Watanzania waishio Comoro wakutana na Balozi Yakubu

Watanzania waishio Comoro wakutana na Balozi Yakubu

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,278
Reaction score
797
Mheshimiwa Saidi Othman Yakubu, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Comoro amekutana na Viongozi wa Jumuiya ya Watanzania wanaoishi nchini Comoro (Tanzania Diaspora in Comoros - TADICO) tarehe 30 Mei, 2024 katika Makazi yake, Voidjuu.

Wakati wa mkutano huo, Viongozi wa TADICO walitambulisha Jumuiya yao na kuelezea mikakati wanayoendelea nayo katika kuhudumia wanachama waliojiandikisha na Watanzania wengine wanaoishi au kumtembelea nchini Comoro. Walijulisha kuwa miongoni mwa hatua muhimu iliyofanyika ni kuwapatia Vitambulisho wanachama 303 Kati ya 374.

Aidha, Viongozi hao walimpongeza Mheshimiwa Balozi Yakubu kwa kuteuliwa kuiwakilisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Comoro na kuahidi kumpatia ushirikiano ili kumuwezesha kutekeleza majukumu yake kama ilivyo kuwa kwa watangulizi wake. Walimfahamisha kuwa Comoro ni kituo muhimu.

Naye Mheshimiwa Balozi Saidi Othman Yakubu aliwashukuru Viongozi hao kwa kukutana naye ili kubadilishana fikra katika masuala yanayohusu Jumuiya yao pamoja na shughuli zao nchini Comoro. Aliahidi kutenga muda maalum ili kukutana nao katika makundi yao ili kupata picha zaidi kuhusu harakati zao.

Aidha, aliwajulisha Viongozi wa TADICO kuwa Diaspora ina wajibu wa kuitangaza Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Comoro kwa kutenda yaliyo mema na kuendeleza sifa njema za nchi yao ikiwemo kuhamasisha umoja na mshikamano katika maeneo wanayoishi, kushirikiana na kutangaza fursa zinazopatikana Tanzania.

Vile vile, aliwafahamisha kuwa, kwa kutambua mchango wao katika maendeleo ya nchini, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imedhamiria kutekeleza mipango kabambe kuhakikisha wanapata fursa ya kuchangia maendeleo nyumbani.

IMG-20240530-WA0090.jpg
IMG-20240530-WA0088.jpg
IMG-20240530-WA0086.jpg
IMG-20240530-WA0087.jpg
IMG-20240530-WA0091.jpg
IMG-20240530-WA0089.jpg
 
Tanzania ununue eneo huko ijenge soko, ili wafanyabiashara wakodi na pia uwe kama kituo cha kibiashara kwa watanzania wanaotaka kufanya biashara huko . (kituo cha kibiashara)
-Watanzania wengi wamedhulumiwa mali zao huko!
 
Back
Top Bottom