Tanzania ni nchi ya aina yake kulinganisha na zingine zote duniani. Kwa hakika ni halali wengine kuiita kuwa ni nchi ngumu sana.
Chukua muda uisome nchi hii kupitia kwa watu wake. Zanzibar wanaweza kuwa tofauti, lakini si bara.
Inasikitisha kuwa Tanzania bara ni jamii ya watu waliojaa ubinafsi, wivu, choyo, husuda, fitna, ujinga, na ujuaji uliopitiliza.
Watu wamekaa kichawi chawi kwamba mafanikio ya mwingine ni mwiba kwao. Watu wapo kusubiria anguko la mwingine ili wapate kufanya sherehe.
Inapiganiwa katiba mpya vipi kwenye jamii hii? Zinapiganiwa haki zipi kwenye jamii hii?
Matokeo yake ni tuyaonayo kutokea kwa CAG, wanavuna waliyopanda. Walisema waungwana hadi akili ziwakae sawa.
Waone wanaojifanya kuwa ni wapigania haki na u ndumila kuwili wao.
Ni Tanzania tu ambako si waziri Nchemba peke yake, bali hata mwananchi kapuku wa Makambako huko, anauthubutu wa kumchagiza mwingine akiwamo asiyemjua kuhamia Burundi.
Siyo bure tuna matatizo makubwa labda kuliko tunavyo fikiria.
Inaweza kuwa ni muhimu sasa tukajitathmini, labda kwa makini zaidi.
Wenye kuutuhumu mwenge wanaweza kuwa na hoja, wasikilizwe!