Mwongozo wa sheria zetu upo wazi kabisa:
1) Ukishirikiana au kumsaidia yeyote kufanya uhalifu, na wewe unakuwa ni sehemu ya uhalifu, na ukifahamika, unastahili kushtakiwa.
2. Nchi yetu imeishi kwenye uhalifu wa kutisha kwa muda mrefu. Uhalifu kama ule wa kuteka na kuua watu; Uhalifu kama ule wa kuunda tume huru bandia ya kusimamia uchaguzi, uhalifu kama ule wa Serikali na watendaji wake kuandaa chaguzi bandia na kisha kuwatangaza watu ambao hawakuchaguliwa na wananchi kuwa viongozi wao.
3. Sheria zetu zinazuia kushirikiana na mtu mhalifu au taasisi ya kihalifu katika kutekeleza uhalifu, hivyo walioshiriki uchaguzi bandia huku wakijua kabisa uchaguzi huo ni bandia na unasimamiwa na tume huru bandia, nao ni wahalifu sawa na aliyeunda ile tume bandia, sawa na wale wasimamizi wa uchaguzi waliotengeneza na kupika matokeo. Baada ya kugundua kuwa Rais alikuwa ameunda tume huru bandia ya uchaguzi, ilistahili wananchi wote wafuata sheria na katiba ya nchi kujitenga naye mara moja, kwa sababu kushirikiana naye ilikuwa ni kushiriki uovu wake.
4. Kutokana na mauaji ya kutisha yaliyofanyika Oct 29, ambayo yalikuwa ni uhalifu mkubwa kuliko wowote uliowahi kutokea dhidi ya wananchi, kama hitaji la kisheria na la kikatiba tunatakiwa kujitenga na kujiweka mbali kabisa na wauaji wote ili tusiwe sehemu ya uovu wao:
-jitenge kabisa na CCM, hawa ndio wenye serikali, na serikali ndiyo iliyoandaa na kuamrisha mauaji.
- jitenge kabisa na samuya maana huyu ndiye mwenyekiti wa chama cha mauaji, na ndiye amiri mkuu wa wauaji wote.
5. Kuendesha uchaguzi bandia ni jinai, ni uhalifu dhidi ya jamhuri. Mtanzania mzalendo unatakiwa kujitenga kabisa na kujiweka mbali kabisa na walioandaa huo uchaguzi halifu, na wote ambao ni matokeo ya huo uhalifu. Hutakiwi kushirikiana, au kutii maelekezo ya kiongozi ambaye ni zao la uovu. Kutoa ushirikiano au kutii maelekezo ya mwovu, ni kushiriki uovu wake, ambalo ni kosa kubwa dhidi ya Jamhuri.
6. Wajibu mkuu wa kiraia, ni kwamba ukiona kuna mazingira ya kuwezesha uhalifu kutokea, unatakiwa kujitahidi kwa namna yoyote inayowezekana, kuzuia uhalifu usitokee. Vijana walioandamana kupinga uchaguzi bandia, ni wazalendo wa hali ya juu sana, na mashujaa wa wa taifa, kwa sababu walitumia uwezo wao wote kutaka kuzuia uhalifu. Watu hawa, wengi wao wamepoteza uhai wao kwaajili ya kulitetea Taifa.
ANGALIZO KUU:
Kama watu kwa maelfu wamepoteza uhai wao kwaajili ya kuzuia uhalifu dhidi ya Taifa, halafu sisi tulio hai, tukawakubali viongozi ambao ni zao la uovu, yaani waliotokana na tume bandia, uchaguzi bandia, kura bandia, mauaji ya wazalendo wa Taifa, HAKIKA SISI TUTAKUWA NI WASALITI WAKUBWA KWA TAIFA NA KWA NDUGU ZETU WALIOUAWA WAKIPIGANIA KUZUIA UOVU DHIDI YA TAIFA.
WITO MKUU
Jitenge kabisa na viongozi waliotokana na uovu, na watu binafsi na vyombo vyote vilivyoshiriki kwenye uovu wa kuwaua ndugu zetu, ili tu waweze kuwapachika viongozi haramu.