Watanzania waliopo Uarabuni na Ulaya wanapokonywa Pasipoti nakutumikishwa; pasipoti hizo zinatumika vibaya. Serikali ifuatilie

Watanzania waliopo Uarabuni na Ulaya wanapokonywa Pasipoti nakutumikishwa; pasipoti hizo zinatumika vibaya. Serikali ifuatilie

feature-image-2.jpg

Wasichana wa Kiafrika waliopitia Kafala System wakiandamana.
 
GER010-05-2.jpg
vijana wa Kiasia walio chini ya Kafala System wakiwa wamelundikwa kwenye makazi yao duni na hatari vijana hutumika zaidi kwenye sekta ya ujenzi huko Uarabuni.

UTU uko wapi?
 
Wapo Wazazi wengi hasa kanda ya Ziwa wanatafuta namna ya kuwarejesha Watanzania ndugu zao Nchini.

Taarifa za baadhi ya watanzania waliofanikiwa kurejea Nchini zinasema pasipoti zao zinachukuliwa na waajiri mara tu wanapofika ughaibuni na kutokea hapo wanaanza kutumikishwa.

Wanadai wakiripoti ubalozini majibu wanayopewa ni kwamba serikali haikuwatuma waende huko hivyo watajua namna ya kurejea Nchini. Baadhi wanafanya mawasiliano wakiwa tayari wameumizwa kingono au kupigwa au kudhulumiwa haki zao.Hali hiyo ipo sana Malaysia, Uturuki, China, Qatary, Oman, Dubai na Iraq.

Chakushangaza, wanapofanikiwa kutoroka kwa waajiri na kupata wasamaria wema wakuwasaidia hifadhi ili waweze kupata pasipoti za karatasi zakurejea Nchini maafisa ubalozi wengi wanadaiwa kutokufanya yafuatayo

1. Hakuna taarifa za familia inayoshikilia pasipoti zinazochukuliwa badala yake wanalazimisha watanzania waseme wamepoteza pasipoti kitu ambacho siyo kweli.

2. Wanakataa kuwaandikia mamlaka za nchi husika wafanye uchunguzi na kuchukua hatua za kisheria za wanaohusika kuficha pasipoti za Tanzania

3. Wanapoambiwa kwamba baadhi ya pasipoti zinauzwa kwa baadhi ya makundi ya kihalifu waweze kuchunguza hakuna hatua wanazochukua.

4. Wakati mwingine wanaomba kuwasiliana na mamlaka za Tanzania kuhusu hali hii lakini wanadai, ukirudi nyumbani utaenda kusimulia ndugu zako. Unajiuliza watanzania wasipokwenda kwenye haya Mataifa wao watapata kazi yakufanya? Je wageni wa Mataifa hayo huku kwetu balozi zao zinawadharau hivi?

5. Pamoja na madhila wanayopitia wakirejea Tanzania wanahojiwa na kuwajibishwa kama waalifu wakati ukweli ni kwamba wao ni wahanga tu na serikali ilipaswa kuwawajibisha waliowaajiri kwani mikataba ya ajira wanakuwa nayo

Kwa taarifa za vijana hawa wanasema zaidi ya pasipoti elfu tano zinashikikiliwa na waajiri, wanigeria na wahalifu wengine kutoka Afrika magharibi. Siyo hivyo tu bali pasipoti hizo zinatumika na wageni kufungulia akaunti nakuzituma akaunti hizo kuweka fedha za kihalifu kukwepa kukamatwa(huko kwa wenzetu wanashindwa kutofautisha kama tunavyokwama kuwatofautisha wachina hapa bongo).

Wito wangu kwa serikali nikuhakikisha wanawaelekeza mabalozi wetu huko nje wakusanye taarifa za maeneo zilipo pasipoti zetu na kuwajulisha mamlaka za nchi hizo kuchunguza na kuchukua hatua

Pili, Serikali iwekeze kulinda watanzania waliopo nje ya nchi. Tusiwaone kama wahalifu huku tukikumbatia wageni Nchini kwetu

Tatu, pasipoti zinapotolewa na Uhamiaji zikabidhiwe kwa muhusika. Watanzania wengi wanaingizwa matatani na mawakala wanaosafirisha wafanyakazi nje. Mawakala hawa ndio wanaokabidhiwa pasipoti badala ya pasipoti kukabidhiwa kwa wamiliki.

Nne, serikali ihakikishe wafanyakazi hasa wa kazi za ndani wanaposafiri wanakuwa na mikataba.

Tano, pasipoti zote zilizopotea au zinazoshikiliwa na waajria huku zikiwa zimeripotiwa kupotea zitangazwe adharani Dunia ili kuiwekea ulinzi na uaminifu pasipoti yetu.

Sita, kila Mtanzania anayerejea nchini akiwa amepoteza pasipoti alazimishwe kueleza alipoacha pasipoti yake na huyo anayeishikilia huko nje atafutwe na kuchukuliwa hatua. Uzuri tuna mahusiano mazuri na Mataifa mengi. Hii itawafanya waajiri na wahalifu kuacha kutumia weaknes ya uelewa wa watu wetu kujinufaisha

Nasema haya kwa sababu nina uzoefu, kuna kipindi miaka ya nyuma tuliruhusu pasipoti zetu zikawa vulnerable matokeo yake ilikuwa ukisafiri nje na Pasipoti ya Tanzania unapekuliwa hadi kufikia unavuliwa nguo na hakuna tamko lililotolewa na serikali.

Hali hii inayoendelea ya mabalozi wetu kupuuzia hadhi ya pasipoti yetu huko nje itatupekea watanzania kuanza kupata matatizo tunaposafiri, tinapotafuta vibali, tunapotaka kufungua akaunti za fedha au tunapotaka kutumia pasipoti zetu kama vitambulisho.

TUSIPOILINDA KWA GHARAMA KUBWA PASIPOTI YETU TUKAACHA WATU WAZITUMIE WANAVYOTAKA TUNAKWENDA KUUMIA. MATAIFA YOTE YANAYOPIGANIA DIPLOMASIA YA UCHUMI WANAIPA HESHIMA PASIPOTI.
Umezitajaza nchi za kiislam kwamba zinawadhalilisha watz na hujataja hata nchi moja ya wakiristo wakati nchi za ulaya report inaonyesha waafrika wakiwemo watz wanabakwa sana hadi wanaume.
Kuwa mkweli unapotaka kulisaidia taifa
 
Umezitajaza nchi za kiislam kwamba zinawadhalilisha watz na hujataja hata nchi moja ya wakiristo wakati nchi za ulaya report inaonyesha waafrika wakiwemo watz wanabakwa sana hadi wanaume.
Kuwa mkweli unapotaka kulisaidia taifa
Uisilamu hauna maana ya kutetea Uarabu pale HAKI za Binadamu zinapokiukwa.
 
maxresdefault.jpg
000_1U022D.jpg

Msichana wa Kiafrika akiwa ametupiwa mizigo yake na kuzulumiwa mishahara yote aliyokuwa akiilimbikiza huko Lebanon Uarabuni.

Hata nauli ya kurudi nyumbani hana UTU uko wapi?

Halafu leo kuna Waisilamu njaa wa Kiafrika wanaosapoti Hezbolah.
 
Mbona tumemuona Rose akishindikizwa na waajiri wake na watoto wanamlilia hawataki aondoke?


Mitanzania mingi ni mivivu, wanafikiri wakienda huko kuna kubweteka kijinga au kuna kuwacha kazi wakati wowote kama wafanyavyo wakiwa Tanzania.

huko ukifika kwa kuajiriwa passport inazuiliwa mpaka siku yako ya kusafiri, mwajiri wako ndiyo sponsor wako.

hakuwachii mpaka gharama ulizomuingiza mwajiri kukupeleka zirudi. La hutaki unazilipa unapewa passport yako eyapoti wakati unasafirishwa kurudi kwenu.

Kwani walienda kutalii huko hata wakae na passport?

Kinachotakiwa wapewe elimu ya watacho kumbana nacho huko kabla ya kwenda.
Mengine siyajui maana sijafika huko..
Ila nakubali jambo moja "WATANZANIA NI WAVIVU"
 
Back
Top Bottom