Nkerebhuke
JF-Expert Member
- Nov 1, 2021
- 796
- 2,026
Huwa nakaa najiuliza nani alituletea hili balaa maana imefika kipindi unaona kabisa jinsi gani watanzania wanashindwa kujali na kathamini taifa lau zaidi ya umaarufu binafsi wa kiongozi mkubwa wa nchi. Tabia ya viongozi kujenga umaarufu binafsi kuliko hata taifa lenyewe limezaa balaa kwenye nchi yetu maana kumezaa machawa na walamba asali ambao wanaamini kiongozi hakosei na wala hapaswi kuelekezwa jambo.
Pia soma: Watanzania wanawaza kumtukuza mtu au Rais kuliko taifa lenyewe
Kama kuna muhasisi wa hili jambo ametuletea balaa maana watu wetu hawataki tena kuelimika na kujifunza wanapenda kusikia nani kakosea, nani kasema hivi au nani katumbuliwa. Zinaimbwa nyimbo nyingi za kumtukuza raisi kuliko hata taifa lenyewe ambalo ndio msingi wa hatma ya kizazi kijacho.
Taifa letu linapita kwenye hali ngumu ya mfumuko wa bei, elimu yetu kudumaa, ukosefu wa ajira kupita kiasi na changamoto tele cha ajabu tuko bize kusifia na kulaumu viongozi wakuu waliopo na waliopita. Tumejaa ubinafsi, uroho, ujuaji na ujinga wa kuwasujudia viongozi badala ya kuwapa changamoto ili kuwaonesha tunataka nini kwa future ya watoto wetu. Watanzania tubadilike.