Watanzania Wawili wakamatwa South Africa na Madawa

Habari ime conclude kwamba hawajatajwa majina lakini.weye heading yako yadai ni wa tzn
 
Hatimaye matokeo ya kutaka utajiri wa haraka yameanza kuonekana, wahenga walisema tamaa mbele mauti nyuma!
 
Huyu mtoto mbona anatumiwa kitambo kupeleka unga south....halafu bado mshamba,mtu mwenyewe anaemtumia anamkopa na kuumpa pesa mbuzi......trip zote za south hata gari hana

Nani?mbona hatujatajiwa majina au wewe unamjua!?tutajie nasi tumjue mkuu.
 
hawakusema kuwa ni watanzania bali waliwasili na ndege kutoka tanzania.....
 
Maisha magumu na tamaa ya utajiri wa mapema ndio sababu
 
qeen video mwenye makalio makubwa

hawa madada zetu tamaa nyingi wana kasi ya malengo wema anaendesha vogue binti kiziwi yupo behind bars agnes masogange kakamatwa na sembe wolper magari kibao kazi au dili zinazoeleweka hawana! Amani kwa kaka voda milionea waambie masela wako waache poda wale mmea.
 
6bil=150kilo that means Kilo moja ya poda ~ 40mils binti wa liumba alikamatwa na kilo ~200
 
alianzia safari Dar,washikiliwa Afrika Kusini

Mizengo Pinda


Wanawake wawili raia wa Tanzania wametambuliwa kuwa ndiyo wanaodaiwa kuingiza shehena ya dawa za kulevya zenye thamani ya zaidi ya Sh. bilioni 6.8 nchini Afrika Kusini wakitokea Tanzania.

Akizungumza na NIPASHE jana, Kamanda wa Polisi Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Geofrey Nzoa, alisema haijafahamika wanawake hao wanatoka mikoa gani.

Kamanda Nzoa aliwataja wanawake hao kuwa ni Agnes Jerald ambaye alisema hajapiga hesabu ya umri wao, ila alizaliwa mwaka 1988 kwa maana hiyo ana umri wa miaka 25 na Melisa Edward ambaye alisema amezaliwa mwaka 1989 kwa maana hiyo atakuwa na umri wa miaka 24. Wawili hao bado wanaendelea kuhojiwa na polisi wa Afrika Kusini.

Alisema Jeshi la Polisi Nchini kwa upande wake linaendelea kufanya uchunguzi kubaini kama dawa hizo walitoka nazo wapi na pia linawasaka watu ambao watakuwa ndiyo wamiliki wa dawa hizo.

Jumapili iliyopita NIPASHE ilipata taarifa za kukamatwa kwa dawa za kulevya aina ya Crystal Methamphetamine zenye thamani hiyo nchini Afrika Kusini wakati zikisafirishwa kutoka Tanzania.

Taarifa hizo zilionyesha kuwa wanawake wawili walikamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Oriver Tambo uliopo eneo la Kempton Park siku ya Ijumaa wiki iliyopita wakitokea Tanzania.

Wanawake hao walikamatwa na maofisa wa Mamlaka ya Mapato ya Afrika Kusini wakiwa na masanduku sita ambayo yalipokaguliwa yalikutwa na takribani kilo 150 za dawa hizo ambazo pia zinajulikana kama ‘Tik’ zikiwa na thamani ya bei ya mtaani ya Randi milioni 42 sawa na Sh. bilioni 6.8.

Baada ya kukamatwa na dawa hizo wanawake hao walikabidhiwa polisi.
Tukio hilo linatoka takribani wiki moja baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Juni 28, mwaka huu kutangaza kuwa tatizo la dawa za kulenya hivi sasa ni janga la kitaifa nchini.

Alisema kumekuwa na wimbi kubwa la Watanzania wanaojiingiza katika biashara haramu ya dawa za kulevya ndani na nje ya nchi na kwamba, katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, watuhumiwa 10,799 walikamatwa kwa kujihusisha na dawa hizo.

Pia alisema katika kipindi hicho, Watanzania 240 walikamatwa katika nchi za Brazil, Pakistan na Afrika Kusini, na hivyo kuharibu taswira ya nchi na kusababisha Watanzania wasio na hatia kupata usumbufu na masharti magumu wanapotaka kusafiri kwenda nchi mbalimbali duniani.

Pinda alisema mwaka huu pekee kumekuwa na ukamataji mkubwa wa dawa za kulevya katika eneo la kimataifa la Bahari ya Hindi karibu na Tanzania.
Alisema hivi sasa mikate, maandazi na askrimu zinazouzwa kwenye shule za msingi, zinawekwa dawa za kulevya.

Alisema vitendo hivyo vinafanya vijana wengi wa shule za msingi na hata sekondari kuwa na tabia za ajabu, ikiwamo kuingia darasani wakiwa na kiatu kimoja mguuni, mkufu wenye nyembe na kidani chenye nyembe kifuani.




CHANZO: NIPASHE
 
jaman Hawa watoto wa mji kwa kupenda maisha ya haraka na starehe ndo yanayowakuta sasa,amuombe mungu wake amsaidie sasa
 
dah dem mkali kinyama lakin ndo ivyo anaenda kuozea jela!
 
Haya niliyatarajia sana tu,...kwa hawa dada zetu walivyo na papara na utajiri wa kuiga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…