Watanzania Washangazwa na Ujasiri wa Msanii Bien akiimba "Ruto Must Go" huku Wakenya wakiitikia

Watanzania Washangazwa na Ujasiri wa Msanii Bien akiimba "Ruto Must Go" huku Wakenya wakiitikia

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
2,818
Reaction score
7,940
Msanii kutokea Bien akifahamika kama Bien-Aimé Baraza kutokea kundi la Saut Sol pale nchini Kenya amefanya show katika moja ya Tamasha kubwa nchini Kenya na kuacha watu kinywa wazi huku Wakenya wengi wakifurahia kibao alichutumbuiza kwa kukipiga mubashara akiimba "Ruto Must Go" huku Wakenya wakimfuatilizia.

Nchi ya Kenya ni miongoni mwa Nchi chache barani Afrika ambazo Raia wake wana uhuru wa kuwakosoa viongozi au uongozi kwa uwazi endapo wanahisi ukiritimba au matakwa ya kiraia yasipotimizwa. Na serikali inaheshimu maamuzi ya Raia kwa kiasi kikubwa.

Watanzania wengi washangazwa na uhuru wa Raia na wasanii wa Kenya, ambapo wengi wakitoa maoni ya kuwa ingekuwa ni Diamond Platnumz, Chibu Dii Chibu Dee Simba uenda angekuwa kashapigwa pini na angetafutiwa kosa la jinai na biashara zake zikiletewa fitina, jambo linalopelekea wasanii wengi kufyata mikia na kuunga mikono juhudi na wengine kuwa Chawa au kwa kimombo "Lice" wa viongozi wa chama tawala. Watanzania wengine wakisema kuwa sisi watanzania ni waoga jambo ambalo ni udhaifu, na viongozi utumia udhaifu huo kuwadidimiza watu wanaojaribu kuwaamsha wananchi dhidi ya mageuzi, huku kukiwa na utekaji au upoteaji wa watu wanaoleta hisia za mageuzi kwenye jamii.

Video ya Bien akiimba Ruto Must Go

 
Huku wasanii wote takataka kutwa...
IMG-20241007-WA0000.jpg
 
Back
Top Bottom