Watanzania wapo kwenye njia panda baina ya Kiswahili na Kingereza


Wacha kudandia treni kwa mbele, umekurupuka hata huonekani kuelewa tunajadili kuhusu nini, au mada imetokea wapi, unajibu ilmradi uonekane na wewe upo.

Hakuna sehemu nimebisha kwamba kuna mataifa yasiyokitumia kingereza, mbona yapo tu mengi ambayo yana lugha zao za asili walizoanza kuzitumia viwandani zaidi ya miaka 500 iliyopita hata kabla kingereza hakijafika kwao, lakini muda wote nasisitiza umuhimu wa kingereza ambao umesaidia watu wa matabaka mbali mbali kukutana na kujadili. Ni kama vile Mnyakyusa akitokea kijijini akutane na Msukuma inawabidi watumie Kiswahili. Ni issue ndogo sana ya kueleweka na mtoto wa chekechea, tatizo lenu huwa mumeganda kiakili hata ukiambiwa vipi huonekani kuelewa.

Na hakuna sehemu nimesema kuongea kingereza ndio ishara ya kuwa una akili sana, ila pia ina hadhi yake maana ni second language kwetu sisi hivyo ina maana umetia jitihada kwa kutumia ubongo wako kujifunza lugha ya pili. Na pia utafiti wa kisayansi uligundua watu wenye uwezo wa kuongea lugha kadhaa wamepevuka kiaina.

Sisi Wakenya tunakipenda Kiswahili, tunakitambua kama lugha yetu ya taifa, tunakifunza mashuleni, tunakitumia kitaani.....lakini tofauti yetu na nyie ni kwamba sisi hatujaganda kwenye lugha moja kama mazombi, tunajitahidi kuendana na wakati, tunajifunza na kutumia kingereza pia, na zaidi tunahamasisha watoto wetu wajifunze lugha zetu za asili za Kiafrika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…