...mtanzania mambo yamebadilika (not 100%),kuna promise kubwa yatendelea kubadilika for the better,mfano TIC wanajua wanafanya nini na sio wababaishaji na kama ni serious investor watakupatia red carpet,kama wewe ni investor nakushauri fanya kazi na hao jamaa sio wababishaji wengine watakumalizia kila kitu,kumbuka Banks nyingi ni private kwa hiyo nao sio rahisi kukutupa mteja bila sababu ingawaje mikopo bado ni very expensive na managing risk kwa TZ ni ngumu sana ndio maana sometimes nao wanakuwa wagumu kudeal na establishment zisizoeleweka
Koba,
Sidhani kama mambo yamebadilika. Mimi nimefanya kazi na TIC toka mwaka 2003 na nimeshaandika mara nyingi kwamba ni institution pekee ya serikali ambayo naona inajitahidi kufanya kazi ipasavyo. Wanaweza kuwa na matatizo yao kwa mfano kuweka nguvu zaidi kwa wageni badala ya kufanya matangazo ya maana ili hata wazawa wajue kuna chombo kama hicho. Sisi wametusaidia sana ingawaje naamini wangeweza hata kusaidia zaidi ya hapo, lakini sio mbaya.
Kuhusu banks huko ndiko kulikojaa ujinga. Wanapata pesa za bure za wafanyakazi mjini na wakisikia miradi iliyoko nje ya mjini matatizo yanaanza. Nikupe mfano kuna bank moja ya maana hapo mjini walitunyima sisi overdraft ya milioni 10 pamoja na kuwa na account nao, kupitisha kwao pesa zaidi ya milioni 100, kuwa na assets zenye thamani ya zaidi ya milioni 200 na pia kuwa na contract ya kampuni ambayo walitaka kupanga ofisi ambayo ndio tulikuwa tunaomba hizo pesa ili kumalizia haraka haraka. Wakatupotezea muda wetu bure mpaka mimi nikapata hizo pesa na kumalizia ofisi na baada ya mwezi tukalipwa.
Hiyo sio mara ya kwanza, nina mifano ya bank kibao. Kuna matatizo mengi sana kuanzia rushwa mpaka ukabila. Kuna jamaa mmoja STANBIC kazi yake ilikuwa kupitisha miradi ya kwao tu. Ukija TRA ndio kabisa, wana ku frustrate mpaka unataka kurusha ngumi.
Serikali yenyewe ndio kabisa, kuna safari nilifunga safari yangu toka UK kuja kuonana na kigogo mmoja wa serikali, nikaahidiwa nitamwona. Nilipofika, mizunguko ikaanza na mpaka likizo ikaisha hakukuwa na kitu. Nilikuwa tayari kupiga gari mpaka kumfuata kule alikokuwa mahali popote TZ, lakini hakuna kitu.
Mimi ni mwendaji wa mikutano ya investors hasa hapa UK, akina Mramba hao wababaishaji tu, anakwambia tunataka vijana kama nyie, siku ametua Dar, huwezi kumwona tena. Wanaahidi ujinga ambao hawawezi kutimiza.
Naweza kuandika kurasa 100 juu ya ujinga wa sisi Watanzania. Mimi wengine wanasena niko arrogant, sawa ukiniletea ujeuri na mimi ninakuwa jeuri. Mimi huwa nasema mtu kama mimi nisipokataa huo upuzi nani wataukataa? Nina kazi yangu ambayo ni gurantee ya maisha yangu, hivyo kila ninachofanya cha ziada hakuna pressure kubwa ya kupata faida haraka haraka, hivyo sioni umuhimu wa kutoa rushwa au kuwanyeyekea watu kama miungu.
Ninaamini nakuwa treated fairly na wazungu huku Ulaya kuliko hao ndugu zetu vigogo hapo Tanzania.
Bila ya ujinga huo kuondoka, tusitegemee maendeleo makubwa. Wewe fikiria kule ninakoinvest mimi, labda mradi wetu ndio mkubwa lakini toka tuanze sijawahi kumwona hata kiongozi wa serikali akija na kutuuliza tunaendeleaje, tuna matatizo gani nk. Unategemea viongozi wa namna hiyo ndio wafanye mabadiliko TZ? Badala yake wanafanya kila kitu kukukwamisha.Wewe nenda kawaaambie wakusaidia barua ya recomendation kwasababu inatakiwa sehemu, watakizungusha na urasimu kibao.
Wachawi wa maendeleo yetu ni sisi wenyewe. Nenda mabaraza ya wafanyabiashara yale ya akina Musiba na wengine, wanajifagilia wenyewe badala ya kuwasaidia investors vijana na wapya ili waweze kushinda urasimu wa pale mwanzoni. Kazi zio kuongozana na rais na kutoa hotuba za mambo ambayo hawayafanyi. Wacha niache maana nimelelemika sana! kwi kwi kwi!!!