Ndio biashara huria hiyo
Kila mtu apange bei yake
Na ndio watu wanaouza bei halisi jiwa nanunua sana vitu vyao
Kuna kipindi fulani nilikuwa naenda kariakoo kununua vifaa vya electronics bei zilikuwa balaa unazunguka wee na wanaanzia juu kichizi ili mshushane mpaka chini
Kitu cha 200k atakwambia 350k ili mbishane weee ndio akuuzie
Katika pita pita moja hapo nishachoka nikaona duka moja kuulizia tu naambiwa 190k, nilishtuka nikajua feki ila kuitazama sababu naijua nikakuta original
Toka siku hiyo ndio likawa duka langu mpaka kesho nikitaka chochote huwa naanzia hapo kwanza
Kuuza bei halisi kunaleta sana wateja