Habari za muda huu ndugu wanabodi wenzangu? Leo nimerudi tena baada ya takribani siku kadha zilizopita kuwa na majukumu mengine na hasa ya kiuchumi pamoja na ya kisiasa...
Ngonjera hizi wapelekee mbumbumbu sio Watanzania wa leo waliokwisha fumbuka macho. Unasema uongozi haujaribiwi. Je mtu hajawhi kuwa kiongozi ina maana hatakua kiongozi milele? Chama hakijawahi kuongoza serikali, hakitaongoza milele? Munataka muwaaminishe watu ccm itatawala milele? 2015 mliparangana kwny ccm yenu mkatuletea hili jaribio (magufuli) matokeo yake ndo haya.
Rais gani ni mbaguzi mfano wa magufuli? Kauli zake: Ukichagua mpinzani sitawaletea maendeleo, mtalimia meno, mtaishi kama shetani, hao usiwavunjie (nyumba) walinipa kura, msichague wapinzani hata kama wana sifa, serikali yangu haitasomesha wazazi (mabinti wanafunzi waliopata mimba), serikali haitawasaidia chakula kwakua haina shamba, nk.
Mnakua kama mazezeta kumsifu binadamu mpaka mnamlinganisha na Mungu. Kwa neema ya Mungu ametuepusha janga la vovid19, leo mnakuja kumsifu magufuli. Alifanya nini cha maana kwenye hili janga? Nani asijua alikimbia mjini kujificha chato? Unasema tafiti zilizofanywa- nani mwenye uhuru wa kufanya utafiti huru Tanzania ya leo?
Nani asie jua yaliyowapata TWAWEZA baada ya utafiti wao kuonyesha umaarufu wa magufuli umeshuka? Nani asiejua yaliyowapata wakosoji wa magufuli- Ben Saanane, Askofu Niwemugizi, Kabendera, Tundu lissu, etc? Tunataka UHURU HAKI NA MAENDELEO YA WATU. Tuchague madiwani wa CHADEMA, wabunge CHADEMA na MH. TUNDU LISSU RAIS tupate UHURU, HAKI NA MAENDELEO YA WATU.