Watanzania waishio Marekani kwanini wasirudishwe nyumbani wakiwa na pingu mikononi kama wenzao wa Brazil na Mexico

Wazungu hawana kheri kabisa.Zamani walipotaka watu wahamie kwao kuwatumikia waliwapeleka kwa minyororo bila ridhaa zao,na sasa wameendelea kiteknolojia wanawarudisha tena makwao kwa minyororo kama mwanzo.
 
Wakupe ungo upae sasa ushahitimu degree ya uchawi..!!
 
Acha roho ya kichawi hiyo chalaangu..
Usimwombee mwenzako mabaya,wanafaida kwa ndugu zao wa karibu,wewe huo ni faida kwakuwa siyo sehemu ya jamaa au ndugu wa karibu,naamini ungekuwa mnufaikaji usingepost hivyo..
 
Asilimia kubwa ya Watanzania waliopo Marekani wapo kihalali ama waliingia Marekani kihalali tofauti na raia wengi wa South and Central America ambao wamevuka boda kwa njia za panya
Huu ndio ukweli na majority kabla ya yote walihangaikia makaratasi kwanza na sio jamii hatari kwa usalama wa nchi
Trump ugomvi wake ni hayo magenge ya wa Amerika ya kusini na baadhi kaskazini kama Mexico
 
Serikali ya Mexico hapo juzi iliikatalia ruhusa ndege ya kijeshi ya Marekani kutua nchini humo ikiwa na abiria wenye asili ya nchi hiyo waishio Marekani. Hatua hiyo ni baada ya kuapishwa kwa raisi Donald Trump japo huko nyuma ilikwishawahi kuwapokea raia hao kwa mikono miwili ikiwaona kama tunu ya kuongeza vipaji nchini mwao.

Kwa upande wa Brazili hapo juzi pia imetoa lawama kali kwa serikali ya Marekani kupitia waziri wake wa mambo ya nje kufuatia abiria 88 kuingizwa nchini humo kinyemela wakiwa na pingu mikononi.

Vyovyote vile itakavyokuwa kwa upande wangu ningependa kujua Watanzania waishio Marekani je, hawana sifa kama hizo kwa utawala wa Donald Trump.

Kwa maneno mengine jee watanzania hao wana sifa gani za kuendelea kubaki Marekani na kukwepa kurudishwa nyumbani kama wenzao wa Marekani ya kusini
Una roho ya kichawi ndugu yangu! Mfano wakirudishwa Tanzania wewe na familia yako mtafaidi kitu gani? Au kwa jinsi wanavyo ishi huko USA wewe unapata hasara gani? Jitafakari
 
Sio Roho Mbaya. Watanzania wengi sana wanaokwenda Ulaya na Marekani iwe kihalali au kimchongo huwa hawana faida kwa Taifa wala ndugu zao. Hawajali wala kukumbuka kwao na hawatoi connection kwa wenzao.(ubinafsi, Roho Mbaya na kukosa uzalendo). Mkenya akitoka na kufanikiwa lazima awekeze kwao, mkenya akitoka lazima avute wenzake wa kutosha tu.

NAUNGA MKONO WABONGO WARUDISHWE MAANA HAWANA FAIDA HATA KWA FAMILIA NA JAMAA ZAO.

NAJUA NA WEWE NI MMOJA WAO
Kukaa kwao Marekani kunakupa hasara Gani ww au wazazi wao walileta malalamiko kwako

Wewe unafikiri walikuwa naaisha mazuri bongo wakakimbilia huko kupambana
Pengine hawajafanikiwa Ila hamna haja ya kutamani wapatwe na majanga
 
Serikali ya Mexico hapo juzi iliikatalia ruhusa ndege ya kijeshi ya Marekani kutua nchini humo ikiwa na abiria wenye asili ya nchi hiyo waishio Marekani. Hatua hiyo ni baada ya kuapishwa kwa raisi Donald Trump japo huko nyuma ilikwishawahi kuwapokea raia hao kwa mikono miwili ikiwaona kama tunu ya kuongeza vipaji nchini mwao.

Kwa upande wa Brazili hapo juzi pia imetoa lawama kali kwa serikali ya Marekani kupitia waziri wake wa mambo ya nje kufuatia abiria 88 kuingizwa nchini humo kinyemela wakiwa na pingu mikononi.

Vyovyote vile itakavyokuwa kwa upande wangu ningependa kujua Watanzania waishio Marekani je, hawana sifa kama hizo kwa utawala wa Donald Trump.

Kwa maneno mengine jee watanzania hao wana sifa gani za kuendelea kubaki Marekani na kukwepa kurudishwa nyumbani kama wenzao wa Marekani ya kusini
Trump hafukuzi kila mgeni; Trump anafukuza raia wa kigeni wasiokua na makaratasi ya kuishi kule. Halafu, ni nini kilicho pelekea wewe kua na wazo OVU namna hiyo dhidi ya Watanzania wenzio? Utapata Nino wao wakirudishwa? Kumbuka tu, "Wivu ni hatua ya mwisho kabisa kabla hajatunukiwa UCHAWI rasmi" look very, yaani angalia sana
 
Kukaa kwao Marekani kunakupa hasara Gani ww au wazazi wao walileta malalamiko kwako

Wewe unafikiri walikuwa naaisha mazuri bongo wakakimbilia huko kupambana
Pengine hawajafanikiwa Ila hamna haja ya kutamani wapatwe na majanga
Sio kupatwa na majanga. Tanzania ina ardhi kubwa sana na mapori ya kutosha. Wanaotakiwa kwenda Ulaya na Marekani kufanya kazi za house boy ni nchi ambazo hazina rasilimali ardhi ya kutosha. Warudi walime. Mtu unakimbilia Marekani na Ulaya unakaa miaka 10 unarudi Tz lakini tunakuzidi maisha tena kwa mbali sana, na ndio maana wengine mnaona aibu kurudi. Pumbavu zenu
 
Naona unaandika uzi huu ukiwa Kaswenswe ndani ndani....
 
Watanzania wenyewe huko ng'ambo kila wakipata pesa zinaishia disco, casino na kwenye mapaja ya mademu
Mkuu hizi ni hadith za kitaa wapo Watanzania wamewekeza huko nje ukiambiwa ni Mtanzania unakataa sema Watanzania wengi hawana connection na Matajiri Watanzania waliopo nje ndio maana hata kuwajua ni ngumu kwa baadhi ya Nchi nilizozunguka nimeona wapo njema sana aisee..
 
Sio kupatwa na majanga. Tanzania ina ardhi kubwa sana na mapori ya kutosha. Wanaotakiwa kwenda Ulaya na Marekani kufanya kazi za house boy ni nchi ambazo hazina rasilimali ardhi ya kutosha. Warudi walime. Mtu unakimbilia Marekani na Ulaya unakaa miaka 10 unarudi Tz lakini tunakuzidi maisha tena kwa mbali sana, na ndio maana wengine mnaona aibu kurudi. Pumbavu zenu
Mkuu ukipata fursa wasaidie tu watu ndio maisha hakuna kingine ila usiwadharau watu ambao leo hawana mazee..
 
1737089181289.jpg
 
Serikali ya Mexico hapo juzi iliikatalia ruhusa ndege ya kijeshi ya Marekani kutua nchini humo ikiwa na abiria wenye asili ya nchi hiyo waishio Marekani. Hatua hiyo ni baada ya kuapishwa kwa raisi Donald Trump japo huko nyuma ilikwishawahi kuwapokea raia hao kwa mikono miwili ikiwaona kama tunu ya kuongeza vipaji nchini mwao.

Kwa upande wa Brazili hapo juzi pia imetoa lawama kali kwa serikali ya Marekani kupitia waziri wake wa mambo ya nje kufuatia abiria 88 kuingizwa nchini humo kinyemela wakiwa na pingu mikononi.

Vyovyote vile itakavyokuwa kwa upande wangu ningependa kujua Watanzania waishio Marekani je, hawana sifa kama hizo kwa utawala wa Donald Trump.

Kwa maneno mengine jee watanzania hao wana sifa gani za kuendelea kubaki Marekani na kukwepa kurudishwa nyumbani kama wenzao wa Marekani ya kusini
Mungu tusaidie watanzania wengi wana roho mbaya Sana ila zimejifisha kwa wachache wenye roho nzuri, kabisa ukamtakie mwenzio mabaya [emoji24][emoji24][emoji24]
 
Wa
Serikali ya Mexico hapo juzi iliikatalia ruhusa ndege ya kijeshi ya Marekani kutua nchini humo ikiwa na abiria wenye asili ya nchi hiyo waishio Marekani. Hatua hiyo ni baada ya kuapishwa kwa raisi Donald Trump japo huko nyuma ilikwishawahi kuwapokea raia hao kwa mikono miwili ikiwaona kama tunu ya kuongeza vipaji nchini mwao.

Kwa upande wa Brazili hapo juzi pia imetoa lawama kali kwa serikali ya Marekani kupitia waziri wake wa mambo ya nje kufuatia abiria 88 kuingizwa nchini humo kinyemela wakiwa na pingu mikononi.

Vyovyote vile itakavyokuwa kwa upande wangu ningependa kujua Watanzania waishio Marekani je, hawana sifa kama hizo kwa utawala wa Donald Trump.

Kwa maneno mengine jee watanzania hao wana sifa gani za kuendelea kubaki Marekani na kukwepa kurudishwa nyumbani kama wenzao wa Marekani ya kusini
Wanaletwa kwa njia hiyo!
 
Back
Top Bottom