Watanzania wameshindwa kununua hisa za Vodacom, imefunguliwa kwa Wakenya

He he..Siwezi thubutu kununua chochote huko bongo. Hujui magu atakurupuka lini aseme wewe Ni mwizi.
Bora ukae huko huko, maana hujui kuwa magu huyo ndo kasababisha haya makampuni ya simu yauze 25% ya share zake kwa locals!
 
Suala la hisa za voda lina sababu nyingi sana, na kwenye uzi ule wa kwanza tulitoa sababu nyingi sana na za msingi kabisa!

Leo ntachangia kidogo sana!

Nianze kwa kukukumbusha kuwa kwa sera ya NEEC (National Economic Empowerment Council) kila kampuni ya simu inatakiwa kuuza 25% ya hisa zake kwa wananchi! Hivyo mitandao yote iliyopo tz ie, Vodacom, Airtel, tigo, zantel, Halotel na ttcl zinatakiwa kuuza hisa hizo!

Vodacom ndo walikuwa wa kwanza kufanya hivyo, lakini walikosea maana wao au NEEC haeakutoa elimu ya kutosha kuhusu ununuzi wa hisa! Pia muda waliweka mfupi sana!

Ikumbukwe pia kuwa Vodacom ni mtandao unaolalamikiwa sana na wateja kwa kutoza gharama kubwa kwenye huduma zake, hivyo mtandao huu umeanza kupoteza wateja kwa kasi kubwa sana!

Kutokana na hilo, wateja wenyewe wa mtandao huu ambao kiuhalisia ndo wanatakiwa kutoa hamasa kwa wengine kununua ndo walikuwa wa kwanza kuuponda na kusubiri mitandao mingine iuze hisa zake ili wanunue!
 
Bora ukae huko huko, maana hujui kuwa magu huyo ndo kasababisha haya makampuni ya simu yauze 25% ya share zake kwa locals!

Huyo Magu mwenye Juzi alikuwa akitishia eti ni kwanini haya makampuni hayarecord profit? Haya. Wacha nikueleze jambo sasa. Huo upuuzi alioufanya Magufuli kabla hajafikiri kuhusu demand ya Hisa zenyewe ndio utabackfire. Sasa unataka kuempower watu amabo hawafuatili soko lahisa? Ikiwa mimi hapa Kenya najua, kwani Watanzania wanangoja lipi ili wajulishwe?

Kuwachezea individual buyers ni rahisi sana. Weka tu bei ya hisa iwe juu na wananchi hawatanunua. Kwani utailazimisha kampuni iize hisa zake kwa bei ya chini? Ni Watu wangapi amabo wanajua kufanya valuation ya Kampuni?
 
Then kama Vodacom wameamua kuweka bei kubwa ya hisa (kitu ambacho watu walisema wamefanya makusudi) bado tunazo kampuni nyingine tutanunua! airtel, tigo, halotel, zantel zote hizo tutanunua!

By the way unaaandaliwa muswada wa kuyawezesha haya makampuni kuingia DSE na kuorodhesha transactions zote! So wizi tz tinaukata hvo
 
Tatizo si Voda bali Magufuli ndio tatizo
Hizo Hisa zingeweza nunuliwa na watu 100 tu zikaisha zote
Mo angeweza weka hata 100bil, kina Mengi etc
 
Nunueni hisa Wakenya
 

Huoni kuwa aim ya Magu itakuwa imeshindwa? Haya makampuni mengi e pia yatafanya tu hivyo
 
Haitashindwa hata kidogo, subiri muswada uende bungeni utarudi hapa kusema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…