Uchaguzi 2020 Watanzania, uongozi haujaribiwi. Chagua kwa ajili ya Uhuru na Amani ya Watanzania

Jiwe alikuwa hajawahi kuwa hata kiranja wa darasa, hata wa chekechea, leo eti ni Rais......
Tunawataka Ben, Azory, Mawazo, Akwilina and many others...... hatusikii lolote katu
KWANINI USIWATAFUTE? NANI KAKUZUIA MPAKA UNAMTAKA LISSU?
 
YAANI KAMA UNA MACHO MA 3 VILE KWA KUONA, SI UNAONA KWA WARUSI KULE? PUTIN KAPELEKWA NA WATU IKULU NA SIO KURA
 
Usije ukatuambia hata manabii walifanikiwa kwa sababu walikuwa kwenye kipindi cha Giza, hahahahahaha.

Kijana ukishajua kutumia kompyuta na smart phones pamoja na ku-download na ku-upload unajiona upo kwenye zama za Nuru hahahahahaha..
Vyombo hivyo hivyo vya dola ushindwa kuzilinda mamlaka zinazokengeuka na kuacha misingi ya kuongoza watu kwa kutumia kanuni za kuongozea wanyama kuongozea watu dola ilishindwa kuziokoa na zilianguka na kufutika kabisa,soma history ya rise and fall of kingdoms au mwambie yeriko akupe shule zaidi kuhusu dola na mamlaka.
 
Habari za muda huu ndugu wanabodi wenzangu? Leo nimerudi tena baada ya takribani siku kadha zilizopita kuwa na majukumu mengine na hasa ya kiuchumi pamoja na ya kisiasa..
Tunamfahamu sasa vilivyo kuliko zamani. Alichowafanyia Watanzania, wengi wanafahamu. Yale tuliyoyategemea, sina haja ya kuyataja maana ni ya kawaida, na yalifanywa na watangulizi wake. Lakini yafuatayo yamekuwa dhahiri chini ya utawala wake:

1) Watu kuuawa na maiti kutupwa kwenye viroba

2) wanaomkosoa kupotezwa

3) wanamkosoa kushambuliwa kwa risasi

4) wanaomkosoa kubambakiwa kesi za uhujumu uchumi, kutakatisha fedha na madawa ya kulevya

5) sheria mbaya za kuminya uhuru wa maoni, uhuru wa vyombo vya habari, na haki mbalimbali za raia

6) kuvunja katiba na kutofuata sheria na migawanyo ya mihimili ya utawala

7) ubaguzi na upendeleo kwa misingi ya itikadi, kabila na maeneo

8) kuvuruga uchumi kwa kuendesha utawala wa kimabavu. Leo ukuaji wa uwekezaji na utalii, umeporomoka maradufu (uwekezaji toka 28% mpaka 4%; utalii toka 15% mpaka 3.6%)

9) udhalilishaji wa utu wa binadamu

10) kuvuruga chaguzi mbalimbali ukiwemo uchaguzi wa serikali za mitaa

Kumchagua tena, ina maana tunataka mambo hayo yaendelee. Nani anayeyapenda hayo? Tulimjaribisha, tumepata majibu. Majibu yamekuwa mabaya. Sasa tujaribishe mwingine.

Kwa nia ya kuokoa nafsi zetu na wenzetu, lazima tufanye mabadiliko.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari za muda huu ndugu wanabodi wenzangu? Leo nimerudi tena baada ya takribani siku kadha zilizopita kuwa na majukumu mengine na hasa ya kiuchumi pamoja na ya kisiasa...
We peleka ujinga wako Lumumba!! Uongozi uongozi!! nilini jiwe aliwahi hata kuwa mwenyekiti wa serikali ya mtaa?? Kama ni ubunge Lisu nae amekuwa mbunge!! Mwanasheria msomi!! mtu wa haki!! amekuwa akitetea watu kabla hata hajawa mbunge!! ni jinsi gani anaupendo na watu!! sio mnafiki Kama walivyo viongozi wenu!

Lisu sio mchumia tumbo, Kama walivyo viongozi wenu!!
Lisu sio fisadi Kama walivyo hao walikutuma uje uwasafishe hapa!!

Lisu ni mtu wa haki tangu ujana wake!! wananchi twendeni na Lisuuuuuuuuuu!
 
Usitake kutuaminisha kwamba mchakato wote huu wa uchaguzi ni danganya Toto, Kama kuchagua chadema na lissu ni kuhatarisha utulivu na amani ya nchi, kosa si la lissu wala chadema ball ni kosa la walioitisha uchaguzi, lissu ana kura nyingi kuliko babu yenu na uchaguzi huu lissu atamshinda babu yenu kwa kishindo.
 
Mkuu. mleta mada ni ushamba tu ndio unamsumbua!! achana nae! uwezo wake wa kufikiri umeishia hapo!!
 
Kiongozi mzuri utoka kwenye taaluma za sheria, uchumi, sayansi ya Jamii, biashara maana huku ni lzm uwe na reasoning capacity nzuri na sio claiming capacity. Na uongozi ni reasoning na sio claiming capacity
 
Kishajichokea lakini anang’ang’ania tu. Alidhani Urais ni lelemama na udhalimu wake ungetufanya Watanzania tukae kimya.

Kazi ya uraisi ni ngumu Sana Kama unaingia kwa lengo la kuumiza, kuwakomoa watu utaishia kuukimbiza tu upepo ni rahisi zaidi Kama nia yako kuinua na kuboresha maisha ya watu
 
Sikiliza video ya Bashiru. ameungana na Lisu kunadi sera zake!!
Kule wamefata maslai lkn hata nafsi zao zinawasuta hasa ukiwa msomi,unajua hakuna Uhuru wa watu Hakuna maendeleo ya watu.
 
Maneno mingii pumba mtupu...kuna amani Tanzania ama watu waliamua tu kuyanyamazia..wakalilia mioyoni mwao

Watu wanakufa....watu wanatekwa, watu wanababikiziwa kesi eti tuchague amani..ipi kwa mfano...

Hiki ni kisiwa cha uvumilivu...!! Watanzania ni wavumilivu mno na tuwasifu maana wamevumilia mengi sana mno ndani ya hii miaka mitano.

Watanzania sasa wameshaamua kwenda na Tundu Antipas Lissu!! Hili halina mjadala...nuna usinune!!
 
Hayo aliyoyaleta ameleta kwa wachache but wengi ameshindwa kuwagusa thus unaona upepo ulivyo
 
Wakati Magufuli akituburuza kwa miaka 5 inaonekana wewe ulikuwa kwenye fungate.
 
Mwaka huu mkatafute kazi za kufanya kwa sababu wananchi raia walio wengi wamechoka na ahadi chungu nzima kila chaguzi na kuambulia vumbi tu, Kura za kutosha tunampa Ndugu Antipas Lissu wengine mkae kwa kutulia,Zingatia Lissu anashinda Uchaguzi na lazima atangazwe, Itachukua muda kutangazwa ila ushindi wa Lissu upo wazi.
 
Wewe ni idiot of the month.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…