Watanzania wasomi na wasio wasomi lakini ni wajasiriamali acheni kukodi fremu ili kufungua biashara

Watanzania wasomi na wasio wasomi lakini ni wajasiriamali acheni kukodi fremu ili kufungua biashara

Tatizo la Door to door ni Moja, Kuna wateja wanataka walione duka lako lipo wapi, hapo tegemea kuwakosa wateja wa aina hiyo maana wanaamini kwenye mambo ya guarantee hasahasa kama unauza electric appliances.
 
Hii tabia imekithiri sana hapa nchini. Utakuta mjasiriamali analipa pesa nyiiiingi kulipia chumba cha duka akitarajia kupata pesa nyingi, ni kosa kubwa sana.
Mkuu kuna biashara ambazo mamlaka hazikupi kibali kama hawajakagua frame yako unayotaka kufanyia biashara.

2. kuna baadhi ya wateja wanalipia huduma kisha wanakuja kuifuata Ofisini, Mtu hawezi kukuachia 3M na wakati hajaona Ofisi yako.

3. Ofisi inaipa thamani biashara yako, ukiwa na Ofisi nzuri una uwezekano wa kufanya biashara kubwa hata kama Mtaji wako ni Mdogo(ina Ongeza imani kwa Wateja). Nenda Frame za Sinza utaelewa hili.

4. Nadhani ungeshauri watu wachukue frame za bei nafuu pale wanapoanza ujasiriamali.

5. Mitandao hutumika kupata wateja, ila wote unaowapata mitandaoni LAZIMA wahitaji Ofisi yako ilipo ili kujiridhisha kuwa wewe sio Tapeli.

Asante.
 
Mambo mengine mnajumuisha sana
Sijui hamuwazii..

Pub inawezaje kufanya door to door? Au niweke tangazo online halafu waje kunywea geto kwangu?

Duka la mangi linawezaje kua door to door?

Banda la chips, nitembee na jiko kama muuza kahawa? Au uweke oda online halafu nije kukaangia nyumbani kwa mteja?

Hiyo ni mifano michache

Hakuna hela rahisi. Lazima uwe dhabiti kwenye biashara yako ili usiende tuu kufaidisha landlord. Frem milioni na bado biashara tunafanya.

Kama hutaki frem, kua dalali wa maduka ya watu, kishoka, nyoka.

Hiyo online itumike effectively kufanya marketing, ila physical address ni lazima.

Ntachomaje kuku door to door, au nitembee na jiko langu kwenye toyo. Online barbeque
 
Jamani eeh, kukodi fremu ufungue duka unapoteza hela zako. Somo hili kichwa cha habari hii kinahusika.

Hii tabia imekithiri sana hapa nchini. Utakuta mjasiriamali analipa pesa nyiiiingi kulipia chumba cha duka akitarajia kupata pesa nyingi, ni kosa kubwa sana.

Njia zifuatazo zinaweza tumika badala ya kumfadisha landlord's.

1. Tangaza biashara yako pelekea wateja wewe mwenyewe (huu mfumo door to door upo lkn kidogo sana)
2. Tumia social media kuuza bidhaa.

Mimi Nina Depo la vinywaji natakiwa kuwa na sehemu ya kuweka kreti empty na zenye bia na soda
Natakiwa kuweka ma caton ya maji na vinywaji vyengine.

Hivyo unanishauri nini?

#YNWA
 
Jamani eeh, kukodi fremu ufungue duka unapoteza hela zako. Somo hili kichwa cha habari hii kinahusika.

Hii tabia imekithiri sana hapa nchini. Utakuta mjasiriamali analipa pesa nyiiiingi kulipia chumba cha duka akitarajia kupata pesa nyingi, ni kosa kubwa sana.

Njia zifuatazo zinaweza tumika badala ya kumfadisha landlord's.

1. Tangaza biashara yako pelekea wateja wewe mwenyewe (huu mfumo door to door upo lkn kidogo sana)
2. Tumia social media kuuza bidhao biashara zote
Siyo biashara zote zinahitaji huduma ya mlango kwa mlango, (delivery services) mfano ya ufundi ambayo niyakuuza akili na nyingine nyingi lazima uwe na ofisi kuna mambo mengi ya muhimu kwanini kuna haja ya kuwa na ofisi
 
Jamani eeh, kukodi fremu ufungue duka unapoteza hela zako. Somo hili kichwa cha habari hii kinahusika.

Hii tabia imekithiri sana hapa nchini. Utakuta mjasiriamali analipa pesa nyiiiingi kulipia chumba cha duka akitarajia kupata pesa nyingi, ni kosa kubwa sana.

Njia zifuatazo zinaweza tumika badala ya kumfadisha landlord's.

1. Tangaza biashara yako pelekea wateja wewe mwenyewe (huu mfumo door to door upo lkn kidogo sana)
2. Tumia social media kuuza bidhaa.
Hii ni kweli ila kuna muda biashara yenyewe inakulazimisha uwe na eneo official

Pia inategemea aina ya biashara pia

JM

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamani eeh, kukodi fremu ufungue duka unapoteza hela zako. Somo hili kichwa cha habari hii kinahusika.

Hii tabia imekithiri sana hapa nchini. Utakuta mjasiriamali analipa pesa nyiiiingi kulipia chumba cha duka akitarajia kupata pesa nyingi, ni kosa kubwa sana.

Njia zifuatazo zinaweza tumika badala ya kumfadisha landlord's.

1. Tangaza biashara yako pelekea wateja wewe mwenyewe (huu mfumo door to door upo lkn kidogo sana)
2. Tumia social media kuuza bidhaa.

Hivi unawajua wateja wa bongo lakini?.
kwa wateja wa bongo location muhimu.
 
Tatizi sio kukodi frem tatizo eneo fanya kwanza research makini mi mtu hajawai fika hata uo mtaa kisa dalali kampamba analipa miezi sita anakaa mwezi mzima wateja wawili watatu anaamua kuhama kapteza pesa na muda kuna biashara zingine unaweza deliver kama nguo .nk haina haja ya kufunguwa frem kama ndo unaanza anzia online na sehem za bure
 
Kuna mtaa fulani niliambiwa watu wanalipia laki nne kodi ya nyumba bado kodi nyingine nikawaona wajinga sana afu wameweka vipodozi tena reja reja aiseee.
Unajua wanapata sh ngapi??

Ni sawa na uende mahali unakuta kuna maduka hayana vitu vingi kwenye mashelf ukawacheka kua wanapoteza pesa kumbe wenzio wanakwepa kodi mzigo unauziwa store huko pale ni geresha tu.

Kama anapata hasara angefunga, kama bado anailipa hiyo laki 4 kila mwezi basi jua wanapiga pesa.

Tena hiyo biashara ya vipodozi ina uhuni mwingi kishenzi.
 
Kuna mtaa fulani niliambiwa watu wanalipia laki nne kodi ya nyumba bado kodi nyingine nikawaona wajinga sana afu wameweka vipodozi tena reja reja aiseee.
Unaweza ukamuona mjinga anauza vipodozi Ila biashara yake haswa sio vipodozi vipodozi geresha tu, Pesa utafutaji una Siri nyingi usimdharau mtu kwa kila Jambo unaloliona mfuate umuulize unalipa pango laki 4 kwa mwezi unauza vipodozi rejareja kwa mwezi hauingizi hata laki hio Pesa ya pango unalipaje atakachokuambia nahisi utabaki mdomowazi, analipa laki 4 anaingiza milioni 4 sasa laki 4 ni nini kwenye million 4?
 
Back
Top Bottom