GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Inaonekana ni kati ya mazao yanayouzwa ghali sana. Sisi tunaoishi mikoa ya mbali na korosho inakolimwa, tumekuwa tukiuziwa korosho za kutafuna kwa bei isiyobadilika, miaka nenda miaka rudi. Kwa bei tunayouziwa mitaani na supermarket, inatoa picha kuwa ni bidhaa ghali kuzidi karanga, n.k.
Lakini sijawahi kusikia mtu ambaye amekuwa bilionea au hata milionea kupitia kilimo cha korosho.
Ni kwamba hawapo au wahusika wanajitahidi kujizuia wasijulikane?
Korosho ni ghali Tanzania, na inasemekana, huko ng'ambo, bei yake "haikamatiki"
Kulikoni hatuwasikii mabilionea waliotokana na kilimo cha korosho?