GE2025 Watanzania wamepuuza kampeni za CCM? Au sababu ya ushindani wa upande mmoja?

GE2025 Watanzania wamepuuza kampeni za CCM? Au sababu ya ushindani wa upande mmoja?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Idugunde

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2020
Posts
7,748
Reaction score
10,288
Unaweza kusema zimedolola. Au watu hawana mpango na siasa za uchwara?

Ukiacha zile za Mgombea urais na makamu wake sababu ya watu kusombwa na malori ta mizigo. Kampeni za ubunge na udiwani zimedolola na watu hawazifuatilii kabisa.

Hata zile nazo kama ni ziara za kunadi ahadi.
 
Kama tayari wameshapangiwa Rais, mbunge na diwani, kwanini watu wapoteze muda wao bila sababu?
 
Ukiwauliza mikoa ambayo wagombea Urais wametembelea hawawezi kukujibu
 
Kampeni zenyewe zinakatisha tamaa.
Baada ya wagombea wa ccm kuhakikishiwa ushindi, hawana tena la kuwadanganya wananchi zaidi ya porojo.

Huko Arusha Makonda amewaahidi wapiga kura kuwaletea mcheza filam mashuhuri Arnold Schwarzenegger January mwakani.
Anadai ameshawasliana naye.
Sasa vituko kama hivi nani apoteze muda wake!?
 
Tumejifunza wanasiasa ni watu wako kazini, heri tufocus na maisha yetu kuliko kuwa mashabik wa wanasiasa ambao wakifanikiwa ni kwa faida yao na watoto wao... mimi mtoto wangu atasoma kayumba na atabaki akilalamika hajapata kaz...utanitoaje nikakushabikie maisha yako binafsi mzee
 
Bila ya kuwepo mpizani nguli Tundu Lissu na Chadema team kwenye hizi kampeni ni sawa na bungeni wakati wa Magu.
 
Tumejifunza wanasiasa ni watu wako kazini, heri tufocus na maisha yetu kuliko kuwa mashabik wa wanasiasa ambao wakifanikiwa ni kwa faida yao na watoto wao... mimi mtoto wangu atasoma kayumba na atabaki akilalamika hajapata kaz...utanitoaje nikakushabikie maisha yako binafsi mzee
Haaaa awa wakiingia bungeni tutaona mziki wake .....siasa ndo huamua hata tunavyofanya shughuli zetu tuna miaka Mitano ya balaa
 
Back
Top Bottom