Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Imekuwaa tooo much, ukiulizaa mtu anajibu kijeurii hamia Burundi kwa hii nchi ni ya wakina nan??Kuna uonevu mkubwa unafanywa na Serikali kiasi cha kufika kiwango cha kutovumilika zaidi ya kujiongeza kama watanzania.
Double taxation ni kitu hakiruhusiwi kwa mujibu wa sheria za kodi.
Mtumishi wa umma ndo limekuwa jalala sasa, ulipe PAYE, KODI, VAT, TOZO....Tusiseme wote sioo watumishi ila kuna ndugu zetu....ni watumishi...
Wao hawajalii kabisaa ni kutukamua tu...mita za umeme, vocha, bando, dukani kwa mangi.
Anzisha biashara sasa uone hiyo kupelekewaa moto....TRA, LESENI, TAKA, OSHA....yaani ukiritimba kila sehem.
Nauliza tuandamane muda huu au tusubili sensa ya watu na makazi iishee....tumechokaaaaa.
Nchi za wenzetu umeme kukatika tu wanaiwajibisha serikali, Watanzania tutalala mpaka lini....??
Mafuta ya kula juu, chakula juu, mfumko wa bei juu, kila kitu unaenda dukani leo kinauzwa bei hii ukirudi kesho bei imebadilika mpaka lini hayaaa???
Naomba kuwasilisha