Mama!
Asilimia kubwa ya watanzania hawalimi,hawafanyi biashara,hawana elimu!in general hatufanyi kazi yaani ni wavivu!Hivyo basi kuuondoa umaskini lazima kuwe na self commitiment kuanzia kwenye kaya hadi kwenye taifa!
Thanks to God tuna kila kitu ila ndo hivyo hatujui kuvitumia najua masikio ya waafrica wengi yako kusikia G8 wameongeza dau gani la msaada!
katika Taifa pia ni lazima viongozi wawe waaminifu kwa taifa lao na si kushiriki katika Rushwa na kuiuza nchi yao!Unajua umaskini unapimwa pia kwa kuwepo na wawekezaji wengi kutoka mataifa ya nje hii inamaanisha serikali imeshindwa kujiendesha na ndo khali tuliyonayo kwa sasa!
In short kazi ipo ila tunahitaji kujitoa ki ukweli kuanzia katika kaya hadi taifa kuumaliza umaskini!kwa kutumika katika uzalishaji naamini tumake POVERTY A HISTORY!
Wakuu,
"Ili kujipatia maendeleo, tunahitaji vitu vinne, 1. Watu 2. Ardhi 3. Siasa safi na 4. Viongozi bora." JKN.
Tanzania kama nchi si masikini hata kidogo, nchi hii ina utajiri wa hali ya juu kabisa kuliko nchi nyingi nyingine duniani.
Kama ni hivyo kwa nini sisi watanzania wenyewe tu masikini wa kutupwa. Ndio, sisi ni masikini sana pampja hata na wale wenye vijisenti. Nao pia ni masikini wa kutupwa. Tuna umasikini wa mali, wa ujinga na wa uwoga.
Iweje baada ya miaka 50 ya uhuru tuwe tumo katika hali hii. Maradhi hayatubanduki, umasikini umetuzonga, ujinga umetutapakaa, rushwa imetuzagaa na ufisadi umetuvaa na sisi tumekaa tunakodoa macho tu.
Msingi wa umasikini wetu ni "inaction." Hakuna kitu kibaya kama kutokufanya kitu. Watu tunao na ardhi tunayo, lakini je, siasa yetu ni safi? Viongozi wetu je? Ni bora?
Madini yetu tu, yangetosha kutupunguzia umasikini kama siyo kutuondolea kabisa. Tungechimba na kuyasafisha, kuyakata, kuyatengeneza na kuyauza wenyewe. Na kama tunashindwa, tungeweka masharti ambayo yangetunufaisha kwa wawekezaji.
Kwa mfano, tungemwambia mwekezaji sisi ndio wenye mali yetu hapa ni 51% na wewe ni 49%. Unapokuwa hapa 5% ya wafanya kazi wataalamu ni wako na wafanya kazi 95% ni wetu na baada ya miaka 10 hao wataalamu 5% wawe watu wetu uliowafundisha. Unataka chukua, hutaki tusalimie. Huyo ndio masikni jeuri. Miaka 50 hii tungekuwa tumeshafikia mahali panapoonekana.
Kama hujala, utakosa wapi kuwa mvivu? Njaa inatuzagaza nje ya nchi. Iwe njaa ya mali au elimu.