Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Watanzania,
Ningependa kusema ya kuwa Lissu atahangaika sana,ataongea sana lakini kamwe na katu hataweza kumchafua wala kushusha imani waliyonayo watanzania kwa Mwamba Mwenyewe Paul Christian Makonda Kijana Jasiri kusini mwa jangwa la Sahara.
Ambayo imejengwa katika misingi ya uchapakazi, uzalendo,utu,huruma na ujasiri Mkubwa alionao Mwamba Mwenyewe Paul Makonda .ambaye amekuwa mtetezi wao kwa kila nafasi anayoipata na kuaminiwa na Mheshimiwa Rais ya kuwatumikia watanzania.
Nimesikia akiongelea na kujaribu kumchafua Mwamba Makonda kuwa Kwanini ameteuliwa ukuu wa Mkoa Wakati anatuhumiwa kupora vitu kama vile magari ya watu. Swali la kumuuliza lissu ni kuwa ni nani huyo aliyeporwa magari? Ni nani huyo aliyeporwa mali na Mwamba Makonda?
Kesi ipo katika mahakama ipi na ni kesi namba ngapi ya mwaka gani? Mwenendo wa kesi umefikia wapi? Inasimamiwa na jaji yupi? magari hayo yaliyoporwa ni aina gani?,namba zake zipo wapi? Nyaraka za magari hayo zipo wapi kuthibitisha uporaji huo? Kwanini lisu anatuhumu bila ushahidi wa aina yoyote ile?
Anaposema Mwamba Makonda alizuiliwa na Marekani kwa sababu ya kufanya vitendo vya kihalifu .swali ni kuwa Marekani ni nani?
Je, siyo Marekani huyo huyo aliituhumu Ilaki chini ya Saddam Hussein kuwa Inamiliki silaha za Maangamizi? Je mumewahi kuonyeshwa silaha hizo za maangamizi? Mumewahi kuonyeshwa kiwanda cha silaha hizo na shehena ya silaha hizo za maangamizi zilizokutwa?
Je, siyo Marekani hiyo hiyo ilimtuhumu Muamar Gaddafi kuwa anaua watu wake na kwamba anakandamiza demokrasia? Je tangia amefariki Gaddafi mmeiona hiyo democrasia Libya? Je maisha waliyoishi Walibya chini ya Gaddafi ndio haya wanayoishi Walibya Leo? Libya ya Gaddafi ndio hii ya Sasa? Je, kuna amani tena Libya? Kuna utulivu? Kuna demokrasia?
Hamuoni zilikuwa ni hujuma tu za Marekani? Hamuoni na kufahamu ya kuwa vita ya Marekani na hasira zao ilikuwa ni kitendo cha Mwamba Mwenyewe Paul Makonda kupiga vita sana Mashoga na watu wote waliokuwa wanajihusisha na vitendo vya kishoga? Je, hamfahamu kuwa Marekani inaunga mkono vitendo vya kishoga kwa kauli ya haki za binadamu? Hamfahamu kuwa Marekani inapambana sana na kwa gharama kubwa na kwa kila aina ya ushawishi kuingiza uchafu huo wa ushoga barani Afrika? Je, wewe mtanzania mwenye akili Timamu na mwenye hofu ya Mungu unaweza kuunga mkono ushetani huo?
Sasa kwanini msifahamu na kuelewa ya kuwa Mwamba Makonda alichafuliwa na Marekani kwa sababu tu ya kitendo na hatua zake za kupinga ushoga hadharani?
Kwa hiyo niseme wazi kuwa lissu hawezi kumchafua Mwamba Makonda kwa namna yoyote ile ,wala kuondoa Imani kubwa waliyonayo watanzania kwa Mwamba Mwenyewe Paul Makonda. Lissu atahangaika sana pengine kwa kutumiwa na wabaya wa Mwamba kujaribu kumpaka matope ,kumshushia heshima,kumtoa kwenye reli,kumvuruga ,kumnyong'onyesha na kumdhoofisha lakini kamwe hataweza kufanikiwa hata kidogo.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.