ArD67
JF-Expert Member
- Nov 14, 2016
- 2,817
- 2,044
Naijua hiyo uiitayo kadhia kwa wafugaji, kwa taarifa tu. Elimu juu ya ufugaji na si uchungaji imetolewa ukanda wote huu. Mwanzoni, faini ilikuwa ndio njia ya kulirekebisha hili tatizo, wachungaji wakawa ni wakaidi kupindukia kwa kiburi cha fedha. Kwamba watalipa tu faini yataisha.Si ajabu kama unavyosema bali ni mshangao. Ni mfumo uliokuepo uliruhusu watu kufika huko!! Na ni mfumo huo ndio unawatia hasara wananchi wake!! Ni sawa mfumo ulioruhusu watu kuazimisha vyeti kuingia kwenye kazi ikiwemo majeshi yetu na ni mfumo huo huo umewazika hata pensheni zao!! .
Ninachosema kosa lilikuwa la nani?! Na kwa nini wawajibishwe wananchi masikini kwa kigezo cha uchapakazi!! Je mfano (serikali) imewajibika vipi kwenye kadhia hizo badala ya mzigo kumpata mwananchi pekee. Ndipo hapo ninaposema mfugaji mTz angepigwa faini na kufukuzwa ktk maeneo hayo yanayodhaniwa kuwa ni hifadhi. Badala ya kumrudisha mwananchi katika ufukara kwa kumdhulumu!! Tujiangalie kuwa matatizo yalianzaje?!
Labda nikuulize tu jambo moja, unaona kuweka hifadhi mbalimbali ktk nchi ni jambo lisilo na maana yoyote? Jibu lako lita justify uwepo wa hizi sheria ama kujustify yale yatendwayo na wachungaji wetu. Elimu juu ya ikolojia ikuongoze ktk kupata jibu sahihi.