea habari nyepesi kama hizo. La ajabu ni kuwa hiyo ni hulka ya watu wengi sana duniani, siyo watanzania tu.
Wanasiasa kadhaa wa upinzani wameona malipo ya nadharia za njama, na ndiyo imekuwa sera yao. Vyombo vingi vya habari vinegudundua malipo ya udaku, na vimekuwa vinaweka udaku sana kwenye habari zao.
Swali: Je kuna uwezekano wa kuvunja hii cycle ya udaku na nadharia ya njama, na badala yake kukuza ukweli unaohusu maisha yetu sote.